Tulonge

Ona maneno ya Mwl Nyerere mwaka 1958 yanavyo husiana na mradi wa kuuzwa kwa ardhi ya Kigamboni Dar.

Hapa ndipo utaamini kuwa Mwl Nyerere alikuwa anauwezo wa kipekee wa kufikiria. Mengi aliyokuwa akiyasema kipindi kile yanatokea sasa. Mambo ya rushwa, kujilimbikizia mali nk aliyapinga sana katika kipindi cha uongozi wake. Kwa sasa mambo hayo yamezidi kwa kasi ya ajabu. Mungu angempa uwezo wa kurudi Duniani nadhani angetoa adhabu ya ajabu kwa viongozi wengi sana wa Tanzania.

Views: 1926

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on May 29, 2012 at 17:45

Mkwe wangu@ kusema ukweli,unazidi kunipa data za kisomi,kusema ukweli "How the west was lost" nikitabu nililichokipenda sana kabla hata ya kukitia machoni,natayari umenipa siri mkwe wangu ya kwanini west imelost,kumbe nikutokana na hiyo   Global Economic Boom of the 1990's.

China nayo ilikuwa kwa sasa inatamba kwenye uchumi,kutokana na uchumi wake kukua kwa kasi kila kuchapo,lakini kumbe uchumi unakua na wananchi wanabaki kuitaabika,!na sasa kwa kuwa imeelekea kufuata system ya kibepari,basi ijiandae kulost.

Na China ikisha lost bila shaka kipindi hicho kikijitokeza nitamuomba Dr. Dambisa Moyo Mtaalamu wa kiuchumi aniachie kazi niandike  kitabu nitakachokiitwa:

"The death of the Chinese Economy"

au nikiite:

"HOW CHINA WAS LOST",ingawa binafsi sio mwanauchumi,lakini ninae mkwe mwanauchumi atanipa hints nikamilishe kitabu hicho,nina imani   pointi zitakuwepo za kutosha  zitakazothibitisha China Recession inayowangojea ikiwa wataendelea kushikilia mfumo huo wa Super Power.!

Comment by Mama Malaika on May 29, 2012 at 15:44

Ha haa haa haaa.... ILYA weee.... nilijua utakipenda zaidi hicho cha "How the West Was Lost" maana wewe na west hasa USA ni paka na chui. Ujue west walijisahau sana baada ya economic boom ya 1990s. Fiscal policies walizo implement nchi nyingi EU ni mbaya kitu ambacho kimefanya nchi nyingi kurudi tena kwenye recession, na hiyo ni kutokana na tabia ya wana siasa kutopenda kushauriwa. 

China ilianza vizuri ila sasa imepotea yafata system ya kibepari (super power na kuhodhi pesa nyingi) huku inasahau walipa kodi wake. Mwananchi wa kawaida China hana social security kutosha, matibabu bila hela hapati. Maeneo ya magharibi na kaskazini mwa China watu ni masikini sana, na hata ardhi wanayoitegemea kwa mashamba waliyoimiliki vizazi hadi vizazi wengi wao wananyang'anywa kwa nguvu na matajiri wa chache waliotajirika na Chinese economic boom. Na maeneo hayo ndio yanabeba population kubwa ya China, watu vijijini hawana barabara nzuri, hawana huduma ya afya (zahanati), shule, maji ya bomba wala umeme, na ukame umefanya watu kufa njaa wengi. 

Comment by ILYA on May 28, 2012 at 23:34

Mkwe@,yaani Mwanadada huyu Dambisa Moyo baada ya mimi kutupia jicho majina ya vitabu vyake kama ulivyoyaandika hapo chini,nimemkubali moja kwa moja,! Vitabu hivyo inaonyesha kuna pointi chuma, maana ikiwa jina la kitabu tu ni noma,itakuwaje humo ndani ?!,bila shaka kuna fikra nondo tupu!.

Ninapotizama kitabu hicho kinachoitwa: "How the West Was Lost",moja kwa moja namkubali maana huwezi kitabu chako kukipa jina hilo ikiwa elimu yako ni kiwango cha kati, maana kitabu chenyewe inaelekea kuna fikra kibao za kichallenge kwa west,hivyo lazima umiliki hatua nzuri ya elimu ili uweze kuthibitisha kwa hoja zisizopingika ni Jinsi gani : -WEST WAS LOST-.!

Itabidi kitabu hichi na hicho cha Dead Aid ni visake vilipo!.

Comment by Mama Malaika on May 28, 2012 at 22:54

Usijali mkwe wangu ILYA kwa gazeti, kwani points zako umezielezea uzuri. Siku moja karibu sana kwenye events zinazotolewa na SOAS kuhusu Africa mjini London, huwa kuna mijadala mizuri sana kuhusu Africa hasa Political Economy kwa ujumla. Wote kina Prof Ali Mazrui, Wole Soyinka, Professor Tunde Ogowewo na wengine wengi wanakuwepo. Mwaka jana tulibahatika kuwa na mgeni aitwae Dr Dambisa Moyo, mwana dada mzaliwa na kakulia Lusaka Zambia (kasoma Oxford & Havard) ambaye kafanya kazi World Bank and other organizations na sasa ni world famous economist anatikisa mataifa ya magharibi kwa pia amebobea kwenye international development field.

