Tulonge

Binti wa miaka 16 anaswa akijiuza na mwanae mgongoni

Ama kweli shida haina aibu wala huruma! Binti wa miaka 16 aliyetajwa kwa jina la Mama K, amenaswa laivu akifanya shughuli haramu za uchangudoa akiwa na mwanaye mgongoni, akidai chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na shida inayoiandama familia yake. Binti huyo alibambwa hivi karibuni akijiuza huku mgongoni akiwa na mwanaye wa mwaka mmoja katika Barabara ya Uhuru (kwenye taa za kuongozea magari), jijini hapa.

Ama kweli shida haina aibu wala huruma! Binti wa miaka 16 aliyetajwa kwa jina la Mama K, amenaswa laivu akifanya shughuli haramu za uchangudoa akiwa na mwanaye mgongoni, akidai chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na shida inayoiandama familia yake.

Binti huyo alibambwa hivi karibuni akijiuza huku mgongoni akiwa na mwanaye wa mwaka mmoja katika Barabara ya Uhuru (kwenye taa za kuongozea magari), jijini hapa.

Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambayo imetinga rasmi mkoani hapa ilinasa tukio hilo usiku wa manane ambapo ilifanikiwa kufanya mahojiano na Mama K aliyekuwa na wenzake wengi walio chini ya miaka 18.

OFM ilichukua maelezo pamoja na picha za mnato huku wenzake wakitoka nduki baada ya kuona mwanga wa kamera.

Cha kushangaza, wakati akihojiwa na OFM, Mama K alidai kuwa haogopi kupigwa picha kwa sababu alishanaswa na kuhojiwa runingani kuhusiana na ishu ya kujiuza hivyo siyo ishu kwake na wala haoni aibu.
Huku akiwa na mwanaye mgongoni, binti huyo alidai kuwa amekuwa akijiuza kutokana na ugumu wa maisha.

OFM: Wewe unatokea maeneo gani na ulianza lini kujiuza?
Mama K: Mimi ni mwenyeji wa Misungwi (wilaya), kwa hapa mjini naishi Mabatini. Sikumbuki nilianza lini lakini yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha.

OFM: Huyo mtoto mgongoni ni wa kwako?
Mama K: Ndiyo ni mwanangu wa kumzaa, ana zaidi ya mwaka. Nilijifungua nikiwa na umri wa miaka 15.

OFM: Baba wa mtoto yuko wapi?
Mama K: Sijui.

OFM: Ukipata mteja unamuweka wapi mtoto au unaenda kulala naye na mwanaume?
Mama K: (huku akiondoka) Nawaachia wenzangu.

Katika kujikusanyia data za kutosha, uchunguzi wa OFM uliogusa viunga mbalimbali jijini hapa ulibaini kuwa biashara hiyo haramu imeshika kasi ya ajabu ikihusisha vitoto vidogo kati ya umri wa miaka 12 hadi 16.

Kuhusu bei, tofauti na Dar ambako bei huwa ni ghali, jijini hapa vibinti hivyo vidogo hujiuza kwa kati ya shilingi elfu saba hadi kumi na tano kwa usiku mzima. Hakuna mambo ya ‘short time’.

Katika kubainisha ukweli wa mambo kuhusiana na vitendo vya ukahaba ndani ya Jiji la Mwanza, OFM ilimtafuta meya wa jiji hilo ambapo simu yake ya mkononi haikupatikana hewani.

Akizungumzia na gazeti hili kuhusiana na ishu hiyo ya watoto wadogo kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alikuwa na haya ya kusema:
“Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia kwako labda unipe muda niongee na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.

via: tuangaze blog

Views: 1905

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 17:31
Haya tunyamaze manake Bonielly na Tulonge wasije kusikia bure deal letu wabaya hizi mtu mbili lol wasije wakaniwekea kitumbua changu mchanga siwaamini kabisa
Comment by Mama Malaika on December 11, 2013 at 17:27
Angela... Hivyo ulivyo watosha. Kitu muhimu ni tabia, uaminifu na kujua pisition yako kwenye marriage.
Comment by Mama Malaika on December 11, 2013 at 17:17
Haa haaaa haaaa... Wahi wahi Angela tena kijana mwenzio yuko single umri miaka 31. Ila nikupe tahadhari, hawa jamaa wakitoka makazini break ya kwanza nyumbani kwa mkewe, ataka wewe na yeye muda wote. Sijui uko tayari??. Ha haa haaaa....
Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 17:15
safi sana mama Malaika unafanya vema, huyo wa miaka 31 ananifaaje walahhi nakimbia faster ngoja niende gym kupunguza hii shape nije huko kembambaaa
Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 16:32
dah kwa mpango huu mama Malaika inabidi nifanye mpango niolewe na mdogo wake baba Malaika ha ha ha lol mwambie shemeji yangu afanye mpango mapema nakuja huko muda si mrefu.
Comment by Mama Malaika on December 11, 2013 at 16:09
Tanzania kunahitaji mabadiriko ya hali ya juu kuanzia sirikali hadi malezi ya watoto wadogo. Na si Tanzania pekee bali Africa kote kwani twapenda sana utwana na ubwana tulioritishwa na waarabu na wahindi.

