Tulonge

Majengo ya ghorofa Kariakoo yabainika kuwa na kasoro lukuki kufuatia uchunguzi uliofanywa

Zoezi lililofanywa na kampuni ya design plus ya jijini Dar es Salaam la kukagua ubora wa majengo katika manispaa ya Ilala limebaini kasoro nyingi katika majengo ya ghorofa yaliyopo katika eneo la karikaoo huku mengine yakiwa hayafai kwa matumizi ya binadamu na kupendekeza baadhi ya majengo hayo yabomolewe na mengine yafanyiwe ukarabati.

Meneja uendeshaji wa Design Plus MUSTAFA MAULID amesema kampuni hiyo imefanya ukaguzi katika maghorofa 90 yaliyopo katika kata ya kariakoo na kubaini kwamba majengo 67 yana kasoro mbali mbali za kiufundi, likiwemo jengo lililopo mtaa pemba kama anavyo bainisha Meneja huyo.Nae Mkaguzi wa majengo kutoka kampuni hiyo DENIS KILANGA amesema licha ya majengo mengi kutokuwa na ubora, pia majengo yamejengwa bila kuwepo nafasi kati ya jengo moja na lingine.

Mapema mwaka huu zaidi ya watu 36 walipoteza maisha baada ya jengo lenye ghorofa 16 kuanguka jijini Dar es Salaam kitendo kilichopelekea manispaa ya ilala kutafuta mzabuni atakaekagua majengo yote ya wilaya ya ilala na kutoa mapendekezo.

Chanzo: kibonde24.com

Views: 432

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on November 6, 2013 at 16:49
Majengo mengi yanajengwa kwa kulipuliwa. Wakuta mtu Dar ajenga ghorofa kwa kulazimisha huku pesa vifaa haitoshi ili mradi tu kuwa na ghorofa. Na siku kukitokea tetemeko la ardhi itakuwa Majanga. Na waendelee ukaguzi kwa Dar yote wasiishie Kariakoo tu.
Comment by habiba mustafa mlawa on November 6, 2013 at 8:44
mm nasema kila siku watanzania ni wavivu kufanya kazi na wanapenda sana rushwa hivi siku zoooooooooote walikuwa wapi kukagua mpaka leo majengo yanaishia eti ndo wanakagua, huku si kurudishana nyuma huku?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*