Tulonge

Aliye mdhalilisha Trafiki Mwenge Dar, kufikishwa Mahakamani kuanzia kesho

Jeshi la polisi limelaani vikali kitendo cha dereva wa gari ndogo ambaye jana alimdhalilisha Askari wa usalama barabarani kwa kumkunja mkono akidai apewe funguo wa gari yake iliyochukuliwa na askari huyo baada ya kuvunja sheria.

 

Dereva huyo alifanya kosa hilo kwa kumchomekea kwa mbele dereva wa daladala hali iliyopelekea mzozo mkubwa kuzuka kati ya Dereva wa daladala na Dereva huyo wa gari ndogo. Ndipo askari alipoingilia kati na kukumbwa na mkasa huo.

 

Akiongea na ITV Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Charles Kenyela amesema wamelaani kitendo cha Dereva hilo kwani kimedhalilisha Jeshi la Polisi. Dereva huyo atafikishwa Mahakamani kuanzia kesho.

Tazama video ya tukio hilo hapo chini:-

Views: 527

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Omary on April 25, 2013 at 23:55

Unajuwa hata mkeo hutakiwi kutumia mbavu maana hata kwenye maandiko tumeambiwa tutumie lugha lain tuwabembeleze sio kutumia mbavu, mbavu hazina nafasi ktika mapenzi ila kweli madeleva wa daladala wanakera sana ila barabara zetu ndio zinafanya watu wawe hivyo ni finyu sana ndiomana watu wanavunja sheria.

@Angela unajuwa ukiwa barabarani lazima ujuwe michezo ya kihuni na unapofanya uhuni unajuwa likitokea hapa kosa litaenda wapi so angejaa yeye kosa lingekuwa kwake ndiomana kapanda ukuta kunikwepa ili jumba bovu lisimuangukie na wenyewe wanajuwa na huishia kukutukana.

Comment by ANGELA JULIUS on April 25, 2013 at 8:10

dah hii kali ila jamaa akikaa vibaya tuu jela inamngoja iwe fundisho kwa wengine, ubabe mwingine umezoea kumfanyia mkeo basi unataka hadi nje ya nyumba yako unajisahau unauonyesha haya tumbo hilo litaarudi kipara.

@Omary umenivunja mbavu lol ajae yeye siyo ha ha ha

Comment by Omary on April 25, 2013 at 5:12

kwanza deleva wa daladala inaonekana ndio zake kuwapeleka mazima maana mwenyewe kasema juzi njiapanda ya kigogo kaonyeshewa bastora means alifanya kosa kama hilohilo la kuwapelekea watu mazima so yeye nae angeadhibiwa maana tunawajuwa madeleva wa daladala walivyo wehu japo sio wote ila wengi wao wako hivyome mwenyewe siku moja kuna mmoja alikuwa nanichezea nikazidisha mwendo nikaenda mbele yake kisha nikafunga brake  ili ajae yeye ili anilipe hesabu yake ya kutwa nzima maana zilikuwa zinamchoma alishaniudhi acha ahangaike huko nyuma mpaka kapanda tuta mie nikatambaa anaishia kusema hawa watoto wa kipemba magari ya shemeji zao wanaringa nayo dadaake akiachwa hatukuoni tena barabarani lol.

Comment by eddie on April 25, 2013 at 0:18

Huyu jamaa atatia akili.

Police si wa kugusa! Ni walinda sheria ingawa police wetu wenyewe wamezoea kupokea rushwa!

Comment by salum kitila on April 24, 2013 at 22:17

kuchukuliwa hatua kwa uvunjif wa amani ni swala  muhimu kwa kila raia nchi yoyote ile,lakin kwa upande mwingine hawa ndugu zetu polisi baadhi yao huwa hawatumii lugha nzuri pale  wanapowakamata  watuhumiwa ndipo inapoleta kutoelewana pande hizi mbili hawa wa2 ka hawakujui aisee ni balaa mmh we acha.Haya bana ila ha2a kamili itajulikana.

Comment by Omary on April 24, 2013 at 21:40

Na hapo wameshampatia sababu utasikia kwanza hiri rijamaa sio riraia ripekeni kwao somalia unatupwa mogadishu ukafie huko.

Comment by Tulonge on April 24, 2013 at 21:30

Majanga mengine ya kujitakia, haya nenda kaoneshe ubabe wako kwa Pilato

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*