Tulonge

Kanisa jingine lachomwa moto Tanzania

Saa chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasihi viongozi na waumini wa dini za Kikiristo na Kiislamu nchini kuwa wavulilivu na kujiepusha na vitendo vya kulipiza visasi, Kanisa la la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji limechomwa moto na kutetekezwa kabisa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Buronge mjini Kigoma.

Kashai alisema kanisa hilo lilichomwa na watu wasiojulikana na kwamba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1,337,000 ziliteketea.

Alisema sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa huku upelelezi wa tukio hili ukiendelea ili kuwabaini wahalifu hao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Simon, alisema: “Nilipata taarifa kuwa kanisa langu limeteketea kwa moto, nilikwenda Polisi Central kutoa taarifa ndipo tulikwenda eneo la tukio tukakuta kanisa lote limeteketea kwa moto.”

Alisema katika kanisa kulikuwa na mabechi 14, mlango mmoja, virago vitatu, masanduku ya sadaka na ubao wa kufundishia, vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,337,000.

Mchungaji Simon alisema hajui watu waliochoma kanisa hilo na kuiomba serikali iangalie matukio ya uchomaji wa makanisa yanayoendelea nchi nzima.

Pia, alilitaka Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili kukomesha vitendo vya uchomaji wa makanisa.

Alisema kanisa ni taasisi ya jamii, hivyo anaomba serikali ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaoabudu katika kanisa hilo wapate sehemu ya kuabudia.


Ni sehemu ya taarifa kwenye gazeti la NIPASHE

Views: 342

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on October 17, 2012 at 18:06

Boko Haramu hawako Nigeria peke yake, wametapakaa kote...

Comment by Christer on October 17, 2012 at 10:44

Hizi ndizo ishara za mwisho wa dunia, tatizo binadamu tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii.

Comment by Regina Lipyana Haule on October 17, 2012 at 8:47

Jamani mbona watu wanahamu na vita kwa nini ni vitu gani vimewajaa kwenye ufahamu wao kwa nini wapo vipofu wa mawazo sawa wamechoma moto sasa hii ghalama tena ya kujenga tena si bora ile hela hata wangefanyia kitu kingine cha kuleta maendeleo katika sehemu hiyo labda kulikuwa kuna hitajika huduma ya hosp au barabara Ee Mwenyezi Mungu wa rehemu watoto wako kwa maana awajui watendalo bali ni upofu wa ufahamu umewajaa

Comment by Mercy Kimario on October 17, 2012 at 8:41

Ee Mungu tusaidie, watanzania tunafikia hatua hii wakati tuna uhuru wa kuabudu?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*