Tulonge

CHIDI BEENZ ATAJA SABABU ZA KUTOBOA PUA.

Rapper Mfalme wa Ilala Chidi Benz baada ya kutoboa pua yake, amekubali kuzungumza EXCLUSIVE na millardayo.com nyumbani kwake kuhusu chanzo cha yeye kufanya hivyo na sababu zake.

Chidi amesema “kila kitu ni mtu jinsi unavyoishi, mimi nilitoboa pua mara ya kwanza nilivyosafiri nikaacha pini kwa hiyo ikaziba kidogo kwa hiyo nilivyorudi nikaenda kutoboa tena, hizi ni hisia zangu na vitu vyangu nilivyoviona kwenye macho yangu pamoja na mimi mwenyewe ninavyoishi vitu vilivyonipitia binafsi mimi binafsi kama Rasheed nikajikuta siku tu nimeamka nikaenda town nikajitoboa nikalipa pesa nikarudi nyumbani baadae ndio nikagundua hivi nimetoboa pua”

Chidi amesema “ni alama ambayo nimeiweka kama ni maumivu basi nitayakumbuka yale maumivu na nisiumie tena, kama ni furaha basi nikumbuke ile furaha.. kwa hiyo mimi ndio ninaelewa, nashindwa kuelewa kama kuna watu wanachukulia tofauti kwa sababu unashangaa nini kutoboa pua na nikitoa pini pua inaziba kama kawaida, nini inasababisha uanamke au u**** kwa kutoboa pua, ukiamua unaamua tu kuna watu maaskari bwana na wanajeshi na watu wanasema huyo hivi na yule hivi kwa hiyo kwa kuongea kwako ovyo ntakushtaki kwa sababu itaziba na hutoniambia kitu unajua”

Kuhusu mashabiki wake kumuuliza maswali, Chidi ameiambia millardayo.com amesema “nimekutana na watu wengi sana wameniuliza kuhusu hili swala lakini nikijibu kama ninavyojibu mimi kwa maana yangu wananielewa lakini inategemea mtu ameniulizaje, akiniuliza kiheshima namjibu vizuri ila akija rafu namjibu eeeeh bwana kweli nimetoboa urembo tu najiremba ni kama vile binti kutoboa sikio sasa mimi nimetoboa pua”

Chanzo: http://www.millardayo.com/

Views: 1097

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on April 4, 2012 at 13:11

hii syle ya kutoboa pua, bado masikio, na kuvaa cbe,

Comment by ANGELA JULIUS on April 2, 2012 at 17:08

LOL BWABWA

Comment by ILYA on March 31, 2012 at 16:44

Chidi Benz , unajua nini kaka:@

Hata michael Jackoson alikuwa na pua yake bomba na mzuri tu,lakini alipoanza kuisugua sugua pua ile na kuinyima uhuru wake,akisaka sijui urembo sijui nini..oooo sijui yuko huru kufanya hivyo madamu pua yake na longo longo zingine...,akawa ndio anajiharibu kabisa, mwishowe pua ikaleta balaa!!,ikawa inaoza kimtindo mtindo na kumsumbua sana marehemu huyo, Mungu amuweke mahala pema peponi,amina.

Tukumbuke kauli hii ya wahenga wetu:

"Umaarufu ni harufu".

Comment by Neema Morris on March 31, 2012 at 16:04

hajapendeza hata kitogo

Comment by Christer on March 30, 2012 at 21:20

Ushoga huanza hivyo hivyo km ambavyo hesabu huanza na o,1,2,3,4 etc

Comment by Tulonge on March 30, 2012 at 18:00

Sijaona sababu ya maana aliyoitoa Chidi

Comment by Bonielly on March 30, 2012 at 17:22

nitaisoma kesho,

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*