Tulonge

M23 yawaambia wafuasi wasitishe mapigano

Kiongozi wa wapiganaji wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.

Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.

Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.

Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.

BBC Swahili

Views: 300

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on November 8, 2013 at 9:38
Hata mie hawa rebels siwaamini, huko nyuma waliwahi sema kauli hii. Hawatabiriki ukizingatia kuna jirani wamekuwa wakiwapa support.
Comment by Dixon Kaishozi on November 8, 2013 at 9:29

Hahahahaa.. Yani wamesha pigwa ndiyo wanajidai wanataka kusitisha na kuleta mazungumzo.. Hakuna cha mazungumzo hapa!!! Ni kichapo na kuwapoteza kabisa, maana hawatabiriki hawa.. walisha ongea alafu tena wakaanzisha mapigano upya!! Ni kuwachapa mpaka dk ya mwisho.. kwanza wamesha ua wanajeshi wetu na kuwafanya raia kukimbia nchi yao na kuwa wakimbizi.. yani naomba wachapwe mpaka wawapoteze wote!!! Pumbafu zao!!

Comment by Hashim Said on November 4, 2013 at 21:15

Hawa waasi nashindwa kuelewa kwanini jeshi la serikali likishirikiana na majeshi ya Umoja wa Mataifa bado wameshindwa kuwateka hawa wauaji!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*