Tulonge

Kufuatia utendaji mbovu, mawaziri sasa kuchekechwa

MAWAZIRI na watendaji wa wizara mbalimbali watakaokuwa wazembe, watachekechwa na kubaki wale ambao utendaji kazi wao ni bora, baada ya kuzinduliwa kwa mpango maalumu wa kupima utendaji wa kazi wa viongozi.

Mpango huo ulizinduliwa jana jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Katika nchi za Rwanda na Malaysia, ambako mpango huo unatekelezwa, waziri anaposhindwa kufikia malengo yaliyowekwa katika wizara yake, anahesabika kuwa ameshindwa kazi na hujiuzulu.

Kwa kuanzia, wizara zitakazoanza kutekeleza mpango huo ni Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Maji.

Akizungumzia mpango huo, Rais Kikwete alisema kuwa ni busara kwa nchi kujifunza kutoka katika nchi zilizofanikiwa kimaendeleo kama Uingereza, Vietnam na Malaysia, ambazo zinatekeleza mpango huo.

Alisema Uingereza chini ya Waziri Mkuu wa zamani, Goldon Brown, ilianzisha mpango kama huo na ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Nchini Malaysia, mpango huu unafanya vizuri zaidi, waziri akishindwa kutekeleza miradi aliyopangiwa, akaitwa kwa waziri mkuu, ina maana ameshindwa kazi na hawezi kuendelea tena kuwa waziri,” alisema Kikwete.

Alisema kuwa mpango huo mpya una lengo la kutoa majukumu kwa kiongozi mmoja, mmoja ili aweze kutoa matokeo mazuri ya kazi zake na kwamba hilo ndilo litakalomfanya aendelee na wadhifa wake.

Katika tukio hilo, mawaziri wa wizara zilizo katika mpango huo walisimama na kuahidi kutekeleza majukumu yao chini ya mpango huo na kwamba hivi sasa watendaji mbalimbali wa wizara hizo wako kwenye mafunzo maalumu kuhusu mpango huo.

Akizungumza, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema kuwa mpango huo ukianza kutekelezwa utakuwa kiama kwa viongozi wapenda vyeo, wasiotekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Utafika wakati watu watazikataa teuzi za uwaziri kutokana na kazi zitakazokuwa mbele yao. Uongozi utakuwa mzigo mkubwa badala ya sasa watu wanatuambia tumeula tunapoteuliwa kuongoza wizara,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema: “Nchi ambazo mpango huo unatekelezwa, Rais anaweza kuwaomba watu kadhaa wamsaidie kuongoza wizara na wakakataa kwa sababu ya kufahamu kazi ngumu iliyo mbele yao.”

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 502

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 12:24

Napenda ile staili ya WAZIRI AKIBORONGA WIZARA YAKE ... ANAHAMISHIWA WIZARA NYINGINE... HIVYO HIVYO KWA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI... sasa naona na huu mpango mpya nadhani utakuwa UMEBORESHWA ZAIDI ILI UKIHAMISHWA KWENDA WIZARA NYINGINE UNAONDOKA NA TIMU YAKO YOTE!!!

Comment by Severin on February 23, 2013 at 18:18

Longo longo haziwezi kwisha Bongo

Comment by ABRAHAM PONERA on February 23, 2013 at 13:03

Hakuna litakaloivishwa kwa serikali hii, mawaziri wangapi wanavurunda(wanaharibu) lakini hawashughulikiwi? Mango bila utekelezaji ni sawa na kupanga kushindwa. Mbona mawaziri wengi hawafuati kasi ya jembe Dr. Pombe Magufuli? na sasa Dr. Mwakyembe? Si unaona vicheko tu hakuna utekelezaji hapo! Inatisha sana kwa Nchi yenye kila rasilimali kama Tanzania, Hiyo Malaysia ilikuwa mwishoni kimaendeleo leo imekuwa Tishio, Tanzania walaji wengi mipango mingi inaishia kwa viongozi kuchekelea wanapo haribu. Yule aliyekwenda Mwanza mgogoro wa Uchinjaji (anaitwa Wassira) ameishia wapi? Nawaambia inatakiwa msasa upite kuanzia juu mpaka chini.

Comment by Mjata Daffa on February 23, 2013 at 12:18

Hapo sawa fanya kazi baba waache waseme wewe tutakupima kutokana na matokeo, wape malengo na wakishindwa usifanye ushkaji fukuza kama ulivyo fukuza LOWASA, Mwakyembe kaonesha njia japo sisi wagongolamboto TRANI yetu bado mpaka leo, iliufanikiwe usishike mambo mengi kwa wakati mmoja mara bandari, mara Treni huku marufuku kuchimba dawa mwishowe yote hatafanikiwa nakushauri anza na bandari kisha njoo kwenye treni SLOW but SURE. Kikwete uko juu wanaokuangusha watendaji.

Comment by maryrose paul on February 23, 2013 at 11:01

DR HARISON MWAKEMBE NAOMBA UFUATILIE ILE BANDARI BUBU KULE PEMBA MNAZI KATI YA SHAMBA LAA AMADORI NA AZAM KUNA MIZIGO INAPAKILIWA NA KUSHUSWA KIALSIKU AMBAYO TUNAKOSA MAPATO ILISHARIPOTIWA SIKU NYINGI MIMI NAKUTONYA TU UIFANYIE KAZI HARAKA IWEZEKENAVYO.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 23, 2013 at 10:45

mipango mipango,kucheka cheka bila utekelezaji huku sie wengine tunaumia na kulia ni mzaa wa ajabu .tunalipeleka wapi taifa wanatuchanganya jamani .mipango mingapi tumesikia mingi mala kilimo kwanza huku njaa nchi nzima.hakuna lolote tuwang'owe ikishindikana TUNA HASI ZINAANZA MBILINGE maana watoto wa taifa hili watatulaani tukifa kwa nini hatukuchukua hatua.

Comment by ANGELA JULIUS on February 23, 2013 at 9:28

@ WAMEFURAHI SIJUI HATA WAMEFURAHI NINI BINAFSI KWANGU KICHEFUCHEFU

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*