Tulonge

Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini

Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.

 

Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.

 

Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.

 

Chanzo: ITV

Views: 591

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Wa Kimberly on December 10, 2013 at 11:55
Mwanzo mzuri maana yanaweza kupeba abiria wengi kwa mara moja.
Comment by Mama Malaika on December 7, 2013 at 15:09
Mbona basi la kawaida tu kama nayoyaona baadhi ya miji ya UK, France, Netherlands, etc. basi waliposema ya mwendo wa kasi nilifikiria yanayotumia umeme.
Comment by Hellen Attarsingh Gupta on December 7, 2013 at 10:49

Hongera Serikali kwa kutuletea bus la kwanza liendalo kasi. Pia kama mtatupunguzia kodi tutashukuru sana. Tena tunakuwa tunalipa kodi mara kadhaa kwenye maeneo mbalimbali.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*