Tulonge

Aliye tumbukiza kichanga chooni ahukumiwa kifungo cha miaka mitano (5) jela

Rukia Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.

 

Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.

 

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.

 

Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao

ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.

 

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu

Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Kichanga kilipokua kikitolewa toka chooni

Maiti ya kichanga ikiwa kwenye beseni baada ya kutolewa chooni

 

Na Mbeya yetu blog

Views: 516

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mustafa Idd on July 13, 2013 at 21:39

Jamaaaani,hiv ninyi mnaotupa watoto kwanini mnakuwa na roho ya kikatili hivyo?mi nadhani adhabu iongezwe kwa wanaopatikana na kosa kama hili,ikiwezekana wanyongwe tuu,

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*