Tulonge

Inasikitisha na kuhuzunisha juu ya picha hii,hivi naomba mniambie kuna haki hapa ya mwanamke huyu asiye na aibu na wala kutambua thamani ya utu wake,mama salma kikwete, anna kilango mpo wapi?

Views: 7193

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on March 24, 2012 at 16:13

ieleweke wazi sehemu hii:

Tunachokisema hapa ni kwamba hawana maadili maadili na ndio maana wanafanya hivyo.Maadili na vitendo hivyo ni vitu viwili vinavyopingana.Kwenye maelezo nashangaa kuna kauli mbili zinazopingana,kauli ya pili inagonga kauli ya kwanza na kuitupilia mbali:hebu tazama kauli hizo:

Kauli ya kwanza:

-Twaweza kufikiri kwamba wamekosa maadili na isiwe hivyo.

Kauli ya pili:

 -Lakini dunia ya leo, maisha yamebadilika sana, kusafiri kwa watu kumewafanya wapate mawazo/akili ya kuweza ku-survive kwa njia yoyote ile! Na watu hawajali hata kama maadili yamekeukwa. Cha maana kwao ni kuweza kuishi.

--------------------------------------------

Kwa mujibu wa kauli ya pili,ni kwamba wanadada hao wanaojivua hadharani wamekiuka maadili lakini wao hawamind kujali maadili au kukiuka maadili,yeye anakwambia wewe unaye jali maadili jali kivyako mimi sijali ninachojali zaidi na cha maana kwangu ni kuweza kuishi.

Yaani hiyo ndio mantiki ya watendao vitendo kama hivyo vya kuvua vua hovyo mbele ya kadamnasi na kuonyesha njia panda.

Hivyo ikiwa mantiki yao ndio hivyo basi kuna tabu gani tukisema kwamba hawana maadili.!???

Na watakuwaje na maadili kaka wakati fikra yao ndio kama hiyo  kuwa:

Hawajali ispokuwa cha maana zaidi kwao ni kuweza kuishi kwa njia yoyote ile!!.

Hatukatai kuwa kuvua kwao hakuwapatii faida,hapana,faida wanapata tena kibao tu na wanakuwa wengine matajiri kupitia biashara hiyo ya kujianika,lakini tutakachokikaa ni fikra hii kuwa wanafanya hivyo na maadili yako pale pale.!!hii fikra piga ua haikubali.Faida wanapata kuishi wanaweza kuishi kwa njia kama hizo lakini  maadili hawana.

Na kama wao (yaani wadada hao kama hao kwenye picha wakionyesha nyeti zao)  wameweza kuvua hadharani na kutangaza nyeti zao hadharani bila tabu yotote,je kuna tabu gani tukisema hawana maadili.?!!

Kama wanataka pia wasifike kwa maadili si waache bali si wavue tabia hizo mbaya na wavae tabia nzuri za maadili!!!!!!!!!

Comment by Bonielly on March 20, 2012 at 16:19

hivi naniii hiv   i hi vi...  mmmmmmmmmmmmmmmmmmmm,

Comment by eddie on March 20, 2012 at 15:06

 Sisi wapita njia mara nyingi tunaweza kuwa na maoni tofauti na ya hawa wanaofanya hizi kazi.

Twaweza kufikiri kwamba wamekosa maadili na isiwe hivyo. 

Tukitazama undani wake wa-africa mambo kama haya si utamaduni wetu.

Ndio maana kuna wabantu wengi watashika marungu kumtwanga atakayeonyesha makalio, "njia panda ", au hata "balcon".

 Lakini dunia ya leo, maisha yamebadilika sana, kusafiri kwa watu kumewafanya wapate mawazo/akili ya kuweza ku-survive kwa njia yoyote ile! Na watu hawajali hata kama maadili yamekeukwa. Cha maana kwao ni kuweza kuishi.

Kuna wengine pia wanapenda kuiga ma-celebrities ambao wana mchezo huo ili wafanane nao bila kujali maadili!

