Tulonge

Kuna utata hapa maana hakuna mtu anajua ukweli wenyewe haswa!!

Maiti hii zilkutwa katika jangwa la Sahara kwenye mipaka ya nchi ya Libya na Niger (mwanzo wa mwaka huu). Watu wameshindwa kuelewa yafuatayo:

 *Je walikua ni wale waanaotokea Nigeria na nchi jirani kupitia Libya wakitafua njia ya kuingia Italy?  au

 *Ni wale walioona vita inaanza huko Afrika ya kaskazini wakaamua kukimbia na kufa njiani sababu ya njaa,      ukame na Sandstorm?

 * Au walikua ndo wanatoroka vita na kufika maeneo hayo wakakumbana na hao watu wakawauwa?

Cha ajabu nikwamba hawana majeraha kama ya risasi au kuumizwa...ila wengi wao wamenyag'anywa viatu na mali zao...maana kawaida msafiri hasafiri mikono mitupu. na sio kwanba ni wajinga wanapita kwenye jangwa bila vyakula na mitungi ya maji!!!

Views: 515

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on December 28, 2011 at 16:29

tumuachie mungu, mungu zilaze roho za marehemu hawa,

Comment by ANGELA JULIUS on December 27, 2011 at 16:42

uwiii hata mimi sijui ukweli wenyewe upo wapi inasikitisha sana lol sina mengi

Comment by Gratious Kimberly on December 24, 2011 at 2:34

Alfani kweli   huduma ya kwanza ndio......angalia vizuri hao , utaonakuna wengine wanapita wamevaaa magwanda ya jeshi.....hapo sasa kuna utata........wasije wakawa ndo kwanza wanulizwa wenzenu wako wapi?....Hatari hapo mkuu

Comment by ILYA on December 23, 2011 at 23:23

Comment by Gratious Kimberly29 minutes ago

Ndoo hali halisi Dismasi...kuna mambo mengine ambayo yanahusu watu wenye rangi zetu....yaani huwa hayasikiki wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari...inatia hasira...grrrrrrrrrr

 

Kweli kaka G.K maana ukirudi huko nyuma ya historia utakuta waafrica wengi sana wameuliwa mauaji ya kimbari kwenye mavita ya dunia,lakini hakuna anayelipigia upatu suala hilo kimataifa na kudai haki za waliouliwa walipwe fidia kama vile kuilipa nchi fidia na vitu kama hivyo.Utasikia nchi za ulaya zikitetea waliouliwa mauaji ya kimbari wa nchi zao tu ama africa utadhani hakuna waliouliwa kinyama katika vita ya 1 na ya 2 ya dunia.Ufaransa juzi imepitisha muswaada kwamba yeyote atakayepinga kuwa Uturuki katika vita ya kwanza ya dunia mwaka 1915 haikuwaua kinyama tena kwa malaki wa Armenia hukumu yake ni kwenda jera mwaka mmoja,Uturuki nayo ikajibu mapigo kuwa haikubali tuhuma hizo,kisha ikasema na wewe Ufaransa rudi katika historia utizame maovu yako ,na wewe ulitenda jinai kama hizo huko Algeria.

 

Ningefurahi zaidi kusikia viongozi wa Africa wakitaja nao  waafrica waliouliwa katika vita hiyo ya kwanza ya dunia na hata ya pili maana Africa nayo ilikuwa mhanga wa vita hivyo.Tena wadai fidia.

Comment by Alfan Mlali on December 23, 2011 at 23:09

Hawa  nahisi walipewa sumu au kupiiziwa hewa ya sumu maana inavyoonekana walikuwa kwa wakati mmoja au unatofautiana dakika chache..Ila nimeona kuna wawili wamenusurika na walikuwa wanapewa huduma ya kwanza nadhani walieleza kilichowatokea!!

Comment by manka on December 23, 2011 at 22:54

uwiii grat, inasikitisha nimeshindwa kuangalia, kweli binadamu wamekuwa wanyama wakali siku hizi.

Comment by Gratious Kimberly on December 23, 2011 at 22:40

Ndoo hali halisi Dismasi...kuna mambo mengine ambayo yanahusu watu wenye rangi zetu....yaani huwa hayasikiki wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari...inatia hasira...grrrrrrrrrr

Comment by Tulonge on December 23, 2011 at 22:28

Aisee nimeshindwa kuendelea kuangalia hii, hata robo sijafika, inasikitisha.

Comment by Gratious Kimberly on December 23, 2011 at 21:59

Duh...yaani ukiangalia vizuri...utaona wengine wamevuliwa hadi masuruali....alafu cha kusikitisha zaidi mtu akiangalia kwa makini kuna maiti pia za wanawake....mimi nihehesabu tatu alafu ni wasichana tu wadogo wasiozidi miaka 25

Comment by ILYA on December 23, 2011 at 21:55

Da inasikitisha namna hii,binadamu mwenzako kukuchomoa roho yako na kutoweka na viatu vyako.

 

Kitendo hiki kama angelikitenda asiyekuwa binadamu kusingelikuwepo na la ajabu,lakini inashangaza sana kuona mtendaji ni mwanadamu,kwanini mtu anafikia hatua ya kuwa mnyama namna hii??,watajibu nini wauaji wakiulizwa na Mola Muumba kunako jinai zao??.

 

Kwa hakika kila anayedhulumiwa ipo siku atapata haki yake,na kila anayedhulumu ipo siku atapata majibu ya dhulma azitendazo.Usiue mwenzio ukadhani biashara ndo imekwisha,bali huo ni mwanzo wa kujiweka matatani.

 

Ingawa mtenda jinai atafanikiwa kukwepa mahakama ya dunia au mahakama ya mwanadamu lakini ajue  hawezi kamwe kukwepa mahakama ya Mwenyeezi Mungu. Ile Mahakama haikwepeki na haina uchakachuaji na haina rushwa.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*