Tulonge

Samani za P.Square ndani ya jumba lao jipya ni balaa, ni za dhahabu.

4eb1c8da43d911e3bc6522000ae91414_8

Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.

3799cde443d611e3be7422000a9e0172_8

Peter ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’

8300d71043da11e399e522000a9e28c4_8

Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’

7493d06843dc11e3a21b22000ae913ab_8

Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”

Hawa jamaa ni noma.

Via: bongo5.com

Views: 1287

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Zainabu Hamis on November 3, 2013 at 18:25

Kwa maoni yangu, ni kwamba hii si sahihi kwa wao kumiliki samani za dhahabu ilihali wana ndugu waishio katika lindi la umasikini-hata kama si ndugu zao, kuna Waafrika wenzao ndani ya Nigeria waishio katika umasikini wa hali ya juu. Ingekuwa ni vyema iwapo hizo samani zao wangeziuza na kuzigawa kwa masikini. Siungani na Jeath Prosper. Ni mawazo tu jamani!

Comment by Jeath Justin Prosper on November 3, 2013 at 12:43

...Kimsingi Maisha ni Sasa na si baadaye. Mungu alisema kwenye maandiko yake matakatifu....Ombeni Mtapewa..........na akasisitiza tena....Mapenzi yako huko Mbinguni yatimizwe hapa Duniani....hii inamaanisha mema yote yapaswa kuwa hapa Duniani......Waalimu wetu wa Makanisani wanasema kuwa mema yako Mbinguni....lakini ukweli kimantiki ni kuwa mema yako hapa Duniani...kule mema ya Nchi na si Mbinguni.


Hivyo kwa hawa mapacha wamefanya mapenzi ya mbingini hapa Duniani......

Big Up kwao......wanafanya kazi kutimiza ndoto zao.

Ikiwezekana waweke Mabati ya Diamond..halafu waajiri jeshi la Al Shabibi kulinda nyumba yao ili jamaa wasiingilie kuvunja.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*