Tulonge

Anunua Kg 10 za sembe kwa Sh70M mwingine atoa Sh200M ili izae mara mbili

Na Peter Fabian, New Habari, Mwanza — WATU sita wametapeliwa katika matukio tofauti mkoani Mwanza, akiwamo mmoja aliyenunua kilo 10 za unga wa sembe kwa thamani ya Sh milioni 70 akidhani ni madini ya rubi (green tourmaline) na mwingine kutoa Sh milioni 200 akitaka zizalishwe ajipatie Sh milioni 400. Matukio hayo ambayo ni ya kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu yamesababisha watu mbalimbali kutapeliwa Sh milioni 309.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa akitoa taarifa za matukio hayo jana kwa waandishi wa habari ofisini kwake, alisema kuwa ,baadhi ya matapeli waliokamatwa wameisha fikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kusakwa.

Katika tukio la hivi karibuni mwezi uliopita, mwananchi mmoja maarufu jijini Mwanza (hakutajwa) mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, alinaswa na mtego wa matapeli hao na kujikuta akiuziwa kilo 10 za unga wa sembe ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye mkoba ikidaiwa ni madini ya rubi (green tourmaline).

“Huyu alilazimika kuuza nyumba yake Mwanza na kwenda na matapeli hao hadi Morogoro ambako alionyeshwa madini hayo na kutoa fedha na kisha kufungiwa kwenye mkoba bila kutakiwa kulifungua hadi atakapofika Mwanza na kukaa siku saba vinginevyo angekiuka masharti na kukuta majini.” alieleza Konyo.

Kamanda alisema baada ya siku tatu, mwananchi huyo aliwapigia simu wauzaji akitaka kufungua lakini walimzuia kuwa asubiri hadi watakapomueleza, akilazimisha atakuta majini, hali iliyomfanya akimbilie polisi kuomba msaada wa kuufungua mkoba na ndipo ilipobainika kulikuwa na unga wa sembe na si madini.

Tukio jingine linamhusu mkulima aliyeuza nyumba yake kwa Sh milioni saba na fedha hizo kuuziwa chupa ya dawa feki ya kuhifadhia mazao ambayo alidanganywa kuwa angeweza kuiuza kwa wakulima wenzake kwa Sh milioni 100 na kwamba dawa hiyo inatafutwa na wazungu na inapatikana katika Chuo cha Utafiti Ukiriguru pekee.

“Mwingine aliuziwa chupa tatu za chuma zilizojazwa kokoto na saruji, kwa thamani ya Sh milioni 26, akidanganywa kuwa ni za zebaki ya kuoshea dhahabu na mwingine akadanganywa asiweke fedha benki ili wamuuzie dhahabu lakini akauziwa gorori za baiskeli kwa Sh milioni sita baada ya kuonyeshwa vipande vya kufuli vilivyosagwa na kung’aa kama dhahabu,.” alisema Konyo.

Kamanda alisema tukio jingine ni la mwananchi mmoja aliyeuza nyumba yake kwa Sh milioni 200 baada ya kudanganywa kuwa fedha zake zingeweza kuzalishwa mara mbili na kuziweka kwenye boksi la mganga mmoja ili zifikie Sh milioni 400, matokeo yake alibiwa na watuhumiwa na kesi iko mahakamani.

Alisema tukio la mwisho ni mwanamke mfanyabiashara aliyejikuta akibakwa, kulawitiwa na kuibwa fedha (hazikutajwa) baada ya kufanya mazungumzo katika chumba cha hoteli moja jijini hapa na kujikuta akinyweshwa madawa ya kulevya na watu hao waliojitambulisha kwake kuwa ni wafanyabiashara kutoka miji mikubwa.

Kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza kuwa macho na matapeli hao ambao wakati mwingine hutumia majina ya viongozi wa ngazi za juu wa mkoa na taifa.

via: wavuti.com

Views: 810

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Omar on November 7, 2013 at 20:55

duh! kumbe afadhali mimi niliuziwa msikiti! nikaamua kukata vyumba na kupangisha lakini hawa wao wameuziwa bahari

Comment by ANGELA JULIUS on November 6, 2013 at 13:11

Habiba soma maelezo yangu siku zote huwa napenda mzaha mwingi ila kwa hili limenikumbusha mbali kidogo yani unatoa chochote ulicho nacho na kumbuka mganga hajigangi na wanayo masharti yao wayajuayo wao wenyewe. shukuru Mungu na uzidi kumwomba Mungu watu hawa wasiingie anga zako yani wakiamua hadi chupi uliyovaa wanakuvua na wewe mwenyewe ndo utakayevua na kuwapa.

Comment by Tulonge on November 6, 2013 at 10:39

Thanx Angela kwa kutujuza mengi, nilikua nafahamu machache kuhusu hawa jamaa.Ni hatari

Comment by habiba mustafa mlawa on November 6, 2013 at 8:51
jamani mi nasema kila siku huyo mganga wa kukupa wewe hela zaidi inamaana yeye hazitaki kabla hatujafanya maamuzi tutafakari kwanza na kuomba ushauri pesa nyingi kama milioni mia mbili unatoa tu from now where eti upate million mia 4 jamani jamani
Comment by ANGELA JULIUS on November 6, 2013 at 8:00

KUNA KIPINDI WALIKUWA WANAPITA HASA KWENYE MAJUMBA YA WATU NA KUWADANGANYA WASICHANA WA KAZI AU YOYOTE WANAYEMKUTA NYUMBANI NA HAYO YOTE NI MAZINGARA YANAFANYIKA DADA ATOA KILA KITU NYUMBA YABAKI NYEUPEEE BADAYE WAMEONDOKA NDO ANAPATA FAHAMU HEE KUMBE NILIKUWA ULIMWENGU MWINGINE BASI TENA NDO HIVO JAMAA WAMESHAONDOKA.

NAKUMBUKA JIRANI YETU ALIMWACHIA MSICHANA WAKE WA KAZI AMSAFISHIE CHUMBANI KWAKE NA HUWA SIKU ZOTE CHUMBA ANAFUNGA YULE DADA KASAFISHA VIZURI YUPO AENDELEA NA KAZI ZAKE ZA NYUMBANI AKASIKIA HODI AKAENDA KUWASIKILIZA WAGENI DAH ALITOA DHAHABU ZOTE ZA YULE MAMA TENA SIKU HIYI YULE MAMA HADI PETE YAKE YA NDOA NA UCHUMBA ALISAHAU KUVAA KIUKWELI YULE MAMA ALIKUWA ANAVAA DHAHABU ZA UKWELI TENA ZILE SPECIAL SIYO ZA KUCHONGA  LOL YULE DADA ALITOA ZOTEEE YULE MAMA ANADAI ZILIKUWA KAMA ZA 4 MILLION KUHAMAKI YULE DADA ANAPIGA YOWE MAJIRANI TUNATOKA  NDO ANATUPA HABARI TUKAMPIGIA YULE MAMA SIMU HAKUAMINI ALIKUJA MBIO KUFIKA NA KUSHUHUDIA HAMNA KWELI NDO MARA YANGU YA KWANZA KUONA MTU AKAPANDISHA MASHETANI WAKAITA MASHEIKH KWANI NI KARIBU NA MSIKITINI WAKAJA WAKAMFANYIA DUA ZAO LKN KIUKWELI YULE MAMA ALIPAGAWA

