Tulonge

Lindi: 9 wafariki, 30 wajeruhiwa kwa ajali ya basi

Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi. 


Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha. 

Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali. 

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ambae alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo Taarifa zaidi za majeruhi hao pamoja na maiti zilizotambuliwa tutawajuza.


Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa Maiti 9 za ajali hiyo.


Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwa

Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo wakiwa mtaroni.. Kwakweli inasikitisha sana, hiyo ikiwa ni ajali mbaya kutokea kwa januari 20 baada ya ajali nyingine mbili ikiwemo ya Noah iliyoua watu na ile ya Mbeya kugongana magari manne kwa wakati mmoja mji mdogo wa Mbalali

Views: 372

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*