Tulonge

Jinsi m/mke anavyotakiwa kujiweka au kujiseti ili alete hisia na kuonekana mwenye mvuto mbele ya m/ume.

Hi:

Ndugu zangu wa Tulonge, sina shaka kuwa hamjambo na mtakuwa mnajianda ipasavyo kwa ajili ya kuikaribisha kwa furaha sikukuu ya Christmas.

 Kwa leo ningependa kuzungumzia suala zima la "mvuto wa mwanamke/binti kwa mwanaume".

Na hili ni katika masuala nyeti kabisa katika ulimwengu wa "upendo" nikimaanisha "ulimwengu wa Love".

Ni muhimu nigusie nukta hii kuwa sifundishi hapa bali nimekuja kimtazamo zaidi.Na nitakunika zaidi

moyo wangu kuyasoma mawazo yenu na michango yenu marafiki kuhusu suala hili la kijamii.

Na ninaweza kuanza namna hii kama ifuatavyo:

 

Sitashangaza nikisema  wanawake/wasichana wamepewa uzuri na Mola wao,uzuri wao hauna shaka,lakini

wamepewa uzuri na Mola wao ama suala la kujenga mvuto hilo wameachiwa wenyewe,na ndio maana utaona

mwanamke pembe 'A' ni  mzuri sana lakini havutii,mvuto hana,lakini ukigeuka pembe 'B' utamuona

mwingine mzuri sana kama wa mwanzo na zaidi ya uzuri anavutia zaidi kwa kutazamwa.

 

Kwa hiyo suala hili lipo kwamba pamoja na uzuri wa baadhi ya wanawake lakini utawakuta bado si

wabunifu bali wanashindwa kuwa wabunifu wa kujenga mvuto.

Ni wazi kwamba uzuri wa mwanamke hautoshi kuwa kivutio tosha kwa mwanaume bali naweza kusema uzuri hauvutii, kinachomvutia mwanaume ni  mvuto wa mwanamke ,hivyo kuna haja kwa mwanamke ya kufanya ubunifu ni jinsi gani ya kujenga mvuto mbele ya mpenzi wake wa kiume hasa "pindi anapokutana nae  kwa mara ya kwanza".

Hivyo hapa nitazungumzia mvuto wa mwanamke pindi tu anapokutana na mwanaume kwa mara ya kwanza.Na ninaposema kwa mara ya kwanza simaanishi ndio mara ya kwanza kukutana bali ukikutana nae leo kesho pia kabla ya kukutana nae, jaribu kujiandaa kukutana nae katika zile dakika za kwanza ukiwa katika hali ya mvuto zaidi ikiwezekana kuliko hata mkutano wenu wa jana.

 

Na ikiwa utashindwa kujenga mvuto basi jua kwamba hatua hiyo itasababisha hisia za mwanaume kuwa

mbali sana na kutomuelekea  msichana/mwanamke huyo asiyejua au afanyae uzembe wa kujiseti kimvuto.

Ikiwa mnapendana wewe na mpenzi wako katika hali hiyo ya kuzembea kujiseti kimvuto basi upendo wenu

unaweza kuwa ngano nikimaanisha  'hadithi'.

 

Lakini ukiwa mbunifu ukazitumia dakika chache na muhimu kujiseti kimvuto ili umvutie mwanaume/mpenzi

wako,basi siku zote utam-drive crazy mchumba wako.

 

Utaweza kufanikiwa katika hilo ikiwa utajari muonekano wako,ikiwa utajari mwili wako na lugha yako

pasina kusahau upangiliaji wa mavazi yako au kwa ufupi niseme uvaaji wako.

 

Wakati muhimu na wa kwanza kabisa wa kuapply utaratibu huo ni pale unapokutana na umpendae sehemu

iliyopangwa.Hakikisha unapotokezea mbele ya mpenzio uonekane kama vile nuru imechomoza.

Utafiti wa hivi karibuni umegundua kuwa karibia robo tatu ya wanaume kitu cha kwanza kabisa kabla ya

yote ambacho hukitizama na kinachowavutia sana pindi wanapokutana na mwanamke ni nywele za

mwanamke,na ni wanaume wachache sana waliosema kinachovutia ni nguo za mwanamke pindi tu

anapotokezea mbele ya mwanaume.Hii ni kwa mujibu wa utafiti huo wa hivi karibuni.

 

Hivyo suala la nywele ni muhimu sana mwanamke kulipa kipao mbele.Na ikiwezekana  chukua muda

mwingi kujali nywele zako then mavazi.

 

Hebu tazama mambo haya matano ambayo ni muhimu kuyazingatia pindi unapokutana kwa mara ya kwanza na mwanaume, mambo ambayo husaidia kuleta hisia kwa mwanaume, na mvuto wako kuonekana mbele ya mwanaume.


