Tulonge

Rais wa Kwanza mwanamke aapishwa nchini Korea Kusini

Rais mpya wa Korea Kusini Park Gun-Hyeh (pichani) ameapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Seoul.

Watu elfu 70 wamehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye jengo la bunge la nchi hiyo.

Akihutubia baada ya kuapishwa, Mwanamama Park ameitolea wito Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia na kuacha kutumia vibaya rasilimali katika kutengeneza silaha.

Bibi Park ni mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini Korea Kusini na ni mtoto wa kiongozi na mwanajeshi wa zamani wa nchi hiyo hayati Park Chung-Hee.

chanzo: dewjiblog.com

Views: 438

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on February 26, 2013 at 18:17

Teh teh teh mama hilo dongo sasa. Yani mimi napenda kushinda ofcn? Una utani na Alfan, hata akipata likizo anaenda kzn kama kawa ili Boss amsifie

Comment by Mama Malaika on February 26, 2013 at 16:20

Asante Dixon, ila sio likizo muwe mnashinda kwenye stools na chupa mkononi. Ha haa haaa......

Ila sina uhakika kama Dismas atafurahia hoja hii maana anapenda sana kushinda kwa office. Teh teh..

Comment by Dixon Kaishozi on February 26, 2013 at 15:47

hahahahaa..... Kwahilo nitakupigia kura @ Mama Malaika!!!

Comment by Mama Malaika on February 26, 2013 at 15:32

Hongera bi Park Gun-Hyeh!

Dismas.. subiri tushike uraisi uone, kitu cha kwanza kuweka sheria kwa nchi nzima kwa kila baba anayepata mtoto (zaliwa) anapewa paternity leave (likizo ya uzazi) ya week mbili apende asipende. Ha haa haa haa....

Comment by manka on February 26, 2013 at 11:05

WEE NGOJA TU @ TULONGE CHAMA KITUTEUE, WANAUME MTAPA VITI MAALUM TU, TEHETEHEEE!!!

Comment by Christer on February 26, 2013 at 9:45

Hahahhahahahhhhhaaaaaaaaaa muacheni bibi wa watu jameni, kachoka hapo alipo anaomba amalize muda wake hata kesho coz ktk historia ya Tzania sijawah sikia Spika katukanwa kwa msg au simu, tatizo anaibaka katiba na muongozo haupi haki yake yuko kichama zaidi lazma akione cha mtema kuni. Hongera mama wa Korea.

Comment by Dixon Kaishozi on February 26, 2013 at 8:56

Yule wa mjengoni ndo anatokota kabisaaa!!!

Comment by Tulonge on February 25, 2013 at 22:49

Wanawake wa Tanzania mpoooo? Au mnasubiri hadi muwezeshwe. Tumewaachia mliendeshe lile jengo lkn limewaelemea.Fujo tupu, urais mtauweza?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*