Tulonge

Kijana aingia uwanjani na kumvamia Golikipa wa timu ya Alkmaar,apokea maumivu na manundu kutoka kwa kipa huyo.

Baada ya Ajax kuongoza iliyokuwa ikimenyana na kutoana jasho na timu ya Az Alkamaar kwa bao 1-0 mnamo dakika ya 35 ya mchezo katika raundi ya 16 ya ya kombe la wadatch wanaojulikana kama waholanzi,Mtu mmoja kutoka siti za washabiki wa soka alijipendekeza na kumvamia golikipa wa timu ya Alkmaar aliyejukana kwa jina la Esteban Alvarado.


Mtu huyo alidhani kipa huyo ni kipa mzembe mzembe au kipa mdebwedo,lakini kumbe hakuwa kama alivyo mdhania.

Kipa huyo alichukizwa sana na uvamizi huo dhidi yake akaamua kuweka ukipa pembeni na kumuonyesha mvamizi huyo kuwa hata masuala ya ndondi na masumbwi ya kityson anayamiliki kisawa sawa, na hii ilikuwa ni baada ya kuamua  kumtolea uvivu mvamizi huyo kwa kumtandika mateke mazito yenye kilo zote,na  baada ya shughuli hiyo refa wa mechi hiyo aliamua kumzawadia  kipa huyo kadi nyekundu kutokana na kuifanya kazi hiyo katika eneo lisilohusika.

Baada ya kipa wa Alkmaar kupewa kadi nyekundu wachezaji wa timu hiyo walionyesha hali ya kugoma kuendelea na mchezo.

Kipa huyo bwana Esteban kitendo chake alichokitenda  kilikuwa ni kulipiza kisasi dhidi ya mashabiki ambao mmoja wao aliamua kuingia ndani ya uwanja na kumvamia kipa huyo na kumpiga ambapo alimua nae kujihami kwa kumkabidhi manundu mvamizi huyo.


Baada ya kipa kutimuliwa uwanjani kwa kupewa kadi nyekundu,Kocha wa timu hiyo ya Alkmaar bwana Gert Jan Verbeek aliamuru timu yake kutoka nje ya uwanja na mechi ikawa imestopishwa na kumalizwa kimya kimya huku Ajax akiwa mshindi wa bao 1 kwa tairi.


Kijana mwenye umri wa miaka 19 aliyemvamia kipa huyo uwanjani alitiwa mbaroni na Meneja wa Ajax Bwana Frank de Boer alisema uamuzi wa timu ya Alkmaar unaeleweka na niwa kimantiki.Kisha akasema:

"Nina uhakika mtoto huyu aliyemvamia kipa wa Alkmaar na kupokea manundu kutoka kwa kipa huyo hatorudia tena katika maisha yake kuingia uwanjani na kumvamia kipa yeyote". Tazama link hii: http://en-maktoob.news

Na:  Chalii_a.k.a_ILYA.

 

Views: 467

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on December 23, 2011 at 23:14

Bonielly umepinda wewe, akili zako zinakutosha mwenyewe

Comment by manka on December 23, 2011 at 20:56

HAHAHA, KIJANA ALIDHANI HUYO KIPA NI MDEBWEDO EEE.

Comment by Alfan Mlali on December 23, 2011 at 18:44

hahahahahhaaha! Hata ningekuwa mimi nisingekubali tena ningehakikisha namvunja mkono au mguu kabisa..Sipendi makipa wengine wanavamiwa wanapigwa wanabaki kulala chini..kuwa ngangari mchakaze then unaenda zako nje kwa kadi nyekundu saaaaafi!!!

Comment by Bonielly on December 23, 2011 at 14:19
hata mimi nilipanga siku moja timu yetu ya twiga stars ikicheza nikambusu ester chalamila, kumbe mambo yenyewe ndio haya simo,
Comment by Mama Malaika on December 23, 2011 at 0:04

Mkwe angalia usije kosa mke.. Ha haa haa...... Hapa nipo na furaha kwani Mashetani wekundu wameonyesha ubabe wao na kumpa mtu kichapo

Comment by ILYA on December 22, 2011 at 23:51

kijanakapokea makonde,nilikuwa napanga siku moja nikitia maguu kwenye mechi ya Arsenal na Mashetani wekundu wa Manchester United niingie uwanjani na kumpiga konzi "NANI", lakini kumbe naweza kupata reply ya manundu,itabidi nibadili nia nisije kupata manundu bure kama kijana huyo alivyopokea maumivu bila kutegemea.

Comment by Tulonge on December 22, 2011 at 23:25

Hahahaaa machizi kama hawa hawakosekani uwanjani

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*