1.Nywele zako:

Nywele huchukua nafasi kubwa sana kutokana na umuhimu wake na hii ni kwa sababu nywele ni rahisi sana kupata doa na ndio alama ya haraka sana kutambulisha mvuto wa mwanamke.

Wanaume huvutiwa sana na nywele zilizo soft,smart,rangi yake na jinsi zilivyosetiwa.Hupoteza sekunde

zao za mwanzo kutizama muonekano wa nywele kabala ya kutizama maeneo yako mengine muhimu.

Hivyo nywele huleta mvuto,sawa sawa ziwe ndefu au fupi,muhimu uziweke katika mtindo wa kuvutia.

 

2.Macho yako:

Kama nywele zako ni fremu ya sura yako,basi macho yako yatakuwa ni madirisha yake.Wanaume baada ya

kuvutiwa sana na nywele zako nzuri hufuatia macho yako,macho yako yanaweza kujenga mawasiliano yenye

speed ya ajabu  kuliko hata speed ya sauti  kati yako na yeye.

 

Macho yana nguvu kubwa sana,ni mawasiliano ya moja kwa moja,na kuwasiliana kwa macho kunaweza

kujenga uhusiano wa papo kwa papo ikiwa uhusiano huo hakukuwepo hapo kabla  kati yenu, na kunaweza kukuza , kuboresha na hata kunenepesha zaidi uhusiano wenu  ikiwa  ulikuwepo tangu hapo mwanzo.

 

Hivyo ni muhimu kwa wanawake kujali macho yao wanapotoka,nikimaanisha inapendeza sana wakiyalemba  na kuyapamba, nadhani wao wanajua zaidi ni makorokoro yepi yanatakiwa ili kuyaweka macho katika muonekano wa kimvuto.

 

3.Kiatu chako:

Nywele na macho umuhimu wake katika mvuto wa mwanamke ni mkubwa sana,hii ni kulingana na matokeo ya uchunguzi uliofanyika ambapo baada ya robo tatu ya wanaume kuulizwa swali kuhusu hilo,walijibu kama nilivyo nena.Lakini hawakutaja viwili hivi tu bali pia walisema:

Viatu vya mwanamke pia vina mchango mkubwa katika kukamilisha suala zima la mvuto wa mwanamke.Hasa hasa vile viatu vyenye visigino virefu.

Viatu vyenye visigino virefu vitayateka macho ya mwanaume kwa sababu viatu hivyo vinakuweka kimvuto

zaidi na kuboresha mkao wako na shape ya miguu yako,lakini ikiwa utaweza kutembea navyo vizuri.

Kama kutembea navyo ni mgogoro kwako basi hutakiwi kuvivaa maana vitaharibu mvuto wako hasa utakapoharibu  utaratibu wa kutembea.

 

4.Tabasamu lako mbele yake:

Kuonyesha ishara ya kuchekelea,au kutabasamu mbele ya mwanaume unapomeet nae kutamfanya mwanaume huyo aone kikweli kweli uso wako.

Mwanaume hawezi kutosheka na uzuri wa mambo hayo matatu yaliyotajwa,hawezi kutosheka pia na uzuri wa midomo yako (lips) pasina kuilemba na kuonyesha ishara ya kutabasamu na kuchangamka.Usikutane na umpendae/mwanaume  kama vile uko kwenye msiba au kama vile konda aliyekosa abiria!.

Hivyo ni muhimu sana unapokutana nae umuonyeshe walau kwa mbali smile yako,hilo sio jambo dogo kwa mwanaume bali ni kubwa sana na hulithamini sana kiasi kwamba ni vigumu kuelezea kikamilifu uthamani wa smile yako kwake!.

smile  yako  humuandalia mwanaume huyo mazingira mazuri ya kutambua mvuto wako na kuzama katika ulimwengu wa  hisia kuhusu wewe.

Akisha kutana na jicho lako,kisha tabasamu lako atashindwa kujizuia kujibu mawasiliano hayo bali nae

utamuona anasmile,na hiyo ni hisia nzuri unaweza kuijenga kwa upande wake mara tu unapokutana nae.

 

5.Mwili wako:

Asikudanganye mtu hakuna kitu ambacho huwavutia sana wanaume kupita maelezo kama muonekana wa mwili wa mwanamke.

Na hii haimaanishi kwamba wanaume wanajaji au kukuhukumu wewe na mwili wako na sura yako pindi

unapotembea may be kwa room ,hapana,bali ni kwamba huwafanya wasiweze kujimiliki na hatimae

kuangalia na mwisho kutizama kwa jicho la chuma mwili huo unaovutia na uliolembwa kwa mavazi mazuri.

