Tulonge

Bajeti ya bilioni 11.1 yapitishwa kukamilisha maziko ya Mandela

Bendera zikipepea nusu mlingoti mbele ya Bunge huku Cape Town Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mzee Mandela.

 

Bajeti ya Land 72 millioni ambazo ni sawa na sh. 11.1 bilioni za Kitanzania zimepitishwa na Baraza la jiji la Cape Town kwaajili ya maandalizi na kukamilisha zoezi zima la maziko ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefariki wiki iliyopita.

 

Soma zaidi

 

Views: 999

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 22:00
Na miezi 6 ijayo kuna uchaguzi mkuu South Africa. Ingawa utawala wa Jacob Zuma umefanya education standard and public health care system kuwa mbaya, rising poverty and unemployment lakini bado majority of black South Africans wako radhi kumpa kura Jacob Zuma sababu wanaona ANC ndio iliyowakomboa from Apartheid, wanasahau kuwa ma comrades wa kweli wa ANC waliokuwa na uchungu na nchi yao wametangulia (kufa) na hao waliobaki ndani ya ANC ni mafisi na waroho wamesababisha matabaka na ukabila.
Na hii ndio mindset that will prevail far beyond the life times of our grandchildren. It is easier to blame apartheid, colonial rule and the White man for the many ills that affect not only South Africa and Zimbabwe but Africa as a whole, than to stand up and accept responsibility and move forward.
Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 21:51
Dixon... ANC has lost itself in Zuma. Nkandla (hiyo nyumba yake) imeleta mzozo sana. Baada ya mgomo wa wachimba migodi niliangalia LIVE debate (on Channel 4-TV) jinsi Zuma alivyo hojiwa kuhusu wananchi kukosa imani na utawala. Aliulizwa mambo mengi ikiwemo wapi kapata pesa ya ujenzi wa Nkandla inayozidi mapato yake, mkewe mdogo kumiliki ndege, mkewe mwiingine mdogo kulipwa millions of US$ from South African government kwa tender hewa, mtoto wake wa kiume kuwa na 30% share kwenye migodi 2 mikubwa ya madini ambako mgodi mmoja wachimbaji weusi walipigwa risasi kufariki na police baada ya kugoma. Bado Guptagate scandal (mfanya biashara wa kihindi rafiki wa Zuma). Zuma alikuwa ajikanyaga kujibu maswali. Inatia hasira sana jinsi viongozi wanavyogeuza nchi kama mali yao na families zao.
Comment by Dixon Kaishozi on December 12, 2013 at 14:15

@ MAma Malaika.... Niliona mchambuzi wa siasa wa SA akieleza kilichotokea!!!! Kushangiliwa kwa Obama na Kuzomewa kwa Zuma kunatokana na huyo bwana Kuto Kumuenzi Mandela kwa vitendo toka aliposhika nchi hadi sasa!!! Kwa habari tu ni kwamba Zuma Kajijengea mjengo wa zaidi Billion 300!!!! mbona Madiba hakuwa hivyo ? mbali na hapo ana kashfa za ndani kwa ndani kwa Watu wake anao waongoza wa S.A . Walichokuwa wanakifanya ni kuuonyesha ulimwengu juu ya yale anayoyafanya.. Kufa kwa Mandela imekua sherehe kwa watu wa Africa Kusini kuonyesha huzuni yao kwa njia ya furaha wakitaka Baba yao Madipa Apumzike kwa amani kwani alisha kamilisha kilichomleta Duniani. 

