Tulonge

Dar es Salaam/Dodoma. Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.

 

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

 

Akizungumza Bungeni Dodoma usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.

 

“Tulifanya operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda. “Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”

 

Katika mdahalo uliogusa nyoyo za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.

 

Mwananchi

Views: 585

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on December 23, 2013 at 11:02

WAMEACHA MIZIGO MINGINE MLUGO,KAWAMBWA,GHASIA,CHIKAWE,LUKUVI, NA BOSS WAO PINDA

Comment by CHA the Optimist on December 22, 2013 at 20:32

Siku zote huwa nasema ukiona mtu anaishabikia CCM, kuna mawili hapo;

Kwanza, mtu huyo yawezekana ana mental disorder--kwani ana macho lakini haoni uozo unaosababishwa na serikali inayoundwa na CCM, na ana masikio lakini hasikii yale yanayotendwa na serikali hii inayoundwa na CCM.

Pili, ukiona mtu anashabikia na kuitukuza CCM lazima ana masilahi either ya moja kwa moja au ana ndugu aliyeko huko CCM ambaye huwa anampatia vijihela vya chumvi, sukari, unga n.k.

Mambo haya yaliyotokea ni ukweli usiopingika kuwa serikali hii haifai, sio tu haifa bali imekuwa haifai tangu Julius Nyerere ang'atuke.

Watanzania wakati ndio huu kwa sisi kufanya mabadiliko makubwa kisiasa. Nasema kisiasa kwa sababu siasa ndio iliyotawala kila sehemu. Ukigusa miundombinu-- siasa is there, ukigusia huduma za kijamii (maji, hospitali, shule etc)-- siasa is there. Sasa kama hatutakuwa na uongozi ulio thabiti, tutakuwa na haya mambo mpaka the coming of Jesus Christ!

Mwenye macho aone, na mwenye masikio asikie

Nahitimisha!

Comment by Mama Malaika on December 22, 2013 at 19:10
Ha haa haa haaa..... Proudly brought to you by JK from Dodoma @ CHA the Omniscient! Hata tunguri walizoficha kwa office hazikuona ndani.
Comment by Mama Malaika on December 22, 2013 at 18:29
Civil rights is not an African custom @ Abraham Ponera. Having said that ni kwamba Tanzanian government imeamua kujikosha kuchukua hatua baada ya vitendo hivyo vya kinyama walivyofanyiwa wananchi kuandikwa kwenye media za west (the Guardian, Independent & Reuters) baada ya International Human Rights kuchukizwa na ukimywa wa Tanzanian government. Nimesoma kwenye the Guardian & Independent (Britain) siku si nyingi imeandikwa kuwa "victims wengine walibakwa na wengine kulazimishwa kufanya mapenzi na wanyama huku government ikijua na imekaa kimya".
Tanzania ilipofikia ni pabaya sana.
Comment by ABRAHAM PONERA on December 21, 2013 at 20:42

Iko shida kwa watala wa Tanzania, hivi kwa nn tuite kuondolewa kwa mawaziri hao kusiwe UNAFIKI? Jamani nani asiyejua vitendo hivyo? Inaingia akilini leo kuona mawaziri hao wakiwajibishwa? kwa nn imechukua muda kiasi hiki? Napata shida sana, vitendo hivyo havikufanyika kipindi hiki cha Mkutano wa Bunge, vimefanyika muda kidogo umepita Jamani hatua zilingoja kamati ya Bunge itoe taarifa? kama pasingekuwa na mkutano wa Bunge tafsiri yake hakuna hatua ambayo ingechukuliwa. Hawa mawaziri wamefanya vitendo viovu sawa na wale ambao wizara zao zimeonesha Ubadhirifu mbona wameachwa? Mf. Ghasia na Kawambwa, mbona wabunge wamelalamika lakini hawajaondolewa? Si watetei hao mawaziri ila shida ni hatua zinazochukuliwa zinaleta maauzi, pia natamani kuona wale mawaziri walioonekana kutosimamia vyema wakiwemo hao wangeondolewa wote

Comment by CHA the Optimist on December 21, 2013 at 17:25

Mengi yamesikika, kwenye ile taarifa ya bunge ya ardhi, malisili, na mazingira inayogusa wizara nne na iliyogusa hisia za wengi waliofuatilia.

Kwa kiasi kidogo namsifu Kagasheki kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa, kwani alikuwa wa kwanza kuonesha nia ya kujiondoa au kung'atuka kabla ya kuondolewa au kung'atuliwa. Wengine (Nchimbi, na Nahodha) hawakuwepo bungeni--sijui walijua kuwa hawatapona hivyo kurudi kwenye maofisi yao kuondoa tunguri walizozificha--tehe tehe tehe). Mwingine (David Mathayo--waziri wa mifugo) akaonesha uroho wa madaraka kwa kusema kuwa kamati haikumtendea haki na mingi blah blah akifikiri atapona; kumbe "apangalo Mathayo David--Kikwete anapangua".

Kwa mara ya Kwanza namsifu Kikwete kwa uamuzi mgumu katika historia ya uongozi wake tangu aingie IKULU ya Tanzania kwa karibu miaka kumi sasa.

Ila kwa hili, hata Mizengo Pinda ilitakiwa ajing'atue, maana itafikia wakati atang'atuliwa kitu ambacho kitakuwa fedheha kwake, familia yake na hata chama chake.

Na isiishie hapo tu bali wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.

Tanzania Kwanza CHADEMA na CCM baadaye.

Mungu bariki Tanzania.

Comment by David Edson Mayanga on December 21, 2013 at 11:31

HAITOSHI HATA WATENDAJI WAO WACHINI YAO WANAPASWA KUPEREKWA MAHAKAMANI ISIISHIE HAPO TU

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*