Tulonge

ANGALIA PICHA ZA MCHUNGAJI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ANAVYOENDELEA SASA

Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini. Hizi ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki kuamini.

sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa.

Mchungaji Umulinde. Ambapo mpaka sasa amekuwa akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu wanaoendelea kumuombea na kumtembelea hospitalini Kampala international ambako amelazwa akiendelea na matibabu pia sasa amewataka waumini wa dini ya kikristo kuendelea kuwaombea wenzao ili wamjue Mungu wa kweli kuliko kuendelea na malumbano nao kwakuwa hakutakuwa na faida yoyote.

Mchungaji Umulinde akiwa nje ya hospitali kupunga upepo,picha juu baadhi ya marafiki waliomtembelea hospitalini.

Mchungaji Umulinde kabla hajakumbwa na tukio la tindikali

Hapa akiwa kwenye moja ya mikutano aliyoiendesha nchini Uganda.

NB: SOURCE - GOSPLE KITAA!!

Views: 1175

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on April 18, 2012 at 9:45

POLE SANA KAKA!

Comment by Bonielly on March 5, 2012 at 16:37

du binadamu ni mnyama hatari kuliko simba, nyoka, hata chui, binadamu ni mnyama mkatili sana, du, amemsababishia kilema mchungaji, mungu yeye ndie hakimu,

Comment by Tulonge on March 3, 2012 at 0:18

Hata sielewi niandike nn,pole mchungaji.

Comment by Wa Kimberly on March 3, 2012 at 0:10

Jamani jamani,kwanini binadamu wengine wamekuwa na roho ya kikatili kiasi hichi??

ee mungu mponye wanao.

Comment by Alfan Mlali on March 2, 2012 at 21:31

Inna Lillah wanna illayh turjaghoon. Binadamu wengine wana roho mbaya kushinda hata wanyama!!

Comment by manka on March 2, 2012 at 18:14

huuu! sina la kusema Mungu wetu ni mwema atamponya na na atakulipia kwa wote waliokutenda ubaya huo, zidisha sala na usichoke kuhubiri neno la MUNGU.

Comment by Mama Malaika on March 2, 2012 at 17:56

OMG! Hii imetokea lini DIXON? Na hao waliomwagia tindikari wameshikwa na vyombo vya dola?

Mungu hapendi watu wake tufanyiane vitendo kama hivi vya mauaji. Hiyo tindikali tosha kumtoa roho mtu. Dini karibu zote duniani iwe Taoism, Buddhism, Rastafari, Judaism, Islam, Shinto, Santeria, Christianity, Druidism, Baha'i, etc. zote zatufundisha UPENDO & UVUMILIVU

Comment by ANGELA JULIUS on March 2, 2012 at 16:29

DAH NIPO SPEACHLESS MMMMM LOL NAUNGANA NANYI NYOTE MLIOCOMMENT BEFORE ME. MUNGU KWA MAPENZI YAKO MPONYE KIUMBE WAKO HUYU.

Comment by Dixon Kaishozi on March 2, 2012 at 13:46

Yani kuna maswali mengine ndugu yangu tunakosa majibu.. @ Chalii

Comment by ILYA on March 2, 2012 at 13:37

oo God,wanadamu ni wabaya sana jamani,hivi huyo aliyemsababishia yote hayo atasema nini Mwenyeezi Mungtu (s.w) akimuuliza?!....

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*