Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.
Peter ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”
Hawa jamaa ni noma.
Via: bongo5.com
Add a Comment
Kusema kweli huwezi maliza matatizo ya ndugu wote hata kama watauza samani zote! Lakini comment ya Mama Malaika imenisababisha nikawatoa thamani kabisa hawa wanadamu. Kweli mama yao mzazi anakufa wanashindwa kumsaidia "eti wako busy" Hivii.. mama yao angesema awe busy si angewatosa chooni zamani sana!! Naunga hoja ya Severin ... huenda hawa wanadamu wametoa kafara.
Ha ha ha ha ha! Mobutu Seseseko Wanzabanga, alikuwa akitunishiana misuli na marehemu Franco-moja ya wanamuziki wakubwa kabisa Afrika enzi hizo. Tuna tatizo sisi Waafrika, si bure.
Haiwezekani ndugu au mwenzako alale njaa, awe hana mavazi mazuri, awe hana elimu nzuri kutokana na kukosa ada then wewe unacheza na pesa kiasi hicho! Angalia tena michango ya harusi zetu, eti harusi ambayo ni ya siku moja, unakuta inagharmu Mil. 10, au hadi 100. Tu wepesi sana kuchangiana kwenye mambo ya anasa, kuliko yale ambayo ni muhimu zaidi. Kuna watu huwa hawahitimu course zao kutokana na kukosa ada, watu kama hawa anaweza kuzunguka nchi nzima kuomba mchango wa ada na asipate, lakini lije swala la harusi--fasta tu.
Jamani dosari zetu lazima tujikosoe, kama ambavyo tunawakosoa wengine.
That's how Afrikanz we are! Si unakumbuka Mobutu Seseseko, na wengine kama hao. Tuna roho fulani hivi ya uchoyo. Ubinafsi. Umimi. etc....
Afrikans!
Aisee! kumbe ni hivyo mama Malaika? ukute wamemtoa mama yao kafara hawa jamaa ili wafanikiwe zaidi. Kama ni hivyo, makende yao kama kengele za wachawi.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge