Tulonge

Serikali ya Awamu ya Nne yaongoza kukopa

TAASISI isiyo ya kiserikali ina yojishughulisha na masuala ya Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema Serikali ya Tanzania ndiyo inaongoza kwa kukopa zaidi, ikieleza kuwa kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2011, imekopa kiasi cha Sh15trilioni na kufanya deni la taifa kufikia Sh21trilioni.

Rais Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005, baada ya rais aliye mtangulia, Benjamin Mkapa kumaliza kipindi chake cha uongozi wa miaka 10 kilichoanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.

TCDD imebainisha kuwa Serikali inakopa fedha hizo kutoka Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii. Pia inakopa katika taasisi za kimataifa ikiwamo, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Hebron Mwakagenda, alisema kuwa kite ndo cha Serikali kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo muhimu pamoja na kuwalipa watumishi wake mishahara, ndiyo sababu ya kukua kwa deni hilo la taifa.

“Serikali ya awamu ya nne imekopa kwa kiwango kikubwa, kwani tangu iingie madarakani imeshakopa Sh15trilioni, sasa sijui mpaka inamaliza muda wake itakuwa imekopa kiasi gani?” alisema Mwakagenda akihoji na kuongeza;

“Hata kama kukopa ni kuzuri basi tukope na fedha tuzifanyie mambo ya maana hasa katika maendeleo, tukope tu pale inapokuwa lazima kufanya hivyo.”

TCDD imeeleza kwamba hali hiyo ni hatari, hasa ikizingatiwa kuwa miaka kadhaa iliyopita, Tanzania kupitia Mpango wa Nchi Maskini zenye Madeni Makubwa (HIPC), ilifutiwa kiasi kikubwa cha madeni, lakini sasa imeanza kukopa tena na deni kukua kwa kasi.

Taasisi hiyo pia imesema kitendo hicho kimechangia kuporomoka kwa uchumi wa taifa kunakosababishwa na riba kubwa za mikopo hiyo, ambapo kulingana na idadi ya Watanzania ukigawanya deni hilo kwa wote, inaonyesha kuwa kila Mtanzania anadaiwa wastani wa Sh450,000.

Mwakagenda, ambaye taasisi yake inafanya kazi ya kuishauri Serikali katika suala zima la deni la taifa na maendeleo, alisema hadi kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9 trilioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyoitoa bungeni mjini Dodoma mwaka jana, taifa linapoteza Sh3 trilioni katika ukwepaji wa kodi na ubadhirifu, huku akishauri kuwa mambo mawili yakifanyiwa kazi deni hilo litapungua au kumalizika kabisa.

“Deni linakuwa kwa kiasi kikubwa na tunakopa katika mabenki ya biashara, ambayo riba yake ni kubwa, fedha nyingi zinazokopwa hutumika kulipa mishahara,” alisema Mwakagenda.

Alifafanua kwamba mwaka 2007 hadi 2008 deni la taifa lilikuwa Sh6.4 trilioni na kwamba, kuanzia mwaka 2007 hadi 2011 deni hilo limeongezeka hadi Sh21 trilioni.

Soma zaidi: mwananchi.co.tz

Views: 327

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 24, 2013 at 18:00
Longolongo tu, hiyo mikopo mishahara ukute yote yaishia posho za wabunge, malupulupu ya vigogo na kulipia shule za watoto wao wanaowapeleka abroad, na nyingine zafichwa Switzerland.
Comment by Mama Malaika on February 24, 2013 at 17:49
Sasa hizo hela wanazokopa wanafanyia nini iwapo huduma za jamii hoi bin taabani? Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi. Mnapoka hela nyingi kwenye hizo benki za biashara wakati TZ ina wa dhahabu na malighafi nyingi, inakuwa kama nchi za ulaya masikini wa malighafi. Fukuzeni wawekezaji simamieni wenyewe mining sector mna gold reserve ya kutosha kuitumia for exchange kwa hizo bank kupunguza deni. Sirikali ijifunze toka China, wanakusanya Africa na kuitumia
Comment by MGAO SIAMINI,P on February 23, 2013 at 23:43

Huyu jamaa akiondoka atatuacha tukiwa taabani, ukimkuta na serikali yake wanavyojisifia kujenga balabala utakoma.Yaani hii ni sawa na baba mwanyefamilia ya chini ya dola moja umsikie anajisifia kujenga nyumba ya mkopo wa CRDB halafu hana hata kazi wala chanzo cha mapato eti kisa anakopesheka.Ndo maana tunashindwa kujiamulia mambo yetu kisa masharti ya mideni na misaada tunayo ombeleza.Tunatakiwa kujisifia maendeleo yanayotokana na nguvu zetu wenyewe.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*