Tulonge

Washukiwa wa shambulio la Westgate wapandishwa kizimbani

Wanaume wanne wanaoshukiwa kuhusika katika shambulio la Westgate wakiwa kortini Nairobi Novemba 4, 2013. Picha/PAUL WAWERU.

WASHUKIWA wanne wa ugaidi Jumatatu walishtakiwa kwa kuhusika na shambulizi la kigaidi katika jumba la Westgate, Nairobi ambapo watu zaidi ya 67 waliuawa na 180 kujeruhiwa.

 

Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Hussein Hassan Mustafa na Ibrahim Adan Dheq walishtakiwa kwa kuhusika katika shambulizi hilo wakishirikiana na watu wengine ambao hawajakamatwa au waliuawa waliposhambulia jumba hilo Septemba 21 mwaka huu.

 

Wote walikanusha kuhusika katika shambulizi hilo ambapo Wakenya na raia wa kigeni waliuawa.

Washukiwa hao pia walishtakiwa kwa kusaidia magaidi kupanga shambulizi hilo. Wakili wa Serikali Bw James Kirui alisema kabla ya shambulizi hilo, Abdi na Liban waliwasaidia magaidi wawili waliotambuliwa kama Moahmmed Abdinur Said na Hassan Mohhmed Dhohullow kutekeleza kitendo cha ugaidi katika jumba la Westgate Mall.

 

Bw Kirui pia alisema Dheq alimpa makao Abdikadir Hared Mohammed, anayefahamika kwa jina lingine kama Mohammed Hussein katika Madrassa ya Salman Al-Faris, barabara ya Muyuyu mtaani Eastleigh, Nairobi kabla ya Oktoba 7 mwaka huu, akijua kwamba alikuwa ametekeleza kitendo cha kigaidi.

 

Kitambulisho

Dheq alikanusha shtaka la ziada la kupata kitambulisho cha Kenya kwa njia ya udanganyifu.

Bw Kirui alipinga washukiwa kuachiliwa kwa dhamana akisema ni wahalifu wa kimataifa wasiokuwa na makao ya kudumu nchini na wakiachiliwa wataingilia uchunguzi ambao unaendelea.

“Uchunguzi ulianzishwa uliopelekea kukamatwa kwa washukiwa kadha wakiwemo washtakiwa waliohusika kwa njia moja au nyingine na shambulizi hilo,” akasema Bw Kirui.

 

Alisema polisi wako na habari kwamba washukiwa wana mtandao mkubwa nchini unaopanga kutekeleza mashambulizi kwa kulipua ofisi za serikali, maeneo ya umma, majumba ya kibiashara na ofisi za kibalozi.

“Kuwaachilia washukiwa kwa dhamana ni kuwapa idhini ya kuzunguka nchini kutimiza lengo lao la kuua, kuharibu mali na kuzuia utendaji haki,” akasema Bw Kirui.

Hakimu Dolphine Okundi, alikubaliana naye na kuagiza washukiwa wote wazuiliwe  kwa wiki moja.

 

Na swahilihub

Views: 463

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on November 5, 2013 at 9:33
wanashukuwa means you are not sure, tutafika waliohusika wametulia nyie mtabaki kuwashuku hata wasiohusika lol!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*