Tulonge

Alichokisema Nassari kuhusu Lema kukamatwa na Polisi

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joshua Nasari

Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.

Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.

Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.

Nyumbani kwa mbunge hakai mbunge mwenyewe. Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke, ndugu etc. Utapigaje mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa mauaji. Lema si jambazi, ni kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana na mzalendo kwa taifa lake.

Hii wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological tortue.

Kama amenielewa atasikia, otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na tulishakuwa tayari, hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani arusha juni 16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu ya mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa mgumu, ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"

Nassari.
Usiku wa april 25.

VIA: Jamii Forum

Views: 732

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on April 30, 2013 at 9:35

polisi wanafanya kazi kisiasa mambo hayo yote kwa sababu yule ni mkuu wa mkoa angekua raia wa kawaida hawareact namna hiyo.

Comment by Hellen Attarsingh Gupta on April 27, 2013 at 16:28

Mimi sio mwanasiasa. Lakini kitendo cha kuizingiranyumba ya Mh. Lema na kupiga mabomu, si cha kibinadamu kabisa!!!! Wakati mafisadi wanaojulikana na kutajwa wazi wanatesa kwa raha zao, wala hawahojiwi!!!! Hakika, Yehova Mungu, atachukua hatua kwa wote wanaohusika. na hatua zake zitakuwa za HAKI kabisa.

 

Comment by David Edson Mayanga on April 27, 2013 at 13:48

KWELI KAKA NASARI INATUUMA SANA HATASIE WANACHAMA WA CCM KAM MIMI IMENIUMA SNA KWA MH .MBUNGE LEMA KUVAMIWA KTK NYUMBA YAKE NAKUVUNJA MALANGO KWELI JAMANI JE KWETU SISI RAIA TENA DO .EMWENYEZI MUNGU SHUKA FASTA UJE MWL.NYERERE AWACHAPEVIBOKO HAWA VIONGOZI KTK NCHI HII E MUNGU SAIDI TAIFA LETU.VIONGOZI KAMA HUYO MKUU WAMKOA ANAVUJISHA AMANI EMUNGU ULIYE JUU TENDA MIUJIZA

Comment by CHA the Optimist on April 27, 2013 at 9:47

ha ha ha ha ha! sina maoni zaidi ya kusema dogo kapendeza, shavu dodo.....tehe tehe tehe.

Kuhusu kukamatwa Lema, ngoja leo nikae tu kimya. Maana jeshi la Tanzania nahisi linaongozwa na mwendawazimu ndio maana hata wale wadogo nao wanakuwa na akili za kiuendawazimu.

Comment by Mjata Daffa on April 26, 2013 at 17:54

siamini na bado naendelea kuamini bado hizi ni siasa za CHADEMA Vp wavamie na mabomu usiku kwani walikwenda kutuliza ghasia? Nasari kuwa mkweli kwa maslahi ya Taifa lako usilete uchochezi

 

Comment by Dennis Lorishu Paulo on April 26, 2013 at 15:57

Ningekuwa na namba za Mh. Lema ningemuuliza kama haya ni kweli maana yana tisha na anahitaji pole.

Comment by Dennis Lorishu Paulo on April 26, 2013 at 15:54

Duh! mama yangu mzazi! ni kweli haya yametokea Tanzania? hakika hatuna viongozi, kama mkuu wa mkoa anaweza kutoa amri polisi kuvamia nyumba ya Mbunge basi amani imetoweka. Kila mtu amwombe Mungu wake atunusuru kwa janga ambayo serikali yetu wanapanda, maana naona hii ni mbegu ya kutweka kwa amani.

 

 

Comment by Mustafa Idd on April 26, 2013 at 12:08

Dah jamaani huu uongozi wa Tanzania hii?tujiangalie sana kama viongozi wenyewe wanafanyiana mambo kama haya je sisi vikaragosi?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*