Kwa wale wasiyo fahamu, Wema(Miss Tz 2006) alikuwa mpenzi wa Diamond lkn walikorofishana.
Baada ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo zoezi lake halikufanikiwa.
...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
...Bembeleza, bembeleza na wewe jamaa ndiyo aliendelea kuwajibika
...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Add a Comment
ila inauma sana cjui lakini mapenzi ni kitu kingine, na kama kweli Wema alikuwa akimpenda Diamond lazima itakuwa imepain sana kiubinadamu, wakati mwingine mapenzi yanakuwepo lakini kinachoponza ni tamaa tu, hivyo wema itamgharimu sana!
dah aibuuu
Jamani wote hawa ni sawa na pipa na mfuniko
Hapo sawa
Kaka Alfan@ si kwamba nampiga tafu wema ispokuwa najaribu kuweka sawa maana Diamond amekuwa hatulii na istoshe ni muongo wa mapenzi sana,halafu ni limbukeni sana wa mapenzi maana alijaribu kulifisha suala la yeye na wema hadi kule Uingereza alipokuwa stejini katika moja ya mitaa ya jiji la London,mara akiwa steji washabiki wake wakashtukizwa kwa swali kutoka kwa diamod akiwauliza ati nichagulieni mpenzi wa maisha yangu kati ya wema na jokate!???
Alizomewa kule London na kuonekana mharibu wa watoto wa kike mwenye kutumia umaarufu wake kuwaharibu warembo kama wema na wengine.Binafsi sioni kama anafanya vema kwa upande wa mapenzi ispokuwa mharibifu tu.!!
Mi mgeni hapa
Chalii acha kumtetea huyo Wema hafai hata kwa kulumangia....Binafsi nimefurahi sana walipoachana na Diamond maana alikuwa anamchafua kijana wa watu!!
chalii mimi nilikuwa kila siku namuomba Diamond aachane na huyo kunguru asiye fugika, anajipendekeza baada ya kumwangw na pedeshee la ikulu, diamond are forever, kamua diamond achana na huyo kuku aliyekosa manyoya hata halioni haya, alikuwa anajitapa eti biula yeye diamond hawezi kuwika kiko wapi sasa?
Nakumbuka:Oktoba 2, 2011, Diamond kwa utashi wake, bila kulazimishwa, alijishaua mwenyewe kumvisha pete ya uchumba Wema huyu mwenye taji la Miss Tanzania 2006-07,au tuseme alimvisha pete kanyaboya isiyo na mapenzi ya moyoni!!. Ikiwa ni hivyo basi Diamond kwa hakika atakuwa ni:
Mtu mmoja "mpenda sifa","mchafuzi wa watoto wa kike", "asiyekuwa na mapenzi ya kweli", "gusa unate", "mkuki popote","limbukeni wa mapenz"i, "anayetumia umaarufu wake vibaya kuwachezea warembo". Na ni kwa msisitizo zaidi Diamond atakuwa ni: "Skirt-chaser and cheater".
Duh! Binafsi machozi membamba yamenitoka maana sio vizuri kabisa alivyofanya Diamond,narudia tena mimi kama chalii:
Sio vizuri kitendo hicho, na hiyo sio tabia nzuri kwa mtu na hionyeshi kuwa wewe ni mwenye utu na ustaarabu, bali itaonyesha wewe si mwenye kusamehe na uko tayari kumdhalilisha yeyote uliyetofautiana nae kifikra au kugombana nae.
Unapokuwa wewe ni msanii, kama diamond na uko juu ya steji,unaweza kutuzwa na mtu yeyote baada ya wewe kumfurahisha kwa wimbo wako,unajua nae au hujuani nae,na wema hakumpa hizo hela kwa kumhonga bali kampa kama wengine wanavyoweza kumpa katika washabiki wake.
Ndio kuna ugomvi kati yao lakini sio freshi kuuonyesha kwa watu,ukizingatia nyinyi pale mwanzo mlikuwa chanda na pete,kubali atakachokupa mbele ya watu walau kwa kuheshimu uhusiano wenu wa nyuma,huo ndio utu na ustaarabu.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge