Tulonge

Reli ya kati yasimamisha huduma zote za abiria kuanzia Leo!

Kutokana na mvua kali zinazonyesha sehemu mbalimbali ya Mikoa ya Tanzania, Uongozi wa TRL umefikia uamuzi mgumu na kufuta safari zote za abiria wanaotumia treni kutoka  Dar hadi Kigoma kuanzia leo tarehe 27/ 12/ 2011  hadi itakapotangazwa vingine.  Abiria waliokuwa wamekata tiketi za kusafiria wiki hii na ijayo, wametakiwa kuenda na tiketi zao katika ofisi za Stesheni masta husika ili warejeshewe pesa zao.

TRL wanasikitika na kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza!!!!!!

Hali hii imetokana na hali halisi ya mvua zinaoendelea kunyesha na habari makini zilizofikia mtandao huu juzi;

MATUMAINI ya kurejea kwa huduma za usafiri wa treni katika reli ya kati bado ni  madogo hasa baada ya kubainika kuwa  reli hiyo katika eneo la Godegode wilayani Mpwapwa, imeharibiwa vibaya.

Juzi Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu aliwaambia waandishi wa habari kuwa safari za treni zimesitishwa kwa muda kutokana na kuharibika kwa kipande cha reli kulikosababishwa na mvua.Hata hivyo uharibifu uliozungumzwa na Waziri Nundu uliongezeka baada ya mvua zingine kunyesha na kubomoa kipande kingine cha reli.

Maji ya mvua pia yalizoa madaraja na kufanya eneo lote kushindwa kupitika.Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri alikwenda Godegode ambako alijionea namna reli ilivyoharibika tena na kuondoa ndoto ya kutengemaa kwa siku saba kama ilivyokuwa ameahidi.

Akiwa katika eneo la tukio, waziri alikiri kuwa hali ni mbaya na kwamba itachukua zaidi ya wiki mbili kurudisha miundombinu katika hali ya kawaida.

Alisema hiyo pia itategemea kama mvua hazitanyesha lakini zikiendelea haikuwa rahisi kutabiri. “Hapa panahitaji kazi ya ziada tofauti na ilivyokuwa awali katika eneo hili na kipande cha stesheni ya Gulwe,kwa jumla kazi hii itachukua zaidi ya wiki mbili kama hakuna mvua lakini zikinyesha  sijui,’’alisema Nundu.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Godegode, Shukuru Mohamed, alimweleza waziri kuwa tatizo katika eneo hilo ni la muda mrefu na kwamba linahitaji ufumbuzi wa kudumu.Alisema Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwa ajili ya kujenga kipande hicho kila mwaka lakini dawa kamili haijapatikana.

Mohamed aliiomba Serikali kukubaliana na maombi ya wananchi ya kujenga bwawa kubwa la kukinga maji ili kupunguza nguvu ya maji kutoka milimani  kwenda katika Vijiji vya Lukole, Kingiti na  Iyenge.Kwa upande wake Msemaji wa Shirika la Reli Tanzania,  Mohamed Rashid alisema zaidi ya Sh 700 milioni zinahitaji kugharimia ukarabati wa kipande hicho.

Views: 498

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*