Tulonge

Anunua Kg 10 za sembe kwa Sh70M mwingine atoa Sh200M ili izae mara mbili

Na Peter Fabian, New Habari, Mwanza — WATU sita wametapeliwa katika matukio tofauti mkoani Mwanza, akiwamo mmoja aliyenunua kilo 10 za unga wa sembe kwa thamani ya Sh milioni 70 akidhani ni madini ya rubi (green tourmaline) na mwingine kutoa Sh milioni 200 akitaka zizalishwe ajipatie Sh milioni 400. Matukio hayo ambayo ni ya kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu yamesababisha watu mbalimbali kutapeliwa Sh milioni 309.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa akitoa taarifa za matukio hayo jana kwa waandishi wa habari ofisini kwake, alisema kuwa ,baadhi ya matapeli waliokamatwa wameisha fikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kusakwa.

Katika tukio la hivi karibuni mwezi uliopita, mwananchi mmoja maarufu jijini Mwanza (hakutajwa) mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, alinaswa na mtego wa matapeli hao na kujikuta akiuziwa kilo 10 za unga wa sembe ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye mkoba ikidaiwa ni madini ya rubi (green tourmaline).

“Huyu alilazimika kuuza nyumba yake Mwanza na kwenda na matapeli hao hadi Morogoro ambako alionyeshwa madini hayo na kutoa fedha na kisha kufungiwa kwenye mkoba bila kutakiwa kulifungua hadi atakapofika Mwanza na kukaa siku saba vinginevyo angekiuka masharti na kukuta majini.” alieleza Konyo.

Kamanda alisema baada ya siku tatu, mwananchi huyo aliwapigia simu wauzaji akitaka kufungua lakini walimzuia kuwa asubiri hadi watakapomueleza, akilazimisha atakuta majini, hali iliyomfanya akimbilie polisi kuomba msaada wa kuufungua mkoba na ndipo ilipobainika kulikuwa na unga wa sembe na si madini.

Tukio jingine linamhusu mkulima aliyeuza nyumba yake kwa Sh milioni saba na fedha hizo kuuziwa chupa ya dawa feki ya kuhifadhia mazao ambayo alidanganywa kuwa angeweza kuiuza kwa wakulima wenzake kwa Sh milioni 100 na kwamba dawa hiyo inatafutwa na wazungu na inapatikana katika Chuo cha Utafiti Ukiriguru pekee.

“Mwingine aliuziwa chupa tatu za chuma zilizojazwa kokoto na saruji, kwa thamani ya Sh milioni 26, akidanganywa kuwa ni za zebaki ya kuoshea dhahabu na mwingine akadanganywa asiweke fedha benki ili wamuuzie dhahabu lakini akauziwa gorori za baiskeli kwa Sh milioni sita baada ya kuonyeshwa vipande vya kufuli vilivyosagwa na kung’aa kama dhahabu,.” alisema Konyo.

Kamanda alisema tukio jingine ni la mwananchi mmoja aliyeuza nyumba yake kwa Sh milioni 200 baada ya kudanganywa kuwa fedha zake zingeweza kuzalishwa mara mbili na kuziweka kwenye boksi la mganga mmoja ili zifikie Sh milioni 400, matokeo yake alibiwa na watuhumiwa na kesi iko mahakamani.

Alisema tukio la mwisho ni mwanamke mfanyabiashara aliyejikuta akibakwa, kulawitiwa na kuibwa fedha (hazikutajwa) baada ya kufanya mazungumzo katika chumba cha hoteli moja jijini hapa na kujikuta akinyweshwa madawa ya kulevya na watu hao waliojitambulisha kwake kuwa ni wafanyabiashara kutoka miji mikubwa.

Kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza kuwa macho na matapeli hao ambao wakati mwingine hutumia majina ya viongozi wa ngazi za juu wa mkoa na taifa.

via: wavuti.com

Views: 812

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on November 5, 2013 at 17:25

Aisee! Kumbe ndio hivyo. Ok. Ok. Ok.

Ila mimi kutapeliwa kipumbavu kama hivyo--iti iz noti posibo.

Comment by Mama Malaika on November 5, 2013 at 17:18
AMA kweli mjini shule, usione watu wana maisha mazuri na kuendesha gari ya 200million ukasema wote wanazi pata kwa jasho kumbe wengine wanazipata kiulaini, mtu apata 70mil kwa kilo 10 za sembe. That's incredible. Kuna watu wana roho ngumu sana, hawaogopi kuokota makopo na kuvaa chupi kichwani.
Mie siwezi uza nyumba niliyojenga na kuitolea jasho kuanzia asubuhi hadi jioni nachanganya zege eti nipate mtaji wa biashara.
Comment by ANGELA JULIUS on November 5, 2013 at 16:17

dah viini macho vipo as you commented my kibelaaaa always short cut is wrong cut

Comment by Dixon Kaishozi on November 5, 2013 at 15:53

Mhhh.. Kweli watu tunapenda "short-cut" ya kupata fedha nyingi kwa mara1 bila kuzifanyia kazi halali - nakumbuka kuna msemo usemao "always short cut is wrong cut" . Hili ni somo kwa wana kijiji wenzangu tuwe makini na tujishughulishe!!!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*