Tulonge

Polisi watuhumiwa kumuua mahabusu kwa tuhuma ya wizi wa taa ya pikipiki

IGP Mwema

Same. Jeshi la Polisi wilayani Same mkoani Kilimanjaro limeingia katika kashfa nzito baada ya wananchi wa mji huu kuandamana hadi kituo cha polisi kupinga kitendo cha baadhi ya polisi kumpiga mkazi wa wilaya hiyo aliyekuwa mahabusu hadi kufa.

Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa marehemu Maftaha Salimu walisema wameamua kuandamana kudai haki kwani ndugu yao alikamatwa Juni 7, mwaka huu na kupelekwa kituoni hapo na baadaye alipigwa sana hali iliyochangia kifo chake.

Dada wa marehemu, Mwanaid Salim akielezea chanzo cha ndugu yao huyo kupoteza maisha alisema, Juni 6 mwaka huu ndugu yao alituhumiwa kuiba taa ya pikipiki (bodaboda) ambapo alikamatwa na polisi kesho yake Juni 7 na kuwekwa mahabusu.

Alisema mara baada ya wao kupata taarifa kuwa ndugu yao yuko mahabusu walimtuma kaka yao na mama kwenda kumwekea dhamana na kufanikiwa kumtoa lakini alikuwa akilalamika kuwa na maumivu ya kupigwa vibaya na polisi.

“Mama alimchukua na kumpeleka nyumbani akiamini maumivu anayolalamika ni ya muda lakini kadri saa zilivyokuwa zikienda ndivyo alivyokuwa akilalalamika kuumwa na alipewa dawa za kutuliza maumivu.”

Alisema ndugu yao huyo hakuweza kutoka na badala yake alisikilizia maumivu kitandani hadi Juni 11, saa 5 usiku hali yake ya afya ilivyokuwa mbaya na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Same, lakini kabla hajapatiwa huduma alifariki dunia.

Kwa mujibu wa dada huyo wa marehemu, ndugu walikutana na kuamua kwenda polisi kujua sababu za kupigwa kwa ndugu yao na polisi kukubali mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi ili ukweli ujulikane.

Alisema waliongozana na polisi hadi katika hospitali hiyo ya wilaya ambapo mwili huo ulipasuliwa lakini cha kushangaza daktari aliyeupasua aligoma kuwapa majibu na kuwataka wakazike ndugu yao kwani majibu hawatayapata kwa siku hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Views: 358

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by mathias mwita on June 17, 2013 at 8:46

hivi utaratibu ni upi hapa, majibu kutolewa kwa wahusika siku hiyo hiyo au madaktari kujadiliana kwanza kabla ya kutoa majibu?

Comment by Danford Kyando on June 16, 2013 at 8:49
Poleni sana mungu awape nguvu! Laana itawapata hao askari waliohusika inauma sana kuona binadamu tunauana kama mbu!
Comment by Danford Kyando on June 16, 2013 at 8:45
Poleni sana mungu awape nguvu! Laana itawapata hao askari waliohusika inauma sana kuona binadamu tunauana kama mbu!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*