Tulonge

Mwanza: Diwani wa CCM matatani kwa kuchana bendera ya Chadema

Diwani wa Kata ya Ngulumungu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Claud Masingija, ameingia matatani baada ya kushusha na kuchana bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Katibu wa Chadema wilaya ya Misungwi, Mussa Mwika, alidai kuwa diwani huyo alifanya tukio hilo Desemba 27, mwaka jana katika tawi moja la Chadema lililopo kijiji cha Chabusongo.

Kwa mujibu wa Mwika, diwani huyo alifanya tukio hilo baada ya kunywa pombe na kulewa ambapo alidai kuwa hataki kuona Chadema kikifanya shughuli zake eneo hilo.

"Nilipata taarifa kwamba huyu diwani siku hiyo alikuwa amelewa pombe, na alipofika katika kijiji cha Chabusongo alishusha bendera yetu na kuichana kisha akavunja mlingoti akidai kwamba hataki kuona Chadema eneo lake,” alisema.

Aliongeza kwamba tayari Chadema kimeripoti tukio hilo katika kituo cha polisi na kufungua jalada la mashtaka namba MIS/RB/1941/2012.

Mkuu wa Polisi wilayani Misungwi, Robert Kwayu, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

Kamanda Kwayu alisema diwani huyo anashikiliwa kwa muda kwa mahojiano huku upelelezi ukiendelea.

Chanzo: ippmedia.com

Views: 417

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 17, 2013 at 10:49

Hukumu imesha toka... Jamaa kahukumiwa miaka 6 jela!!!! Pumbafu zake!!!

Comment by william massawe on January 14, 2013 at 10:43

WATAFANIKIWA KUCHOMA BENDERA,LAKINI HAWATAFANIKIWA KUCHANA MYOYO YE2!!

Comment by Mama Malaika on January 9, 2013 at 13:39

Mie siko CHADEMA wala CCM lakini mtu aliyefanya kitendo hiki hafai kuongoza mtu/watu katika jamii yeyote ile dunia

Comment by mathias mwita on January 9, 2013 at 9:08

dalili za uongozi uliokosa busara

Comment by Dixon Kaishozi on January 9, 2013 at 8:49

Yele yale ya "Bange".. Huyo akilizake hazimtoshi...

Comment by David Edson Mayanga on January 9, 2013 at 0:41

hatuwezimvumilia wanachadema pia ajiulize je kunasehemu bendera ya ccm ilishawahichanwa?

Comment by David Edson Mayanga on January 9, 2013 at 0:30

huyo lazima tumkomalie

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*