Tulonge

Kondomu bandia aina ya Durex na Trojan zauzwa nchini

KONDOMU zinazodaiwa kuwa ni bandia ambazo zilipigwa marufuku nchini Uingereza kutokana na kubainika kuwa hazina ubora unaotakiwa, zimetapakaa katika maduka mbalimbali ya dawa nchini, Mwananchi limebaini.

Kondomu hizo ni Durex na Trojan ambazo zina vipele na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa zinauzwa katika maduka mbalimbali ya dawa kwa bei ya Sh5,000.

Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilifanya msako mkali kwa lengo la kukamata mamilioni ya kondomu hizo, wakati ambao ilikuwa imepita takriban miezi 18 tangu zilipokuwa zimeingizwa nchini humo.

Mdhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya wa Uingereza alinukuliwa akisema kuwa mamilioni ya kondomu hizo feki ziliingizwa kutokea Mashariki ya Mbali na kwamba tayari zilikuwa zimetumiwa na idadi kubwa ya watu.

Kondomu hizo zinadaiwa kutokuwa na ubora hali inayoweza kuongeza hatari kwa watumiaji kwa kusambaza kwa kasi magonjwa ya zinaa, virusi vya Ukimwi au kusababisha mimba zisizohitajika, hivyo kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha kuwapo kwa taarifa za kondomu hizo za Durex na Trojan na kuongeza kuwa mamlaka hiyo imewaagiza wakaguzi wake kuzichunguza ili kubaini kama zina ubora ama la.

“Wakaguzi walichukua sampuli ya kondomu hizo kwa lengo la kuzichunguza, nipe muda kidogo ili nizungumze na mkurugenzi ili kujua uchunguzi ule umefikia wapi,” alisema Simwanza.

Alipotafutwa baadaye alibainisha kwamba uchunguzi wa sampuli hiyo bado upo maabara na kwamba majibu yake hayajatoka. Hata hivyo hakusema ni lini yatatolewa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Leandri Kinabo aliomba apewe muda ili afuatilie kujua ni kondomu za aina gani zilizowahi kukamatwa na kupigwa marufuku zisitumike.

“Nipe muda kidogo nifuatilie ili kujua zilizopigwa marufuku na ambazo tulizizuia kuingizwa nchini, nitafute mchana,” alisema Kinabo ambaye alipotafutwa baadaye alisema yuko kwenye kikao na kwamba alikuwa hajaweza kuwasiliana na watu wa maabara.

Hii siyo mara ya kwanza kuibuliwa kwa taarifa za kuwapo kwa kondomu feki nchini, kwani Desemba 20, mwaka jana kontena lililosheheni kondomu za kiume aina ya Melt Me kutoka nchini India lilikamatwa na kuzuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi.

Maofisa wa TBS walilazimika kufanya msako katika baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuziondoa kondomu hizo katika soko.

Kwa mujibu wa TBS, kondomu hizo zilikuwa na thamani ya Sh222.1 milioni na zilibainika kuwa na vitundu, zinapasuka haraka na hazikuwa na viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 820

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 28, 2013 at 10:23

koma kabisa wote waliotumia na watakaotumia maana mi nashangaaga watanzania wanavyopenda ulimbukeni bidhaa za ndani hawataki we kondom inauzwa elfu tano wakati salama zinauzwa 500 na familia 500 tena ziko nyingi.Wafe kabisa hau mamluki waliokosa uzalendo.

Comment by manka on February 26, 2013 at 11:14

HII TZ HAIISHIWI MAJANGA,.

Comment by hidaya ally mpamba on February 26, 2013 at 11:05

Hivi hili tatizo la kuingia kwa bidhaa feki ni lini litakomeshwa, maana kila kukicha bidhaa feki zinaingia nchini, mhhh haya bwana tutafika tu.

Comment by Wa Kimberly on February 25, 2013 at 13:55

Kila kukicha majanga yanaongezeka.

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 13:51

Kaka David Edson!!! Hili ni janga la jamii nzima si "mimi/wewe" ambao tunatumia hizi bidhaa.. Inakuhusu kwa njia moja ama nyingine, mfano mdogo tu ... Najua una NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.. kwa hayo makundi watatu tu kunauwezekano ambao kati wanatumia hii bidha na kwahiyo kupata madhara ambayo kwa njia moja au nyingine inaweza kukuhusu kwamfano kutoa huduma/mchango kwa atakaye dhurika na bidhaa hii. Ni kamtazamo kangu tu kaka!! Tehe

Comment by David Edson Mayanga on February 25, 2013 at 13:27

haya kwawatumiaji unajua mimi situmiagi kabisa kwakuwa nampenda mkewangu nasijawahi kwenda nje ya ndoa kati yangu namkewangu niliye naye mkewangu mama watotot wangu

Comment by Mama Malaika on February 25, 2013 at 12:47

Christer... dogo anasema kweli, huyo Trojan ni tishio kali. Ha haa haaa

Comment by Mama Malaika on February 25, 2013 at 12:46

Halafu hao wanaoluziwa yaelekea hawajui nini kinachowapeleka kwa office, wako wana rusha tu mpira.

Comment by Christer on February 25, 2013 at 10:06

Ntajuaje? mimi sio mtaalam kama wewe dogo, doh! kwaiyo kondom ina jina la kirus hahahahaaa hapo lazima itishe.

Comment by Tulonge on February 25, 2013 at 9:54

Christer kwani hujui kuna virus mmoja anaitwa Trojan? najua hata hapo kwenye computer yupo

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*