Tulonge

Lema (Mb) asomewa shitaka na kupewa dhamana

Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa Arusha baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.

Mbele ya hakimu Devotha Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”

Hata hivyo, mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo.

Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 29 Mei mwaka huu.

Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA.

---
Taarifa hii ni kwa mujibu wa JamiiForums, MabadilikoTanzania Google Group na Facebook.


Via: wavuti.com

Views: 325

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Omary on May 1, 2013 at 3:51

Kiukweli wana nch wanachoka na kuburuzwa kila siku na ahadi za uongo unajuwa kwenye uongozi kuna vitu 3 Hekima, Imani, na Elimu sasa viongozi wetu wengi unakuta wanamapungufu hawajakidhi mahitaji ya uongozi, pia wanafanya uongozi ni sehemu ya kujitajirisha hawajui kuwa uongozi ni utumwa. Omar bin Khattab alikuwa kiongozi ilikuwa kama adhabu kwake maana alikuwa akitembea usiku na mchana kutafuta matatizo kwa watu anao waongoza ili ayatatuwe maana anajuwa majukumu alio nayo na anapaswa kufanya hivyo la sivyo adhabu kwa Mungu inamngojea ila viongozi wetu hawajali hayo wao wanaangalia leo tuh.
Hadith ya Omar bin Khattab ni ndefu na ina mafunzo makubwa sana kama viongozi wetu wangekuwa na Imani ya kidini hakika wangeuogopa uongozi, Inshaallah nikipata wasaa nitawadadavulia kama mtapenda kujuwa japo machache.

Comment by Mama Malaika on April 30, 2013 at 20:09

Sirikali ya TZ haina tofauti na Putin wa Russia

Comment by MGAO SIAMINI,P on April 30, 2013 at 8:51

kweli Lema mwanaharakati watu kama huyu ndio kiboko ya ccm vinginevyo ccm hawasikiagi

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*