Tulonge

Michelle Obama akionesha 'kijiwivu' kwa mbaliiii (picha 5)

Usifanye mchezo na mume wa mtu aisee. Wakati viongozi mbalimbali Duniani walipokutana kufuatia kifo cha Mzee Mandela huko Afrika Kusini, kuna kautani kalikua kakiendelea kati ya Rais Obama na Waziri Mkuu wa Denmark,Bi.Helle Thorning Schmidt. Obama alionekana akimsaidia Bi.Helle kuweka vizuri simu sikioni na pia kupiga picha bila kumhusisha Michelle.

Utani wao ulimfanya mke wa Obama kuonesha kuchukizwa, na kushindwa kujizuia kukunja uso kama uonavyo pichani. Yasemekana baada ya Obama kugundua kuna 'kawivu' kamemuingia mkewe akaamua kuhama na kumuacha Michelle akae katikati yao.

Michele akiwa kando bila amani

Obama akapunguza makeke baada ya kuanza kugundua kuna kawivu kanaendelea pale.

Mzee mzima akaamua kumuacha mkewe akae katikati ili kuepusha shari, na Michelle anaonekana kukaa mkao wa kumziba kabisa Bi.Helle asifanye mawasiliano na mumewe. Kazi kweli kweli

Views: 772

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 20:43
Ha haaa haa haaaa...Joan.
Comment by Joan on December 16, 2013 at 20:28

Mama M hapana chezea Obama, angekua single hata mimi ningejipendekeza hahhahahaaa

Siku hiyo Michelle LAZIMA alikataa kutoa mchezo, hizo hasira alizonazo ni balaa

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 14:05
Chezea mmatumbi (Barack Obama) wewe. Michelle ana kazi kweli kweli kwa mumewe. Na iwapo Obama angekuwa single mbona angewabada wengi. Teh teh teh.....
Comment by Dixon Kaishozi on December 12, 2013 at 13:59

Kweli mwanamke akiamua kukunyamazisha lazima utafyata tu.. hahahaaa walianza kwa makeke na kujipiga mapicha yakutosha.. mwisho wake sasa... hahahahahaaaaaa balaaa.. na tena angesema waondoke warudi nyumbani.. Air4c1 ingeunguruma.. hahahahahaaa

Comment by ANANGISYE KEFA on December 11, 2013 at 17:17

alijisahau kama yupo msibani, lakini nampongeza mama obama kwani ukiangalia picha ya mwisho utagundua kuwa ameishamrudisha obama msibani.

Comment by David Edson Mayanga on December 11, 2013 at 13:54

umeonaeee kumbe nawao wana wivu do

Comment by Mjata Daffa on December 11, 2013 at 8:43

mume wa mtu ni sumu

Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 8:20
Tulonge huyo wa pili yake yupo juu zaidi kidogo kwa hiyo hawapo beneti sana naona mama Uhuru Kenyatta katulia zake tuu na mumewe, ila haisaidii mzee akiamua kupata mchele toka kwa mdada mkuu wa denmark anaweza tatizo la sisi wanawake uwivi ila kiukweli hata ningekuwa mimi the same ila final conclusion ni kwamba mume wangu akiamua kusaliti anytime na mimi nipo hapohapo.
Comment by Tulonge on December 11, 2013 at 8:14

Mimi imenifurahisha picha ya mwisho jijnsi Michelle alivyomzinga huyo mama kwa kutumia bega.Yani kamuwekea kibega kabisa ili kukata mawasiliano. Ila naona bado tatizo lipo, maana upande wa pili pia naona kuna kimwana mwingine, tena paja nje nje. Obama asije akaanzisha utani na huyo tena teh teh teh. Sijui Michelle angefanyaje?

Comment by ANGELA JULIUS on December 11, 2013 at 8:06
hahahaha lol kweli picha zinajieleza ila hata ningekuwa mimi lol kawivu lazima ila ukija kwa jicho la pili haisaidii kwani mtu akiamua kutokuwa mwaminifu kwako anaweza kufanya tena na wewe mwenyewe ukiwa upo hapohapo wanazunguka tuu wakirudi wanaweka nguo zao sawa lol ha ha ha

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*