Umeona eee Omary! Watu wote inapokuja kwenye huduma tuko sawa. Foleni ni ya wote. Hawa jamaa hawana utwana wala ubwana, wana heshimu binadamu wenzao. Mama Malaika na ulalahoi wangu bado maternity wards UK nimelalalia vitanda wanavyotumia wake wa viongozi. Tena doctors ni wanyenyekevu, wanafanya kazi yao kwa maadili ya kazi na utu, wako very friendly. Sijawahi lipia matibabu kwani income tax nayolipa kwa government iko ajili ya ku-provide free medical service (tena best quality) kwa walipa kodi wake.

Nchi za wenzetu zinajali sana watoto kwani wanaamini watoto ndio taifa lake kesho na government iko responsible na hiyo ndio imefanya kila mwezi mtoto apokea pesa toka sirikalini na haijalishi wazazi twafanya kazi au la, kila mtoto raia/mkazi ANA HAKI ya kupokea Child Benefit hadi hapo atapomaliza Secondary School/college. Na pesa ya mtoto ni yake, mzazi sitakiwi kuitumia kwa starehe zangu. Pesa ya mwezi mmoja tu peke yake yatosha mnunulia mtoto viatu, uniform na bado pesa yabaki anunulia toys za kuchezea akipenda au kuweka kwenye bank account yake.
Britain, elimu ya mtoto hulipii (bure) tokea Pre-School (Nursery School) hadi pale amalizapo Sixth Form (waitavyo wao Form Six). Study materials wanapewa shule pia. Wanapofikia University ndio mambo ya ada yanaanza na kununua materials.

Hivyo ingawa kunakuwa na ugumu wa maisha bado kuna unafuu through income distribution, na system hii hata Tanzania ilikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl Nyerere. Kipindi hicho government Secondary Schools za Tanzania zilikuwa free, government Secondary Schools fee Tanzania imeanza 1985. Kulipia huduma ya afya sijui kumuona doctor imeanza nakumbuka kitu kama 1992 or 1993.
Comment by Omary on December 11, 2013 at 1:34

Kiukweli inch za wenzetu wanathamini sana watoto japo wakishafikia miaka 18 wanakuwa na maamuzi yao na huwa hayaingiliwi ila kuanzia mwaka 0 to 17.11 anakuwa chini ya serikali mama akiwa na uwezo mdogo analipwa pesa ya matunzo na serikali mpaka mtoto afikishe miaka 18 ndio huduma inaishia hapo, mtu ukiumwa utatibiwa mpaka upone ndio utatumiwa bill kama una kazi utailipa kdogokidogo kama huna kazi serikali italipa bill hiyo ila huachwi ufe tena utawepea huduma sawa na mtu tajili hosptal hiyohiyo anayotibiwa tajili nawe unatibiwa hapohapo wenzetu ughaibuni wameweza kuweka usawa humjui tajili nani masikini nani? kwani kama ni foleni wote mnapanga foleni hakuna kigogo wala muheshimiwa wote mnapanga foleni 1 nimeipenda hii watu wote mnaheshimiana. Ila hapa kwetu loh! majanga kuna wizara husika ila sijui inashuhulikia nini? maana sioni kazi yake ni bora ifutwe na isiwekewe majeti tena maana haina mana kawa waliowekewe wizara hiyo ndio hao wanaoteseka mitaani na wanaofaidika ni wengine leo mtu akichaguliwa wizara fulani anafanya sherehe kwa kuuchinja maana ulaji umefika atabadilisha maisha yake kwa muda mfupi tu  hahahahah. Hapa bongo kuna rafikiangu mmoja anaitwa Paulo Hecks ana kiwanda chake cha kutengeneza vinyago yeye kaajili walemavu watupu mwanzo kilikuwa raskilomoni akaona ni mbali akakisogeza karibu pale osterbay kiukweli amewasaidia sana na walemavu wengi wanajitegemea wengine wameoa wameolewa na wana watoto hawasimami tena barabarani wanafanya kazi ya mikono yao na mtu anapewa kazi atakayoiweza kutokana na ulemavu wake. Serikali ina tenda nyingi sana inagawa kwa wachina wahindi hali yakuwa wizara husika inaweza kuchukuwa kazi hizo na kuchukuwa vijana waschana wanaojiuza na kuwapa kazi kuna kazi nyingi hazihitaji elimu hata zinapohitaji kuna watu wakiwezeshwa wanaweza.

Comment by Mama Malaika on December 10, 2013 at 14:05
ANGELA.... Natamani viongozi wangekuwa na moyo wa utu kama wewe. Najiuliza kwa hali hii ya sasa na HIV/AIDS sijui miaka 20 ijayo Sub Sahara Africa itakuwaje maana nchi nyingi sasa watoto wadogo wa kike wanajiuza.
Comment by Mama Malaika on December 10, 2013 at 13:57
Zikomo wa CHA (Asante CHA). Nasubiria course ya kiswahili hamu kubwa.
Comment by ANGELA JULIUS on December 10, 2013 at 8:11

dah inauma sana Mungu wangu ningekuwa na uwezo mkubwa nawakusanya wadada wote wa namna hii na kuwapa education but before ni kuwajenga kisaikolojia na pia kuwaweka tayari kwa lolote khs afya zao.

Mama Malaika nimekupata ila kwa system hiyo ya hapo kwenu UK kwa Tanzania bado sana hapa sasa hv kila mtu na chukua chako mapema

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*