Tulonge

BBC Documentary - The Chinese Are Coming ; Hapa nimeshikwa na hasira.....ndugu zangu jamani....tuamke...machozi!

Views: 573

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by manka on December 22, 2011 at 21:12

wapo wachina na watanzania wa kiume na wa kike Mama Malaika, na wanasema wateja wao wakubwa ni watu wenye pesa zao na wakubwa wa serikalini yaani wewe acha tu.

Comment by Mama Malaika on December 22, 2011 at 21:08

Asalaleeee! Yaani wachina wamefikia hatua hiyo Tanzania? Sasa hiyo extra massage inatolewa na mchina au ni mtanzania mweusi kaajiliwa hapo?

Comment by manka on December 22, 2011 at 20:59

kweli kazi kweli kweli mama Malaika, kuna kipindi kiliwahi kurushwa na TBC kinaitwa usiku wa habari kipindi hawaja msimamisha Jerry Muro kwa tuhuma za rushwa, wanawake wa kichina wanaendesha madanguro jijini Dare es salaam, wanafungu masagi senta matkeo yake kuna masagi inaitwa extra masage sasa ni uamuzi wa mteja kuchagua kama unataka extra ndiyo unamaliza mambo yako yote huko kama ni mwanamke unashughulikiwa na mwanaume na kama ni mwanaume unashughulikiwa n

na mwanamke. yaani ni uozo mtupu.

Comment by Mama Malaika on December 22, 2011 at 20:44

Kesi nyingi zihusuzo wageni kuwaonea raia nchini Tanzania huwa hazifiki mbali. Halafu ukumbuke kuwa wachina kwa corruption ndio wenyewe ingawa wanajifanya kwao haipo.

Olivia hao ndio zao kutolipa ujira kwa watu wanaowafanyia kazi. Hata huko kwao uchina wana kasumba hiyo na ni kitu cha kawaida, ule uwanja mkubwa mashuhuri uliotumika kufanyiwa sherehe za Beijing Olympic 2008, mwaka huu mwezi July kuna watu waliohusika kujenga uwanja huo bado walikuwa wanadai malipo yao. Na wale waliofanya maandamano ya kudai malipo yao wametiwa magerezani na serikali ya uchina.

Nasikia hiyo pia ndio inachangia kwa serikali ya uchina kumkalia shingoni mwana harakati wa haki za binadamu wa huko uchina Mr. Ai Weiwei kwani naye alihusika na naku-plan na kuuchora ule uwanja wa Beijing Olympic.

Kazi kweli kweli....

Comment by manka on December 22, 2011 at 20:21

wanaroho mbaya sana mama malaika, walikuwa wanajenga barabara ya minjingu wanachapa watu bakora kabisa wanapodai pesa zao za vibaru wakiulizwa wanasema waliwavamia, kuna kijana alishikwa na hasira akawafuata na panga matokeo yake walimpiga kwa kumchangia mpaka akauawa, kesi sijui imeishia wapi,  wao wanadai kijana alienda kupora mali zao, wamemjaza mimba mwanafunzi alipoenda kumwabia mchina akampiga mtoto wa watu matokeo akapoteza ujauzito na kesi ipo mahakamani, TZ inavyowaona hawa watu kama Miungu wao matokeo tutaambiwa  mtuhumiwa hana hatia.

Comment by Mama Malaika on December 22, 2011 at 19:49

Umeona enhee Olivia... hapo baadae tutatawaliwa na kupigwa bakora na wachina, na wachina walivyo wakorofi na roho mbaya huko kwao wao kwa wao itakuwaje kwetu sie weusi? History inajirudia, wakoloni waarabu walianza kuja Africa wakatutawala na hawajaondoka hadi leo. Wazungu nao wakaja taratibu na kimya kimya, walianza kuja kama missionaries (e.g. Dr Livingstone) na baadae wakajazana kututawala na kutugawa (mipaka ya nchi) na legacy waliotuachia ni vita na mifarakano isiyoisha.

Comment by manka on December 22, 2011 at 19:15

mbona wachina wapo tangu siku nyingi Gratious, huku tanzania kwa sasa ndiyo wamejaa kama nini na wanamaduka ya kuuza bidhaa ndogo ndogo kama wenyeji, siku za nyuma  walikuwa wanakuja kwa sababu ya kutengeneza miundo mbinu ya barabara lakini kwa sasa wanafanya biashara za kawaida sana ambazo zingepassa kufanywa na wazawa, kwa mfano kariakoo wamejazana pale wanauza maua na mapambo ya ndani. huku Moshi wamefungua migahawa ya kawaida sana ambayo haifikishi hata thamani ya milioni kumi, na sasa wanafungua makanisa ya kilokole yanaitwa breziberin church na makanisa hayo wanayafungua kwenye makazi ya watu. serikali ya Tanzania inachekelea na inawaita wawekezeji na kuwamwagia sifa kibao kwamba kwa sasa wana ufa dhili mkubwa kwa Tanzani. huko tuendako tutatawaliwa upya kimabavu tofauti na sasa wanakuja kimyakimya.

Comment by Mama Malaika on December 22, 2011 at 17:29

Gratious ina maana wewe ulikuwa hujui? Sio kwamba "The Chinese are coming", bali yapasa useme "The Chinese are here with us for nearly three decades". Ukisoma Economics ndio utachukia na kushikwa hasira zaidi... kwani wachina walianza kuingia Africa taratibu miaka ya 1980s, walikuwa miji mikubwa ya Africa wakifanya biashara na wengine kumiliki construction companies, na viongozi wetu wa kiafrika waliwapenda wachina na kuwaona ni marafiki wa kweli. Hadi kufikia mwishoni mwa 1990s ndio wakaanza kujitanua kwenda miji midogo na baadae vijijini.

Unakumbuka uchumi wa Zambia ulipoanguka kipindi cha raisi Chiruba? Wachina ndio walioathirika sana na ile ciris na kipindi hicho kila kona ya Zambia ilikuwa na wachina wanalima kuanzia vitunguu na maharage vijijini hadi biashara ya machimboni kule Copper Belt na biashara ya meno ya tembo, vifaru na ngozi za chui. 

Libya tu kwenye mwaka huu wakati wa vita, unaambiwa more than 50% ya wageni waliokuwepo nchini Libya walikuwa ni wachina. Na wengi wao hawakurudi China bali wamekimbilia nchi za west Africa. Mwaka 2009 niliwapeleka watoto na mume wangu kumuona babu yangu Malawi, tumekuta  wachina wametapakaa Malawi nzima, tena wana mashamba na migogoro ya ardhi ndio inazidi kwani viongozi wa Malawi wamewanyang'anya wenyeji mashamba yao na kuwapa wachina. Na hao wachina wamejichanganya na wanaongea Chichewa na Chitumbuka kama hawana akili nzuri, kiingereza hawakijui

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*