Tulonge

Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja (wa pili kushoto), akipokea moja ya kamera ndogo 20 zilizotolewa kama msaada na kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa lengo la kuimarisha ulinzi nchini.

Kamera zenyewe ishirini tu jamani, hapa sasa mimi naona kuna walakini...watazichakachua hao...angalia ofisini kwenyewe wamejaa mabosi wamejifungia kufuta ushahidi. kama unabisha nenda baa za quarters kama hujakuta vimada wao wana vikamera vipya...mhhh!

Views: 765

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on January 1, 2012 at 19:39

halafu hao watu wa Puma Energy wanachekesha sijui ilikuwa ni mbinu yao kuchakachua ili wagawane na mapolisi? Tokea lini camera hizo zikatumika barabarani? Camera ya barabarani nafikiri yazidi 100x Optical Zoom, sasa hizo kwenye picha hapo juu sizani hata kama zinafikia 6 Optical Zoom.

Comment by Mama Malaika on January 1, 2012 at 19:32

Hizi camera mie nina wasiwasi baada ya miezi 3 zitabakia camera 4 tu.

Ha haa haaa...Gratious umenichekesha, ulipeleka umatumbi wako kwa wakoloni (Germany) ukifikiri hawatokushika? .... Ha haa haaaa

Dar raha yake uwe na tractor ambalo liko converted kwa kutembelea kama gari, hapo naona drivers hasa wa daladala watakuogopa kidogo na wenye magari binafsi watakuachia njia bila kupenda.

Comment by chaoga on January 1, 2012 at 9:29

nimekupata mkuu gratious....

Comment by Gratious Kimberly on January 1, 2012 at 7:39

Asante kaka Chaoga...unajua mimi nikiwa bongo huwa nakaa siku sita hadi 7 sishiki usukani......mchuzi wa kongoro na supu ya ulimi vikisha nikolea hapo ndo naingia road sasa....tehteh.  Nawachomekea hivyo hivyo wanavyo endesha maana bila hivyo inakua haiendi. Unajua kuna kipindi cha nyuma kama miaka 10 hivi iliyopita nilikua na kidaladala changu ( toyota [custom] hiace) basi madereva walinizingua kinoma ...hesabu ovyo kila siku alafu nilikua mdogo. Kila nikipata dereva mpya hadithi ndo hizo tena kidogo waniharibie hadi engine. Dereva wa mwisho alikua na umri kama wa baba yangu basi huyo ndo alikua magumashi kupita kiasi.....mwishoni nikaona ujinga...niliiingia mwenyewe raod nachapa TLB ya mwenge -kariakoo kupitia manzese.....wewe acha tu kazi hiyo ilinifundisha ujanja sana....napiga watu miswaki...nachomekea kama kawa  kisa kulamba vichwa. mwishoni nilikauza kabasi maana walikua wamekaharibu kinona kwa kupeana deiwaka...nikapanda pipa nikatabaa huku...nikasema biashara ya magari kumwachia mtu ndo mwisho , bora biahashara nyingine!!

Comment by chaoga on December 31, 2011 at 12:48

kaka gratious mchango wako nimeupenda sana,  na wewe ukija huku ukaendesha gari kwa kwa kufuata sheria za huko haki ya nani vile nakupa masaa kadhaa tu barabarani kwanza utaanza kula mitusi wewewe mwenyewe, wazazi wako hadi bibi yako..halafu sizani kama utamaliza siku bila gari lako kubonyezwa kizenji...bonyeeeeeeeeeeeeee....

Comment by manka on December 31, 2011 at 10:28

hizo ndizo zinatakiwa huku tz, maana watu wanajiendeshea tu magari hovyo, kama kipindi hiki cha sikukuu ndiyo usiseme watu wanajifanya wana ela hata askari akimkamata anamtoa na buku tano safari inasonga, na askari wetu wa kikukamata anakwambia nipe ugali kama utaki kwenda kituoni. wakiweka cctv watu watafuata sheria za barabarani na rushwa ingepunga kama siyo kwisha kabisa. lakini ndiyo hivyo wanafurahia digital za kuwapiga picha vidosho wao, badala yakuangalia mbele zaidi kwenye teknolojia zenye uhakika.

Comment by Gratious Kimberly on December 30, 2011 at 22:03

Siku moja nilijifanya kuleta ujanja wa kibongo. Basi nilimchomekea mtu alafu bahati mbaya nikamkwangua pasi pembeni ya gari lake. Kuona hivyo nikatoka baruti.  Weeeeee   jamaa hakuchelewa alipiga simu polisi (bure) akatoa namba za gari aina yake na rangi!!!....Kwani nilifika mbali, walejamaa nilipokatiza mataa wakaninasa kwenye kamera..........wakawasiliana na wenzao waliokuwa barabarani basi kwenda mbele tu kidogo nikakuta jamaa wananisubiri.....nikatolewa hadi bastola maana walidhani mimi ni mhalifu (sababu nimekimbia ajali)   Duh hadi kituoni...nikajitetea kwamba nimekimbia sababu watu pale walianza kunionyesha dalili za ubaguzi wa rangi kwahiyo ikabidi niokoe maisha yangu!!.....Hiyo faini tu ilikua Euro 1100 na hapo bado insurance ilipe gharama za kurudisha rangi kwene gari ya yule jamaa.    Usipime!!

Comment by Gratious Kimberly on December 30, 2011 at 21:52

Olivia pole...naona umetoa mchango wa mboga ya mama marwa siku ya mwaka mpya...teh

Comment by Gratious Kimberly on December 30, 2011 at 21:51

Haaaa Mzeee Chaoga na kamanda Alfani mmenichekesha kweli....alafu point zenu zina mbolea saana...kamera za traffic light ni chiboko....Yaaani madereva huku tuna adabu  na woga kwelikweli.....ukikamata usukani unashika adabu kama unaswali vile.  Hizo kamera wamefunga kwenye mataa ni chiboko...yaaani pale njano ukitaka kuwa nyeku ndo zinafanya kazi yake alafu automatic.....zinapigwa flash hapo kama 20 kwa sekunde hadi nyekundu bado zinapiga alafu zimeunganishwa ndani na speed meter....ukipita hapo na speed isiyo ruhusiwa wewe  ujue video yake utaikuta ubaoni tena bila ubishi.....Hayo makosa mawili fani yake ni chiboko haipiti siku utasikia polisi wamekufuata nyumbani. Hata ukibisha kuwa dereva alikua sio mimi itabidi umtaje huyo uliyemwachia gari...au picha zenyewe zinaonyesha kabisa nani alikua ndani ya gari. hakuna ubishi hapo!!

Comment by Alfan Mlali on December 30, 2011 at 18:47

Hahahahahha! Umeonaeeeeh...? Yaani wangepata na faida kibao tu tatizo sijui vichwa vyao vimejaa maji??? @Chaoga

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*