Tulonge

Mwisho wa kubadili leseni kwa madereva ni Machi 31, 2013

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya zoezi la kukamata madereva ambao hawana leseni mpya ifikapo mwezi Machi mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Yusuf Salum. (Picha: Fidelis Felix/MWANANCHI)


MWISHO wa kubadilisha leseni za zamani za kuendesha magari umetangazwa kuwa Machi 31, mwaka huu na baada ya hapo hakutakuwa na ubadilishaji wa leseni hizo.

Aidha mfumo wa utoaji leseni utabadilishwa ili kubakia na uwezo wa kutoa leseni kwa madereva wanaoomba leseni kwa mara ya kwanza tu.

Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johanes Kahatano alisema hayo jana jijini Dar es Salaam na kuwataka madereva wahakikishe wanatumia muda uliopo ili kubadilisha leseni zao.

“Wananchi wote wanatakiwa kutumia muda huu wa miezi mitatu iliyotolewa kubadilisha leseni zao, ili kujiepusha na usumbufu wanaoweza kuupata baada ya muda huu kumalizika kwa sababu baada ya hapo, ukaguzi wa leseni utafanyika nchi nzima,” alisema.

Alisema kuwa Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wameboresha mfumo wa leseni za udereva na kuanza kutoa leseni za kisasa zaidi (smart card) Oktoba Mosi 2010 ili kuendana na kukua kwa teknolojia duniani.

Mfumo huo pia umelenga kuondoa leseni za kughushi, kuongeza udhibiti wa mienendo ya madereva kwa kupitia kumbukumbu za makosa zitakazotunzwa kwenye leseni za madereva, kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali pamoja na kurahisisha upatikanaji wa takwimu za madereva nchini na kuisaidia serikali kupanga mipango yake vizuri.

Zoezi la kutoa leseni mpya za udereva lilianza Oktoba Mosi Mwaka 2010 kwa awamu ya kwanza iliyohusisha mikoa (9) na machi 2011 mikoa mingine 13 ilianza kutoa leseni hivyo zoezi hilo kukamilika.

Alisema, hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana, leseni 616,349 zilizokuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya hizo leseni 135721 ni za kundi lenye madaraja C zingine 480,628 ni za makundi mengine.

Hata hivyo takwimu hizo zikilinganishwa na idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa na Mamlaka ya TRA nchini hadi kufikia Desemba 2012 vinafikia 1,164,574 hiyo inaoonyesha kuwa kuna madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni halali.

Chanzo: Habari Leo

Views: 490

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on January 10, 2013 at 22:57

Upo sahihi Mjata, unajua sirikali ya Tz ni watu wa longolongo nyingi.Kwahiyo watu huwa wanadhani ni longolongo tu, sasa wakiona wamefanya kweli ndo wanaanza kugombania.

Comment by Mjata Daffa on January 10, 2013 at 11:56

sasa utaona watu wakipigana vikumbo kugombania lesseni, wabongo bwana hawafanyi jambo kwa wakati mpaka wawekewe DEADLINE

Angalia vingamuzi watu wlitoana macho utasema hakuwa na taarifa ya kuhamia digitali tubadilike jamani

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*