Tulonge

"Mshahara wa Rais ni mil 32 kwa mwezi bila makato" Zitto Kabwe

Zitto Kabwe

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa
mwezi pasipo kukatwa kodi.


Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya
viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu,
aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.

 
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara
yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge
wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi
wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi
kutokana na usiri wa jambo hilo.

 
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao
walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho
jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya
nchi.

 
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa
sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa
wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila
kitu na serikali.

 
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais
atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu
cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea
kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.

 
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka
kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi
kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,”
alisema Zitto.

 
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha
kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka
1998.

 
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa
kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin
Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na
biashara huru.

 
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa
viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda
vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi
wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.

 
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama
fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo
kujua wataendeleza vipi.

 
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni
juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi,
na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa
Watanzania.

 
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema
imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa
kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza
mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for
social security to small holder farmers).

 
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia
uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo
yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa
wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.

 
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma
ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa
Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesebu za Serikali (PAC)
itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.

 
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh
bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua
fedha zinatumika namna gani.

 
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba
wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo
hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini. 

Chanzo: Tanzania Daima

Views: 1229

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on October 17, 2013 at 13:30
Kwenye nchi huru, yenye democracy, na yenye sirikali inayoendeshwa na open system (not dictatorship), wananchi wana haki ya kujua mishahara ya watu walio wapigia kura. Mfano mzuri ni Kenya, jirani ya Tanzania. Kipindi cha uchaguzi mkuu, kitengo kinachosimamia mishahara kilitoa/tangaza (officially) salary structure (State Officers' Salaries Bill) kwa nchi nzima kujua kiasi cha mshahara na malupulupu atayopokea mtu atayeingia baada ya raisi Kibaki, na vivyo hivyo ya deputy wake, mawaziri na wabunge.
Comment by habiba mustafa mlawa on October 17, 2013 at 12:04
anza na wa kwako kuutangaza maana hata kutaja maovu ya mwenzio unatakiwa uanze ya ya kwako kwanza kama unaweza ndo utaje ya ya wenzio kama huwezi kaa kimya sasa hapo ulitakiwa utaje wa kwako kwanza na ufisadi unaofanya ndo utaje na wa rais
Comment by Mama Malaika on October 16, 2013 at 11:01
My pleasure @ Siogopi Uchawi
Comment by Siogopi uchawi on October 15, 2013 at 23:32

@ Mama Malaika  point well taken 

Comment by Mama Malaika on October 15, 2013 at 17:36
Siogopi Uchawi... Kwanza kabisa, the United States haipo kwenye nchi nilizotaja. Pili, nafikiri hujamielewa uzuri nini namaananisha. Wale waliochukua Macroeconomics wamenielewa. Simaananishi mshahara uwe 100% of GDP, bali ni very, very, very small percent ndani ya Government Spending (G), na hiyo Government Spending ni moja tu ya variables nyingi, au niseme hiyo variable Government Spending ni very small percentage of GDP. Government spending (in economics term) yajumuisha mishahara yote ya viongozi (pia wabunge) na watumishi wote wa sirikali ikiwemo jeshi, police, doctors/nurses hadi walimu wa nursery schools, manunuzi yafanywayo na sirikali ikiwemo vifaa vya hospitals, vifaa vya shule za sirikali, vifaa vya jeshi & police, magari ya sirikali, mafuta ya hayo magari, chakula iwapo wanapata bure, bills za umeme na maji vinavyolipwa na sirikali, matibabu ya nje yalipwayo pesa ya sirikali, na mengine mengi yalipwayo pesa ya sirikali.
Ndani ya GDP kuna variables nyingi na lazima zioane, hivyo huo mshahara wa raisi sijui mbunge na posho apatazo kwa mwaka ukizizidisha na kugawa visizidi matumizi ya shule au hospitals, n.k. Kwa maana nyingine raisi akipata mshahara 32mil kwa mwezi basi hospitals kuwepo vitanda kutosha, shule mwalimu awe na vifaa kutumia kufundishia, n.k.. Na hii ndio imefanya baadhi ya nchi kuwa na tofauti inapokuja kwenye welfare system and income distribution, kuna nchi bila kuwa na pesa mkononi au insurance hupokelewi na doctor au kupewa matibabu, kuna nchi mzazi unapozaa tu waanza pokea compulsory child benefit ajili ya mwanao haijalishi uko tajiri au la, wakati nchi nyingine mtoto azaliwapo mzazi hujui utamlea vipi mwanao kwani hakuna msaada wowote toka sirikalini iwe wa malezi, afya au elimu.
Comment by Jeath Justin Prosper on October 15, 2013 at 15:10

Africa Unite.............:)

Comment by David Edson Mayanga on October 15, 2013 at 12:40

KUMBUKA KUWA MHESHIMIWA RAIS HAJAWAHI KUTANGANZA KIHIVYO POSHO ZENU WABUNGE ,IMEKUWA AJE WEWE KUMUANIKA RAISI WETU KIJANA WEQWE ZITO ?

Comment by Rahim on October 15, 2013 at 10:08
Asante sana mh. Zitto kwa kutujuza mambo mengi... hatukujua hapo awali!! Bado tumetega masikio yetu ili tusikie zaidi toka kwako.
Comment by Rahim on October 15, 2013 at 10:08
Asante sana mh. Zitto kwa kutujuza mambo mengi... hatukujua hapo awali!! Bado tumetega masikio yetu ili tusikie zaidi toka kwako.
Comment by Siogopi uchawi on October 15, 2013 at 0:07

Mama malaika umetoa wapi hizo habari kwamba mishahara inalipwa kutokana na GDP YA NCHI .SI CONDONE Rahisi wa tanzania kuto kukatwa Kodi ila nashangaa hizi opinion za watu  kama wewe sijui zinatoka wapi    (yes ni opinion ) just imagine prime minister wa Canada alipwe mshahara kutokana na GDP YA NCHI (GDP PER HEAD OR PER COUNTRY) hakuna nchi za Europe au Asia wala North America zinafanya hivyo 

Lakini sio sawa kwa Rahisi wa tanzania kulipwa pesa Hizo ukizingatia US president analipwa laki nne kwa mwaka na anakatwa tax na rahisi wa tanzania analipwa hiyo pesa bila tax ukipiga hesabu rahisi wa bongo analipwa pesa nyingi kuliko wa USA NUMBERS DONT LIE 

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*