Tulonge

Hiki ndicho kilichowatokea waumini walio kula nyasi huko Afrika Kusini

Dada akitoka nduki kuelekea chooni pale tumbo lilipoanza kusokota baada ya kula nyasi

Hiki ndicho kilichotokea baada ya mchungaji Lesego Daniel mwenye kanisa lake huko Garankuwa, Kaskazini mwa Pretoria, nchini Afrika Kusini kuwaamuru waumini wake kula nyasi. Alidai kwamba binadamu anaweza kula kitu chochote kwa imani. Baada ya kula nyasi hizo, waumini walianza kusumbuliwa na matumbo na kupelekea kuanza kutapika. Hali hii iliwafanya waumini hao kupishana chooni kwa kasi ya ajabu.

 

Wapo waumini walisema waliponywa magonjwa yao mbalimbali baada ya kula nyasi hizo.

 

Mchungaji huyo alipokea malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii lakini alichojibu ni hiki "God is at work and His people are testifying right now".

Huyu naye akisukutua mdomo baada ya kula nyasi

Jamaa akitapika baada ya kula nyasi

Mchungaji Lesego Daniel

Lesego akiendelea na huduma kwa style ya kukanyaga watu

Views: 790

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dunda on January 15, 2014 at 19:33

Walikuwa wanamuonea gonge mbuzi anavyojiachia kwenye majani kama kapenda vile

Comment by CHA the Optimist on January 14, 2014 at 20:05
Inahitaji akili ya ziada kutambua ukweli na uongo katika hii dunia. na akili hiyo ni Mungu pekee wa kuitoa kupitia sala. Muamini Mungu, Mshukuru Mungu kwa kila jambo, na haya mengine hayatokusumbua.
Comment by Monica Male on January 13, 2014 at 12:34

Mbona hatukuona Mchungaji mwenyewe na yeye akila nyasi?

Comment by Dixon Kaishozi on January 13, 2014 at 10:18

Nimekosa cha kusema .......................

Comment by David Edson Mayanga on January 13, 2014 at 5:30

KWELI KAMA NDIO DINI HIVI MH

Comment by Mama Malaika on January 11, 2014 at 20:22
Ha haaaaa... tumbo likianza kusokota lazima utoke nduki, jamaa kakiinamia choo.

Hmmm.... hao aliowakanya picha ya mwisho

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*