Ukipata nafasi tafuta vitabu vyake viwili usome;

1) How the West Was Lost: Fifty Years of Economic Folly - And the Stark Choices that Lie Ahead

2) Dead Aid: Why Aid is Not Working and How There is a Better Way For Africa

 

Myself, as economist, namkubali Dambisa Moyo ni kichwa kwani hadi Queen Elizabeth II alimualika kwake baada ya kusikiliza speech yake ya nguvu aliyoitoa pale Westminster Abbey (kanisa kuu) mwaka jana kwenye sherehe ya Commonwealth iliyohudhuriwa na viongozi wa Uingereza na wale wa nchi za Commonwealth. Viongozi wa Africa wangekubali kufanya kazi pamoja na watu kama Dambisa na kukubali kushauriwa basi Africa ingekuwa mbali sana, tatizo viongozi hawapendi na matokeo yake nchi za magharibi zinafaidika sana kwa kuwatumia wasomi weusi.

Comment by Mama Malaika on May 28, 2012 at 22:06

Ushindi wachaguzi nyingi wa viongozi wa Africa sio wa kweli, iwapo ingekuwa Malaika watakatifu wa Mungu wanashushwa toka mbinguni kuhesabu kura na kutoa matokeo ya uchaguzi kwa critera zao bila mkono wa binadamu, kwa hakika matokeo ya chaguzi Tanzania 2010 yangekuwa sio yale tuliyoyasikia.

Kwenye grassroots level, kwa wengi barani Africa hasa Tanzania mojawapo iliyofanya hivyo ni policies nyingi zilizowekwa zinabana na kuvuruga mwelekeo na matumaini ya watu kiasi kwamba watu wanakufa moyo. Ndio maana nchi nyingi Africa sasa wananchi wanataka reforms (kubadili katiba) na kurudisha power kwa wananchi, hiyo itawawezesha sana wananchi kuamua nini muhimu kwa maendeleo yao, na hicho nimeona kinapiganiwa sana na wabunge wa upinzani nilipokuwa Tanzania last June (2011) ingawa sikuwa na muda wa kutosha kusikiliza bunge sababu nilikuwa busy kutembelea ndugu na jamaa kuhami misiba na kuona wagonjwa.

Comment by ILYA on May 28, 2012 at 15:28

Mkwe@ asante sana kwa pointi hiyo.wenyewe wanasema: "U made ur point!...Ni kweli kabisa Tanzania inaharibiwa na hao Greedy  Politicians.

Lakini nyuma yao kuna wanaowasaidia na kuwapa nguvu ili waharibu.! Na kuhusu hilo naweza kufunguka kama ifuatavyo: (Samahani kwa gazeti..tuvumiliane.. !)

Grassroots people mara nyingi mimi huwa nawalaumu sana,kwani asilimia kubwa katika nchi (hasa kwa nchi ya Tanzania ninayoijua mimi) ni ya watu hao wanaoishi maisha ya kiwango cha chini.Watu hao kuna hatari  wakabakia katika level hiyo miaka kedekede, wao na vizazi vyao na vitukuu vyao,ikiwa hawatakuwa makini na ikiwa watakaghafilika au kughafilishwa na kupumbazwa ili wasifuate njia muafaka za kuwawezesha kuikimbia ngazi hiyo ya chini katika maisha.!

Si sahihi kwamba watu walio wengi wanaoishi maisha ya kubahatisha,wale ambao leo anacho kesho hana uhakika!,hawana njia za kuepukana na hali hiyo,! nitakuwa wa kwanza kupinga fikra hiyo,bali naamini watu wa maisha ya chini ndio waliokuwa na uwezo asilimia 95 wa kubadilisha hali ya nchi na hatimae neema kuenea kwa wananchi wote ndani ya nchi.! Na pointi yangu kuhusu hilo inaweza kudhihiri namna hii kama ifuatavyo:

Nchi inatengenezwa na kuimarishwa na kuinuliwa kiwango cha uchumi wake  kutegemea au kupitia viongozi makini,waadilifu na wenye machungu na nchi na wananchi.Tukiitizama nchi kama Tanzania,tunakuta kwamba inao viongozi kibao wanaotosha kurekebisha uchumi wa nchi na kuifikisha Tanzania katika mustawa wa kiheshima unaokaribiana au kuwa sawa na nchi zingine zilizopiga hatua katika maendeleo.

Lakini pia si kwamba Tanzania ina viongozi wanamna hiyo walio wazuri peke yake,bali pia Tanzania ina viongozi mafisadi,wezi,walaghai,wenye ahadi za uongo,wanaojali nafsi zao na kuzitosa nafsi zingine,wanaotumia vyeo vyao kujipatia vipato haramu.....

.......Nitarudi hivi punde kumalizia fikra yangu, hivyo ...Staye tuned!

