Tulonge

Nigeria: Chuo Kikuu cha Benin chadai kugundua dawa ya UKIMWI

Profesa katika chuo kikuu cha Benin cha nchini Nigeria amesema tiba ya Ukimwi imepatikana.Isaiah Ibeh ambaye ni Dean wa School of Basic Medical Science katika chuo kikuu hicho amesema dawa hiyo ya asili imefanyiwa majaribio kadhaa yenye mafanikio.

“Tupo njiani kuweka historia kwa maana kwamba tunaonekana kuwa na kitu ambacho kitaondoa kitu kilichoshindikana kwa muda mrefu,” alisema Profesa huyo.

“Tunaongelea ugunduzi mpya wa dawa ya kumeza iliyotengenezwa kutoka kwenye mimea nchini Nigeria kama tiba ya uhakika ya janga la Ukimwi.”

Ibeh alisema utafiti wa mradi huo ulianza mwaka 2010 na dawa hiyo imechunguzwa nchini Nigeria la Marekani.Aliongeza kuwa majaribio zaidi yanafanyika kubaini ni wakati gani mgonjwa hupona

Chanzo: bongo5.com

Views: 638

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 18, 2013 at 14:13

mi ninauelewa na utafiti wa madawa na nimefanya kazi na NIMR,huwaga kuna phase yaani stage za maendeleo ya utafiti wa dawa mpaka upate degree of confidence yenye error 0.001au 0.05 halafu ifanyiwe utafiti na WHO ndo dawa inaruhusiwa kutumika tena kwa uangalizi maalumu kwa muda waliotumia huo sasa ni uganga tu wa kienyeji tunao ujua.Watuondokee hapa alikuwepo babu loliondo watanzania wote wakamia.

Comment by Mama Malaika on January 10, 2013 at 17:30

Hawa waniacha hoi. Utafiti wa mradi umeanza mwaka 2010, leo 2013 (miaka 3) wanatuambia wamepata tiba.Toka lini research ya dawa ya magonjwa makubwa ikachukua miaka 3? Tena ugonjwa wenyewe AIDS ambao virus wana uwezo wa kukaa mwilini mwa binadamu hadi miaka 20 na kujificha?  

Comment by Longumok L. Mollel on January 10, 2013 at 15:20
hakuna jipya under the moon, yale yaleeeeeeeeee
Comment by dauson katuritsa on January 10, 2013 at 12:24

naona ni njia nyingine ya kujipatia cheap money maana za kwenye mtandao wameshajulikana hawapatagi tena wajinga wa kuwadanganya!!!!!

.

Comment by Mntambo Mburi on January 10, 2013 at 12:16

Yasije yakawa kama mambo ya jirani zetu na ile dawa ya kemron!

http://en.wikipedia.org/wiki/Kemron

Comment by lugembe on January 10, 2013 at 12:06
Au ni kama kikombe cha Babu na cha Bibi Tabora ?.
may be.
Comment by Tulonge on January 10, 2013 at 11:57

Mmmh! mimi sidanganyiki haraka haraka kihivyo

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*