Hayo ni maoni/mtazamo wa mchambuzi wa siasa . S.A

Comment by jemadari mimi on December 12, 2013 at 10:31

Mama malaika najua unafahamu juu ya maisha ya waafrika,jinsi tunavyoishi ktkt nchi zetu hizi.ebu niambie wasauzi wanajua anachofanya zuma na hawana sehemu ya kusemea zaidi ya hapo kwa kuonyesha hawana imani naye.tujiulize kwanini wasifanye hivyo kwa mzee mbeki au askofu tutu,hapo lzm kuna kitu alichowakosea na ndio maana wanamzomea,ni kweli kwamba niaibu kwenye msiba kufanya mambo kamahaya ya kuzomea viongozi wa nchi,ni aibu kwa ANC na serikali ya afrika kusini lkn siaibu kwa wananchi wa taifa hilo kwa walichokidhamiria wametimiza.

mama malaika hili ni fundisho kwa wale viongozi wanaofanya mambo kinyume na taratibu zilizowekwa,nawaomba viongozi kujifunza kwa yale yaliomtokea zuma  

Comment by Mama Malaika on December 11, 2013 at 18:54
Jana nimeangalia shughuli ya mazishi mwanzo hadi mwisho, sikufurahishwa kuona wananchi waliokuwa ndani ya uwanja wanazomea raisi wao Jacob Zuma alipoingia, na bado ile akionyeshwa asalimiana na mtu wanazomea. Kuna kipindi Askofu Desmond Tutu na ANC deputy Mr Ramaphosa ilibidi waingilie kati wakatoa sauti ya ukali kuwakataza watu kuzomea. Hata Kama raisi wao hawampendi ni aibu kubwa ukizingatia hiyo ilikuwa ni sherehe ya Mandela, mtu wa amani. Na sherehe ilikuwa yarushwa LIVE duniani nzima tunaona
Comment by Mama Malaika on December 11, 2013 at 18:29
Tayari kuna kashfa imeibuka kuhusu mtu aliyekuwa pale mbele kwenye jukwaa akitafsiri (sign language) hotuba kwa viziwi zilizokuwa zikisemwa/tolewa na waalikwa pale jukwaani ikiwemo hotuba ya raisi
Obama. Kwenye kashfa hii yasemekana huyo bwana kaletwa na mtu mwenye cheo ndani ya ANC na amelipwa pesa toka kwenye budget ya mazishi ili asimame pale jukwaani wakati hana ujuzi wa facial expression ambao watakiwa kwa watu wa sign language, na chama/shirika la viziwi la South Africa linadai kuwa mtu huyo hakuwa anaeleweka vizuri kitu ambacho kimefanya walemavu hao/viziwi kutokuelewa hotuba kwa ujumla.
Chama/shirika hilo laviziwi lasema kwamba mtu huyo jina lake halijasajiliwa na wala hawamjui. Chama cha viziwi kina dai kuwa kwa wao kutuma mtu wao kutoa huduma hiyo ingekuwa bure ukizingatia Mandela ni baba wa taifa.

Habari imetolewa kwa ufupi kwenye mainstream media (CNN) ila hawajaelezea kiundani, ukitaka undani soma media za South Africa (iol, soweto, etc.). Hii ndio Africa yetu isiyojulikana na wengi. It's sad but true.
Comment by Omary Maftuhi Mwinshekhe on December 11, 2013 at 18:19

Angela ni hao hao Marekaaaaaaa na Uingereeeeeeee ndio walikuwa wanaikandamiza na kuinyonya SA, lakini sisi tulioikomboa hatuonekani.

Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 17:40
Tenaaaaaa Omaryyyyyyy nani anamjua pale, pale ni marekaaaaaaa na Uingereeeeeee ndo hapo ujue kuwa .............................. habari ndo hiyo kule wanaonekana kama mimi na wewe tungekwaa pipa tukashuhudie mazishi ya mpendwa wetu tata Madiba.
Comment by Omary Maftuhi Mwinshekhe on December 11, 2013 at 17:25

Nasikitika Mkuu wa nchi iliyopambana kwa hali na mali kuhakikisha Afrika Kusini inakuwa huru hakupewa nafasi japo aseme chochote, Any way RIP MADIBA

Comment by ANANGISYE KEFA on December 11, 2013 at 17:11

iwe bajeti kubwa au ndogo hiyo ni wao wenyewe, cha muhimu hapa ni alama yetu halisi ya upendo na amani tata madiba mandela anaenda kupumzika kwa amani.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*