Comment by ILYA on May 28, 2012 at 15:25

Fikra yangu naweza kuikamilisha namna hii kama ifuatavyo:

Viongozi hao wa aina mbili, yaani :

1-wale waliokuwa wazuri,waadilifu,wenye nia na wanaotamani Tanzania ipate maendeleo kupitia juhudi zao na sio wapate maendeleo kupitia Tanzania!...

2-Na wale waovu,mafisadi,wenye ahadi hewa,wanyenyekevu wakati wa kuomba kura,na  wenye kuitafuna nchi(kutafuna mali za Umma) baada ya kuwezeshwa na kufikishwa katika viti vya kiuongozi kupitia kupewa kura ,....

Aina hizi mbili kwa ujumla zina nia tofauti,na haziwezi kuingia madaraka ispokuwa kupitia kura za wananchi.

Na pale mwanzo nimesema kwamba: Wananchi waliokuwa wengi ni Grassroots people,kwa maana kwamba , wanaweza kutimka kutoka level hiyo na kuingia katika High Level People,kupitia kura zao wakati wa uchaguzi wa viongozi.

Ikiwa watakuwa makini,wakazitumia kura zao kuwapata viongozi wazuri watakao wafikisha katika pointi ile waliyoikusudia kuifikia,basi kwa hakika na bila shaka watakuwa ni People of high level,lakini ikiwa watazitumia kura zao vibaya,wakashindwa kujua ni nani kiongozi afaa kuwa kiongozi wao na nani hafai kuwa kiongozi hata wa nafsi yake!, wakashindwa kujifunza kutoka kwa viongozi waliokwisha tangulia wazuri au wabaya, na wakashindwa kuutambua msemo huu usemao:

"Uking'atwa na nyoka mweusi,basi chochote cheusi ukionacho mbele yako ,ukionapo utakiepuka!"  basi kwa hakika watabakia tu siku zote kuitwa: The grassroots people!.

Greedy politicians:Hufika katika uongozi kupitia kura za watu hao wa ngazi ya chini,kwa kuwalaghai,kuwapa ahadi hewa,kununua kura zao kupitia kuwapatia vijizawadi kama vile tisheti,kofia...na watu hao kwa kuwa hawajui thamani ya kura zao basi hughafilika na kuuza kura zao kirahisi kwa kuwapigia watu wasio faa.Ambapo  kwa namna moja ama nyingine kushiriki (wakijua au bila kujua) katika ufisadi wa viongozi hao.!

Hivyo,wito wangu,ni kwa wananchi,pliz ndugu wananchi !:

pliz ndugu wananchi! ,nchi inatengezwa kwa mikono ya wananchi,na mikono hiyo ya wananchi ili kuijenga nchi  inaweza kuwa ni hao viongozi wanaochaguliwa na wanachi.Hivyo wewe kama mwananchi,tambua kwamba mkono wako ukiwa mzuri basi nchi itakuwa namafanikio,na mkono wako ukiwa mbaya,basi jua nchi inaelekea kubaya.Na ili mkono wako uwe mzuri,ni pale utakapochagua kiongozi anayefaa,ama ukitaka mkono wako uwe mbaya,basi chagua kiongozi asiyefaa,kuchagua kiongozi mbaya ni sawa na kuufanya mkono wako unaotakiwa kuwa imara ili kuijenga nchi uwe dhaifu.Na ukiwa dhaifu hakuna kitakachofanyika wakati mkono ni mbovu.

                  Na hapo ndipo utakapoitamani jana na kuitizama leo kwa jicho baya!.

Comment by Mama Malaika on May 28, 2012 at 11:36

ILYA... Tanzania na Africa nzima imeharibiwa na greedy politicians. Huwa nasoma articles za Professor Ali Mazrui wakati mwingine hadi machozi yananitoka jinsi anavyoandika. Viongozi wa sasa wako tu kama miti mikavu imesimama, hawajui nini kinaendelea ndani ya nchi zao na hawako karibu na wananchi wao hasa masikini kujua nini kinaendelea kwenye grassroots level. It's sad but true.

Comment by Mama Malaika on May 28, 2012 at 11:25

Nyerere was a true African nationalist and Pan-Africanist, he worked with the masses at the grassroots level (poor people) which most African intellectuals don't do that. Na ndio sababu aliweza sema mambo yote haya.

Hebu fikiri yule mzee tajiri wa kizaramo nimesahau jina lake (kitu kama aliitwa mzee Tambaza), kabla ya Uhuru alikuwa akimiliki ardhi kubwa tokea maeneo ya Ferry (Kigamboni) hadi Kariakoo na msimbazi yote, iwapo yeye na matajiri wengine waliokuwa wakimiliki ardhi kubwa kote Msasani hadi Kawe wasingenyang'anywa na Mwl Nyerere ingekuwaje? Masikini wangeendelea kuwa watwana

Comment by Bonielly on May 28, 2012 at 7:16

ilya umeongea kwa usahihi na umakili kwa jinsi alivyo mwalimu na ndio maana akawa mwalimu, ukifuatilia walimu wengi wanafanana, kama magufuli ni mwalimu wa kweli, unajua walimu wengi wanakuwa watu wa busara sana,

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*