Tulonge

Mzungu akamatwa na kg 4 za Cocaine Kilimanjaro.

Polisi nchini inamshikilia raia wa Lithuania kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya kokeni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Polisi Viwanja vya Ndege Dar es Salaam jana, anayeshikiliwa ni Christina Biskasevskaja (20) ambaye ni mwanafunzi, mwenye pasipoti namba LTY 231302121 iliyotolewa Lithuania Agosti 7.

Mshukiwa huyo alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) juzi saa 9.20 alasiri, wakati mzigo wake ukipita katika mashine ya ukaguzi uwanjani hapo.Taarifa hiyo fupi ilisema Biskasevskaja alikutwa na mzigo wa kilo 4.4 akiwa njiani kwenda Ubelgiji kupitia Addis Ababa, Ethiopia na ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopian.

Jeshi la Polisi halikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo ambalo ni la aina yake kuhusisha raia wa kigeni ambaye ni mwanafunzi.Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja, kuwa mwanafunzi huyo anasoma shule au chuo gani na wapi; na alikuwa nchini kwa madhumuni yapi.

Hata hivyo, inatia udadisi kuona kwamba pasipoti yake haina umri mkubwa, kiasi cha kutilia shaka kuwa huenda aliipata kwa ajili ya kuja nchini kuchukua ‘mzigo’ huo.Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza katika Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya hivi karibuni, alisema wakati mwingine hata viongozi wa kisiasa hujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuchangia kuendeleza vitendo hivyo katika jamii.

Pinda, ambaye hakufafanua kuhusu kuhusishwa kwa viongozi wa kisiasa katika dawa hizo, alitoa mfano wa Rais wa zamani wa Panama, Manuel Noriega aliyekamatwa na majeshi ya Marekani na kupelekwa nchini humo na kushitakiwa mwaka 1986.

Akizungumzia zaidi kuhusu biashara hiyo, Pinda alisema nchi inapokuwa kitovu cha dawa za kulevya, inajivunjia hadhi kimataifa na wananchi wake hushukiwa kila wanaposafiri nje ya nchi na hupata tabu katika viwanja vya ndege vya kigeni kwa kupekuliwa sana.

Alisema tatizo la dawa za kulevya bado lipo nchini na linazidi kukua kila mwaka ambapo Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama inajitahidi kupambana nalo. Chanzo: Ziro99.blospot.com

Views: 371

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*