  Kuna kundi lingine wanaitwa exhibionists, hawa wanaweza kuwa ni wenye njaa na walioshiba na hawajali maadili! Wao miili yao bila kuionyesha hadharani ni kama samaki kumtoa majini!

 Katika jamii inabidi tuheshimu kazi au mambo yafanywao na watu!

 Kama tunaona kichefuchefu kuangalia, basi jifungie ndani ili usione.

 Mfano aliotoa Dixon ni tosha kabisa, kwamba kuna watu ambao wanafanya hivyo kwaajili hawana jinsia. Na wana ndugu wanaomtegemea kwa hiyo kazi.

Comment by ILYA on March 20, 2012 at 13:48

Kweli kaka Dixon,unachosema ni kweli,maisha magumu humpelekea mtu kuchagua kuyakabilia namna hiyo si kw akupenda kwake bali ni hali yenyewe.Lakini kuna wengine si maisha kwa sababu ya maisha magumu wanafanya hivyo,bali wako poa sana kimaisha lakini utaona wanafanya mammbo hayo,hebu cheki hapo kwenye pics za chini kuna mmoja katoka home bila chupi tena huyo ni wema wa bongo,anajaribu kuvuta nguo ili ifunike matako yake,sasa huyu ana tabu gani ya kimaisha,hebu cheki na hako kanako onyesha chupi,sijui kana matatizo yepi tukasaidie,hebu cheki na yule wa chini kule kavaa suruali sijui ni suruali iko kama vile vyavu nyekundu,huyu tena kakaa pozi kabisa anasubiria mpiga picha amtungue picha,kavaa nyavu suruali kasahau kutanguliza chupi ndani The 2 matakoz  yako nje moja kwa moja.Hi ni haki kweli.!??

Na dnio maana mi nikasema kwamba:

Kuna wanao  fanya hivvyo kutokana na ukosefu wa maadili,maadili haba.wengine wanafanya kutokana na maisha kuwa magumu hawana tena jinsi ispokuwa wafanye hivyo.

Na wengine wana maisha magumu lakini hawako tayari kufanya madude hayo yanayovunja heshima yaoo,wanavumilia na kutafuta njia salama za kupambana na hali ngumu ya kimaisha ambapo wanafanikiwa na wanabaki salama kiafya,hawako tayari kabisa kufuata  njia hii ambayo ni hatari sana kwa maisha yao,maana hiyo ni tiketi ya magonjwa hatari.

Comment by Dixon Kaishozi on March 20, 2012 at 10:41

Kwa njia moja au nyingine wafanyao kazi hii  wanafanya si kwa kupenda.. ingawa wengine pia wanapenda kufanya hii kazi kutoka moyoni kabisa.

kulikuwa na show ya khanga moko hapa arusga kwa mara ya kwanza.. sikusita kwenda kwani nilikuwa naisikia tu... sikuamini nilicho kiona .... LAKINI... kulikuwa na "walinzi" waliokuwa wanazuia watu kupiga picha au video.. unajua tena mambo ya teknologia "SIMU" . Na nilimsikia dada mmoja kwa masikio yangu akisema.. jamani msitupige picha, hata sisi tuna watoto na familia..

kwa haraka haraka nikahisi huyo dada anafanya hiyo kazi si kwa kupenda bali ni maisha ndiyo yamefanya ajikite kwa ajira hiyo..

Comment by ILYA on March 16, 2012 at 16:07

Na huyu nae vipi,kakumbwa na nini!! ,au nae ni entertainer!!

MAADILI HABA!


Ni ndani ya bongo hiyo!

