Tulonge

Anthery Mushi azikwa bila huduma ya Kanisa

Mwili wa marehemu Anthery Mushi umezikwa kijijini kwao Ongoma bila huduma ya kikanisa. Familia ililimuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo ili aridhie familia ya Anthery isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.

 

Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.

 

Watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha ibada kutokana na taratibu za kanisa za kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya Anthery.

 

Mtoto wa marehemu Alvin Anthery (ambaye alizaa na Ufoo), hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.

 

Hata hivyo, hali ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana, ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery.

 

Kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo: “Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya kilichotokea maana mtbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana na habari zinazotangazwa. Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.

 

Anthery Mushi (40) alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe, Anastazia Saro, na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, (mtanzangaji wa kituo cha televisheni cha ITV), huko nyumbani kwao, Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 

Chanzo: NIPASHE

Views: 668

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on October 27, 2013 at 17:19

Pole yake

Comment by habiba mustafa mlawa on October 22, 2013 at 8:17
umeona ee Mjata anaehukumu ni Mungu peke yake nyie mtamhukumuje mtu, kama wewe ni mwema na huna hata dhambi moja ndo unaruhusiwa kufanya hivyo unless otherwise unakamilisha taratibu zote zinazohitajika kama ni za kanisani au Msikitini mengine mwachie mwenyewe Muumba
Comment by Mjata Daffa on October 21, 2013 at 9:43

Hiyo sheria ni ya mungu au ya kanisa? katika uislam, mtu anaekufa bila kujali kafaje anahaki ya kutendewa mambo ma 4 na walio hai:-

1. Kuoshwa

2. Kuvalishwa sanda

3. Kuswaliwa/Dua

4. Kumzika

msipofanya mambo hayo 4 hata kama marehemu alijiua mwenyewa eneo/Kijiji chote mnapata DHAMBI. 

Sasan huyu Anthery mwisho wasilku alizikwa kwa imani gani? au walimfukia kienyeji tu?

Comment by Tulonge on October 20, 2013 at 17:14

Duuh! kumbe ni hivyo Baraka? sikua najua kabisa

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on October 20, 2013 at 9:52

Sheria za Kanisa Katoliki ukijiua tu, hupati huduma hiyo. Tena ukizingatia ameua na mwingine.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*