Tulonge

Morogoro: Kijana huyu ndiye aliyemuua mama yake mzazi kwa shoka

Kushoto ni kijana Frank akiwa amefungwa pingu ndani ya gari la polisi akiwa na mwili wa marehemu mama yake (picha na ).

Frank Hillary (27) kushoto ndiye kijana aliye muua mama yake mzazi kwa shoka huko Chamwino Morogoro baada ya mama yake kumwambia kuwa anatakiwa aanze kujitegemea kwani ni mtu mzima kwa sasa. Tukio hili liliwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani Frank na Mama yake walipendana sana na walikua wakiwa pamoja muda mwingi. Hadi kanisani walikua wakienda pamoja.

Kingine cha kushangaza ni pale paka wa mama huyo ambaye baada ya mama huyo kufariki alienda kulamba damu na kujilaza kichwani kwake.

Views: 639

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on March 20, 2013 at 15:55

DAH AMEWEKA HISTORIA AMBAYO HATAWEZA KUISAHAU MAISHANI MWAKE EMBU ANGALIA MWILI WA MAMA YAKE UPO MBELE YAKE NA YEYE NDO AMEMUUA DAH SINA LAKUSEMA UCHUNGU TUU KAMA MZAZI.

Comment by Mama Malaika on March 20, 2013 at 13:55

Huyu kijana alideka na hakufikiria maisha yake. Sasa ndio atajua kula kwa damu yake na jasho lake huko kwenye makazi mapya (gerezani). Watu kama huyu Frank aweza kukutumia watu wakuue wewe kaka yake au dada yake ili apate kurithi nyumba yako na mali zako kiurahisi.

 

Paka ni kiumbe chenye akili na utu kuonyesha mapenzi na majonzi kwa mtu anaye mpenda na kumthamini, hii yaonyesha marehemu alimthamini na kumpenda sana paka wake. Tatizo weusi kunako paka tunahusisha imani potofu za kichawi

Comment by Dixon Kaishozi on March 20, 2013 at 10:35

Miaka 27 bado tu anataka akae na mama yake kwa kumtegemea kwa kila kitu... Huyo mama alikuwa na upendo wa dhati kwa mwanae na ndiyo maana akamwambia kuwa sasa ni wakati wa kujitegemea..

Sasa chamoto atakiona, tayari kaisha mpoteza mama yake na jela inamuhusu maisha yake yote!!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*