Tulonge

Magufuli asema wakazi wa Kigamboni wameridhia nauli mpya za vivuko. Aliongea na mkazi gani???

Katika hali ya kushangaza waziri wa ujenzi Dk John Magufuli ameshangaza uma kwa kusema kuwa wananchi wa Kigamboni wameridhia kutoa nauli mpya bila wasiwasi wowote. Haijajulikana alipata taarifa hizo toka kwa mkazi gani wa Kigamboni. Je ni asilimia ngapi ya wakazi wa Kigamboni wamekubaliana na suala hilo.

Ni kweli wakazi wa Kigamboni wanaendelea kutoa nauli mpya kwa sababu hawana njia nyingine ya kuwavusha, haimaanishi kuwa wameridhia kutoa nauli hizo mpya. Alitaka aone watu wamekaa nyumbani bila kuvuka ili ajue kuwa wamegoma?

Wakati huo huo wabunge wa Dar wanatarajia kukutana ili kujadili suala hili la nauli na kauli yake ya kuwataka wakazi wa kigamboni waogelee kama hawana nauli. Kauli hii imeshangaza watanzania wengi wenye busara na kushindwa kuamini kama ilitoka kinywani mwa waziri wa ujenzi. Wabunge hao wa Dar wamemuomba Magufuli awaruhusu wasimamie mapato angalau kwa siku moja ili waone kama kiwango kitakachopatikana ni kile kinachosemwa na Magufuli.

Magufuli amekuwa akitetea uamuzi wake wa kupandisha nauli kwa kuwa vipo vivuko vingine nchini ambavyo vinatoza nauli kubwa zaidi ukilinganisha na vivuko vya Kigamboni. Haina uhakika kama amefanya utafiti wa umbali wa vituo vya vivuko hivyo, Idadi ya watu wanaotumia vivuko hivyo (ukilinganisha na wakazi wa Dar) na gharama zake za uendeshaji.

Hadi sasa Magufuli ameahidi kutobadilisha uamuzi wake wa kupandisha nauli kwani amefuata sheria zote katika kuamua hilo.

Views: 654

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 19, 2012 at 9:02

Pole Dismas.. najua kwa njia moja au nyingine hili la kupanda nauli ya kivuko lina kuhusu.. lakini kumbuka kuwa gharama za uendeshaji zimepanda... nauli ya sh. 100 kwa zaidi ya miaka 9? tehehehee... wakati mafuta, dola, maisha kwa ujumla yamepanda... hebu tuwe tunafikiria kwa undani na si kukurupuka.. kwenye ukweli tutetee na kwenye maovu tupige kelele mpaka mwisho... Ni wazo tu.. tehehehee usije nipiga konzi ka DON..

Comment by Alfan Mlali on January 10, 2012 at 23:55

Yap, tunatafuta mtu wa kutuonyeshea mfano ndipo na sisi tufuate....tehteheteehetehe@Gratious

Comment by Gratious Kimberly on January 8, 2012 at 18:30

Haaa alfani wewe.......kama unataka kutjioa muanga nenda kajitose, sio lazima ukae kigamboni...teh teh..au mbaka wadogo zake osama waje wwatoe mfano!!

Comment by Alfan Mlali on January 8, 2012 at 12:04

Bahati yake siku hizi siishi kigamboni..Ningefuata maneno yake yan kupiga mbizi then nikifika katikati nazama huku waandishi wa habari wakichukua picha hapo ndipo angeshika adabu na kujutia kauli yake..Tatizo bongo hakuna watu wakujitoa muhanga!!!

Comment by manka on January 7, 2012 at 19:56

mheshimiwa makufuli,misimamo yako mara nyingi haiangaliagi ubinadamu, embu basi na wewe piga mbizi  kuonyesha mfano kwa hao wasio na uwezo wa kulipa hizo nauli elekezi.

Comment by Tulonge on January 7, 2012 at 17:38

Wewe Don M ungekuwa karibu yangu NINGEKUKUNG'UTA bonge la KONZI.

Hiyo kauli ya kusema watu wa mikoa mingine wanatoa nauli kubwa haiwezi toka kinywani mwa mtu mwenye busara hata siku 1. Magufuli anaongela bei kubwa ya vivuko vya sehemu nyingine bila kusema lolote kuhusu sababu zinazoweza kupelekea bei yao kuwa kubwa. Pengine ni distance ya kituo cha kuanzia na kuishia, pengine watumiaji wa vivuko hivyo siyo wengi hivyo lazima gharama iwe kubwa ili angalau mapato yawe juu, pengine ni gharama za uendeshaji za eneo vivuko vilipo.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea viviko vingine walipe hela kubwa, ukute pia walizoeshwa hivyo toka vivuko hivyo vinaanza kazi au hata kama nauli iliongezwa kulikuwa na sababu za msingi.

Sasa yeye anasema tu eti mbona sehemu nyingine wanatoa nauli kubwa, huwwezi kutulinganisha cc na hao wa huko.

Comment by Don M on January 7, 2012 at 16:09

Mbona watu wa Dar es salaam Mna kiburi sana??? hao wengine katika mikoa mbalimbali wanaolipa nauli kubwa ya vivuko wao ni matajiri sana au?? au huko hakuna walemavu, wazee na wagonjwa?? mbona Daladala wanapandisha nauli na mnalipa? ningependa hicho kivuko kingebinafsishwa ndo mngetia adabu!!.

Comment by Gratious Kimberly on January 7, 2012 at 12:01

Huyu naye asilet magumashi hapa.....wameridhia amejua wapi au ana kimada huko Geza ulole?   Yeye anaona wanapanda feri anadhani wameridhika.  watu lazima wavike wakasake maisha hawana jinsi maana ndo njia yenyewe hiyo....Asilete zake hapa!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*