Comment by ANGELA JULIUS on November 6, 2013 at 7:50

HAWA WALIOTAPELIWA NAIMANI HADI SASA WATAKUWA WANAJIULIZA ILIKUWAJE KWANI MBINU HIZI ZA KISHIRIKINA ZA KUTAPELI WATU ZIPO NA ZINAFAHAMIKA NIMESHAMSHUHUDIA TAPELI KAPEWA KISAGO NA WANANICHI KIDOGO KUFA POLICE WAKAJA KUMUOKOA ILE ANAMALIZA KUTOA MAELEZO YAKE TU PALE POLISI NA JAMAA ALIKATA ROHO KWANI ALIKUWA NA INTERNAL BREADING YULE TAPELI ALISEMA HUWA WANATUMIA UKUCHA WA SIMBA KUMTAMBUA MTU ALIYEKUWA NAZO NA ASIYE NACHO ULE UKUCHA AKIUKUNJA UKIKUBALI BASI YULE MTU ANACHO UKIKATAA BASI YULE MTU HANA KITU NA NDO MANA HUMU KWENYE KUGOMBANIA USAFIRI WENGI WANAIBIWA KWA STYLE HIYO NA WANAHAKIKISHA WANAKUFUATILIA HADI WANAKUPORA KAMA SI KUKUPIGA FINGER. PIA KWA WALE WANAOPIGISHWA STORY HADI KUUZA KILA WALICHONACHO ALISEMA HUWA KUNA DAWA WANAIPAKA MKONONI WANAINUIZIA THEN UKIMPA MKONO TU AU UKIKATAA KUMPA MKONO AKIFANIKIWA HATA KUKUSHIKA POPOTE KWENYE MWILI WAKO IMEKULA KWAKO KWA KWELI WATU MACHO YALITUTOKA ILA JAMAA NDO ULIKUWA HUMWANGALII MARA MBILI NA HUWA WANAVAA HIRIZI KWANI ALIWAONYESHA WALE POLISI KANZU WALIOKUWA WANAMUHOJI NA ILIPOVULIWA ILE HIRIZI JAMAA ALIKATA ROHO. HATA KILICHONIPELEKA PALE KWA KWELI ILIBIDI NIRUDI KESHO YAKE KUENDELEA NACHO KWANI NILIOGOPA SANA.

Comment by ANGELA JULIUS on November 6, 2013 at 7:37

WADAU WENZANGU TENA NAOMBA MTEME MATE CHINI NA UMSHUKURU MUNGU HAWA WASHENZI MATAPELI HAWAJAKANYAGA ANGA ZAKO KIUKWELI HUWA WANATUMIA DAWA ZA KUPUMBAZA KWA MUDA FULANI NDO MAANA MUHUSIKA ANAKUJA KUGUNDUA BADAYE KUWA KATAPELIWA CHA MSINGI UKITAKA KUWAKOMESHA HAWA WASHENZI ILE WAMEKUJA NA SWAGA ZAO ZA KUKUSOMESHA WASTOPISHE KABLA HAWAJAKUSHIKA MAHALI HUWA WANA SEHEMU WANAKUSHIKA BASI KUANZIA HAPO NDO UNAANZA KUPOTEZA UELEKEO NA KUUZA KILA ULICHONACHO NA KUTOA KILA ULICHONACHO

Comment by Omary on November 6, 2013 at 2:19

Mie nitamuonea huruma mtu aliekabwa kama Dismas ila huyo alietowa mwenyewe kwa akili mbovu wala simuonei huruma naiwe fundisho akauze na shamba lililobaki ampelekee tena huyo tapeli aziongeze.

 

Comment by Omary on November 6, 2013 at 2:16

Ila watu wengine niwapuuzi utauzaje? nyumba ukampelekea mtu aizalishe yeye amekuwa kiwanda? Isee hainiingii akilini eti wanakufungia kwenye mfuko nenda ukafungulie mbali hivi huu msemo wa kiswali kabisa mbuzi kwenye gunia hawaujui? yaani mie mtu atemane na mimi kabisa hata asisogee kuniletea upuuzi eti mganga?! si aingie bank bila kumuona akazichote atakazo.

Comment by Tulonge on November 5, 2013 at 20:58

Huwa sielewi kama hawa matapeli huwa wanatumia dawa au vp?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*