Mwanaume huyo ataweza  kutupia jicho katika mwili wako ndani ya sekunde kadhaa na huenda sekunde hizo zikaenda mpaka dakika hasa wewe binafsi utakapoonekana kuwa comfortable zaidi na mwili wako.

 

So, jaribu wewe kama binti/mwanamke kuvaa mavazi ya heshima ,mavazi smart,mavazi yanayokwenda sawa na body yako ilivyo,yenye rangi nzuri na yatakayoonyesha ubora wako ,uzuri wako na mvuto wako.

Usipendelee kuvaa mavazi yaliyochorwa makatuni,au makoro koro ya ajabu,mikatuni hiyo inaweza kumpeleka mbali mwanaume anayekutazama badala ya kushughulishw ana mvuto wako anauchukua muda mwingi kutathmini makatuni anayoyaona kwenye nguo yako,so nguo zenye makatuni zivae nyumbani kwako tu usitoke nazo mbele ya mtu wako muhimu/mwanaume.

Usikate tamaa juu ya ukubwa au udogo wa viungo  vyako vya mwili,cha msingi jaribu kupangilia mavazi

yanayooana na umbo lako.

 

Mambo haya matano yasiwe mwisho wa fikra zako na mawazo yako,bali onyesha ubunifu wako wa kujiweka

kimvuto zaidi mbele ya umpendae -nikimean mwanaume- katika fursa zote uzipatazo hasa  katika fursa

zile za muhimu.Fursa hizi za muhimu na nyeti kitaalamu hujulikana kama 'Golden Chance',hivyo usikubali zipite hivi hivi pasina kumuonyesha umpendae/mwanaume maajabu ya Kilove.

 

Namna hiyo ikiwa hayo ndio yatakuwa mazoea, basi uhusiano wa upendo utakaojengeka au uliojengeka

baina ya mwanamke na mwanaume hauwezi kutetereka hata siku moja,na mwanaume ataua kabisa mawazo ya kuanzisha uhusiano mwingine sehemu nyingine.

Namna hiyo  mtazamo wangu utakuwa umetimia.

 

Na Chalii_a.k.a_ILYA

 

 

Views: 16628

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Lucie on January 6, 2012 at 11:13

hatarudi mi shahidi@bonie

Comment by Bonielly on January 3, 2012 at 11:38

@lucie angela atataka kwenda kwa kina dick, atarudi kweli? kuna senene kule

Comment by Lucie on January 2, 2012 at 17:15
Ajajajaja bonge la somo, ilya uko juu

@angela mbona unamuonea boni hahahahhaha
Comment by ANGELA JULIUS on January 2, 2012 at 16:49

WEWE BONIEELY UNANIONEA HURUMA MIMI SHANGAZI YAKO? NGOJA NIENDE ZANGU NIKIRUDI NAKUWEKEA NA WEWE KWENYE HOTPOT AU SIYO MTANI WANGU

Comment by Bonielly on January 2, 2012 at 12:33

we nenda huko bk kama utarudi dar, ukila ndizi za huko si zani kama ukumbuka kurudi nakuonea huruma angela,

Comment by ILYA on December 30, 2011 at 18:35

Yote tisa kumi ni ile ya mkwe wangu,alidhani ati Katerero ni silaha,nimechaka mpaka utumbo watingishika!!!!

Comment by Dixon Kaishozi on December 29, 2011 at 8:43

HAHAHAHAHAAAAA... Kama kawaida yenu.. mnanipa burudani si kitoto..HAHAHAA @ Bonielly & Angela

Comment by ANGELA JULIUS on December 28, 2011 at 17:59

HE HE HE HEEEE HALOOOOO NACHEKA UTAFIKILI MAZURI MIMI KATERERO NAENDA NA GRATIOUS MANAKE YEYE NAIMANI NDO ANAPAJUA VEMA KULIKO WEWE NA ISITOSHE AMENIKARIBISHA NA AMENIAMBIA MENU ZA KULE TAMU SANA. WEWE UKIENDA KULE LAZIMA WAKUTOE ULIMI CHEZEA WAHAYA WEWE SHAURI YAKO.

Comment by Bonielly on December 28, 2011 at 15:58

angela omba likizo nikupeleke katerero uamini kama nimemaanisha, unavyofikiri wewe, ukitaka kuamini, huo mwezi mchanga mimi siujui mimi najua kwamba wewe hupajui katerero mimi nitakupeleka huko ninapo maanisha mimi, hicho kichina cha msisitizo utaandika kisomari,

Comment by Mama Malaika on December 27, 2011 at 1:26

Asante sana Dixon kumbe kuna kibao kabisa cha Katerero... yaelekea ni kiji almaarafu sana hicho atiii.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*