Tulonge

Pamoja na kutimiza miaka 89, Rais Mugabe atumaini kushinda uchaguzi ujao

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kwamba ana matumaini ya kushinda katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.

Akizungumza hapo jana mjini Harare katika sherehe yake ya kuadhimisha kuzaliwa kwake ambapo amefikisha miaka 89 Mugabe amesema, anaamini atamshinda hasimu wake katika uchaguzi ujao wa rais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu na kubakia madarakani kwa miaka mingine mitano.

Aidha rais huyo mkongwe wa Zimbabwe amewatuhumu wapinzani wake kuwa, wanakusudia kuzusha machafuko ya kisiasa nchini humo kwa lengo la kumfanya ashindwe kwenye uchaguzi ujao.

Hivi karibuni Mugabe alitangaza kushiriki kwa mara ya sita katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambayo ameiongoza kwa zaidi ya miaka 33.

Via wavuti.com

Views: 445

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by emanuel Lyanga L. on March 5, 2013 at 20:42

hata kama wazimbabwe mnamtaka huyu babu mimi siwaungi mkono, akapumbuzike abaki kuwa mshauri inatosha aaaaaaaaaaaaa

Comment by Jeath Justin Prosper on March 5, 2013 at 13:12

Hata kama yeye ni Kiongozi bora na mzuri......................imetosha..................!Au mpaka awe anafanya vikao kwenye Ambulance kwa ajili ya uzee..............!kweli ,,,,,,No Hurry In Africa................Hakuna Matata..................

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 5, 2013 at 10:49

Babu huyu king'ang'anizi sema anaogopa kufikishwa mahakamani.

Comment by Mama Malaika on March 5, 2013 at 9:23

Uncle Bob anataka kuingia kaburini akiwa bado Ikulu, siajabu anaogopa kuburuzwa mahakamani kama alivyofanyiwa jirani yake babu Banda (Dr Kamuzu Banda).

Comment by Dixon Kaishozi on March 5, 2013 at 8:55

Huyu ata akipigwa ili atoke madarakani poa tu!!! Hii ndiyo shida ya viongozi wengi wa Africa. Ni ulafi wa madaraka, we na umri wote huo bado unataka nini ? Hebu toka huko EBO!!

Comment by Christer on March 5, 2013 at 8:23

Huo ni ubinafsi wewe babu, pisha vijana waongoze nchi!

Comment by ANANGISYE KEFA on March 5, 2013 at 7:13

huyu mzee anataka afie madarakani

Comment by Tulonge on March 4, 2013 at 22:58

Naona huyu mzee hataki kabisa kupumzika

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*