Tulonge

Kigamboni: Halmashauri, Wizara wabomoa nyumba 37 usiku; 100 hawana makazi

Watu zaidi ya 100 wanaoishi eneo la Minondo, Kigamboni hawana makazi baada nyumba zao 37 kubomolewa katika zoezi lililoendeshwa usiku wa manane na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi ya Maendeleo ya Makazi.
Zoezi hilo limefanywa ili kupisha ujenzi wa nyumba za viongozi wanaodaiwa ni wa serikali wakiwamo watumishi wa Jeshi la Ulinzi na Usalama.
Kwa mujibu wa wananchi walioathirika na zoezi hilo, tukio la ubomoaji lilifanyika saa 9:00 usiku hadi saa 12:00 alfajiri chini ya ulinzi wa vikosi vya polisi wa kutuliza ghasia na askari mgambo wa jiji.
Wakiongea mbele ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, ambaye alikwenda eneo hilo kuwapa pole kutokana na tukio hilo, walisema zoezi hilo halikwenda kihalali, kwani zilitumika nguvu na ubabe kwa kuwaondoa watu ndani ya nyumba zao.

Kwa niaba ya wananchi hao, Stamili Mwinyimvua, alisema kwa muda wa siku tano sasa, wakazi hao wakiwamo wazee na watoto wanalala nje na kunyeshewa na mvua.

Alisema mgogoro wa eneo hilo, umeanza tangu mwaka 2007 baada ya serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kulitenga eneo hilo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa nyumba hizo bila kukubaliana na wananchi hao.

Mwinyimvu, alisema walishangaa kuona viongozi wa wizara hiyo wakifika hapo na kuwataka wananchi hao kupokea fidia ya Sh. 700,000 kwa heka moja, kitu ambacho hawakukubaliana nacho.

Kutokana na mvutano huo, waliamua kwenda Mahakama ya Ardhi kupinga hatua hiyo, lakini wakati wanasubiri kesi hiyo isikilizwe, ghafla siku hiyo wakashtukia magari ya polisi na tingatinga yakifika hapo alfajiri na kuanza kubomoa nyumba.

"Tumepotelewa na vitu vingi, mnavyotuona hatuna nguo, chakula wala vitu vya kulalia, baada ya polisi kuvitupa porini na kututishia kutupiga risasi endapo tutarudi katika maeneo yetu," alisema mkazi mwingine Kasimu Kabergete.

Dk. Ndugulile amelaani kitendo hicho na kukielezea hakikujali utu wa binadamu.
Alisema kiwango cha fidia ya Sh. 700,000 wanachotakiwa kulipwa wananchi hao ni kidogo sana, ikiwa hivi karibuni wenzao wa Gezaulole wamepewa Sh. Milioni tatu kwa heka moja.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Englibert Kiondo, alikiri polisi wake kusimamia ubomoaji huo, ambapo alisema wao walikuwa wasimamiaji tu na ikitakiwa maelezo zaidi waulizwe Halmashauri ya Temeke au Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Imeandikwa na MOSHI LUSONZO
28th April 2013
Chanzo cha habari: NIPASHE JUMAPILI

Views: 242

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on May 1, 2013 at 21:14

Iko siku yao, huo ubabe wa sirikali na viongozi wake utafikia kikomo

Comment by KUNAMBI Jr on April 30, 2013 at 8:58

uonevu huo dadadeki

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*