Tulonge

Pwani: Walimu na Wanafunzi waishi kinyumba

Imwandikwa na John Gagarini, Bagamoyo via gazeti la Majira

MWALIMU wa Shule ya Msingi Msoga, iliyopo Wilaya ya Bagmoyo, mkoani Pwani, Joel Mjema, anatuhumiwa
kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la sita shuleni hapo (jina tunalihifadhi) hivyo kushindwa kuendelea na
masomo baada ya kumaliza darasa la saba.

Tuhuma hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha pamoja kati ya wazee maarufu, viongozi wa dini, wajumbe wa Serikali ya Kijiji, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Mkuu wa Wilaya hiyo, Ahmed Kipozi.

Katika kikao hicho, mwalimu mwingine aliyefahamika kwa jina la Samwel Mjema, naye alidaiwa kuishi kinyumba na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Msoga (jina tunalihifadhi).

Ilidaiwa kuwa, baada ya wazazi wa mwanfunzi huyo kubaini mtoto wao anaishi kinyumba na mwalimu huyo, waliamua kumalizana kimya kimya na mtuhumiwa.

Akizungumza katika kikao hicho juu ya tuhuma hizo, Kipozi aliagiza walimu hao wasakwe na kukamatwa ili
wafikishwe mahakamani.

“Naambiwa mwalimu Joel Mjema pia aliwahi kumjaza mimba mwanafunzi mwingine aliyekuwa akisoma kidato cha tatu Shule ya Sekondari Lugoba (jina tunalihifadhi), kumkatisha masomo na kuishi naye kinyumba...hii ni aibu kubwa kwa mwalimu ambaye amepewa dhamana ya kulea watoto kimaadili,” alisema.

Aliongeza kuwa, mwalimu Samwel Mjema alifumaniwa na wazazi wa mwanfunzi huyo lakini cha kushangaza suala hilo limemalizwa kimya kimya kati ya mwalimu huyo na wazizi husika.

“Kitendo hiki hakikubaliki, nataka huyu mwalimu akamatwe na kuchukuliwa hatua mara moja pamoja na wazazi wa mwanafunzi kwa kufikia makubaliano ya kulimaliza suala hili jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi,” alisema Kipozi.

Alisema walimu hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikiuka maadili na kanuni za utumishi kwa kufanya ngono na wanafunzi kitu ambacho sheria za nchi na taratibu za utumishi zinakataza. Aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kuvumilia uchagu huo hasa kwa mtu anayepaswa kuheshimiwa kama mwalimu kuamua kuwashawishi wanafunzi na kufanya nao ngono. Kipozi alisema, jambo la kusikitisha zaidi ni wanafunzi hao kukatishwa masomo hivyo kukosa mwelekeo wa maisha ya baadaye.

Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa, mwalimu Swamel Mjema tayari amekamatwa kuhusiana na tuhuma hizo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati mwalimu Joel Mjema, anadaiwa kutoroka na anaendelea kutafutwa.

Views: 446

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on April 6, 2013 at 16:33

Hahahhahaahahaa eti unda tume

Comment by MGAO SIAMINI,P on April 6, 2013 at 15:33

unda tume

Comment by emanuel Lyanga L. on April 4, 2013 at 23:16

watoto wakifeli tuunde tume

Comment by Christer on April 4, 2013 at 9:46

Si wangewaweka walimu wenzao kinyumba?  Kamata wote adhabu ni haki yao.

Comment by Mjata Daffa on April 4, 2013 at 8:49

mbaya sana

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*