Comment by ILYA on March 16, 2012 at 15:10

NGOJA NITOE MFANO HAI:

Mwizi akiiba anapata faida na kukithi mahitaji yake ya kimaisha,lakini kitendo hicho kinabakia kuwa kitendo kiovu na kinachoashiria ukosefu wa maadili na malezi.Hivyo kurekebisha maisha yake kupitia njia hiyo ya wizi aliyoichagua kunafanikisha malengo yake lakini pia hakuondoi uhalisi wa tendo hilo,nao ni uhalisi huu kwamba wizi ni uovu,masaa yote sawa sawa ulete faida au usilete faida.

Na kusahau chupi kama huko home kama ilivyokwenye pic ni ukosefu wa nidhamu,maadili na malezi ingawa mwenyewe alitendo kitendo hicho anapata maslahi kwa kazi hiyo.Hivyo maslahi atapa lakini ni ukosefu wa maadili na malezi bora.

Na hili halina tofauti kusema ukweli,yaani nchi zote duniani hata huko ulaya,hakuna anaweza kusema kuvua nguo mbele za watu au picha kama hizi hapa sehemu hii vyote vinatokana na kuwa na maadili bora!!! hapa hakuna mtu mwenye fgikra hiyo,wanadamu wote ukiwauliza watakwambia hakika mammbo hayo ni ukosefu wa nidhamu,maadili na malezi bora.

Hata msichana mwenye kutembea uchi au nusu uchi au robo uchi,ukimuuliza kunako kitendo chake???? hawezi kukwambia nafanya hivi kwa saababu ndio maadili bora na ndio malezi bora!!!!,atakachoweza kukifanya ukimuuliza swali hili ni kunyamaza tu !!! maana hawezi kujiponda kuwa hana maadili na malezi bora.

Comment by ILYA on March 16, 2012 at 15:07

Sikatai@ kuwa mamamboz kama hayo ya wadada hawa ikiwemo hii ya kusahau chupi kuwa ni mbinu ya ma-entertainer kujitafutia kipato maana wanalipwa kadiri wanavyoburidha na kadiri wanavyoingiza watu  kwenye kumbi za show.

Ninachotaka kukisema mimi ni hiki kuwa:The way they appeare kwenye hayo mashow-rooms kiasili bali kiakili inadhihirisha ukosefu wa maadili.

Sikatai faida wanayoipata,bali nasema vitendo hivyo vinatokana na ukosefu wa maadili.Na hata hapa Iran wapo wanaofanya vitendo vya kihasara kama hivi,si tu wairan walioko nje ya Iran bali hata hapa wapo na sana tu,na yote hayo ni ukosefu wa maadili.

Kupata faida baada ya kutenda vitendo hivi vya kuvua vua mbele ya kadamnasi ni suala,na kukosa maadili kutokana na matendo hayo ni suala jingine.

Kukosa kwao maadili haiwazui wasipate faida kwa hayo matendo yao ya ukosefu wa nidhamu na malezi bora.

Comment by MARTHA MSHANGA on March 16, 2012 at 10:32
Mmhhh!!!
Comment by eddie on March 16, 2012 at 2:40

Wanasema nyani wengi waking'ang'ania tawi moja wote wataanguka. Kuna rangi za aina nyingi duniani, nyeupe nyeusi nyekundu, nk.....tabia za watu zinatofautiana kama zilivyotofauti za rangi tuzijuazo. Maadili ya watu hutofautiana...tukubali tusikubali!!

Uwezo wa binadamu vilevile unatofautiana, ni kama vidole tulivyonavyo mikononi, vyote vina urefu tofauti.

 Hawa ma-entertainer wanalipwa kwa lolote wanalofanya ili kujaza watu kwenye ma-show rooms, hata hiyo ya kusahau chupi huenda ndio mbinu mojawapo.

Ni kama mvua samaki ukiweka mahindi hagusi samaki hiyo ndoano, sasa wewe weka chambo utaona!!!

Ukiishi nchi za IRON CURTAIN huwezi kuona haya kila siku. Nimewaona jamaa wa Iran beach za huku

wakiona mwanamke topless utafikiri kaona mazingaombwe!!!

Tusiwe wanafiki, lets face reality!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*