Tulonge

Serikali yaonya wanaojipenyeza kwenye kambi za waathirika

 

Ofisi ya Waziri Mkuu imewaonya viongozi wa serikali za mitaa iliyokumbwa na mafuriko kuacha kusajili watu hewa kwa lengo la kuwawezesha kupata viwanja vya bure vinavyotarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha, serikali imesema haitawavumilia watu wanaojipenyeza katika makambi ya waathirika ili kupata huduma za chakula, mavazi na vitu vingine vinavyoendelea kutolewa na wahisani, ikisema imeandaa utaratibu makini na watakaobainika watashtakiwa mahakamani.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa, alitoa onyo hilo alipotembelea kambi za Hananasif katika manispaa ya Kinondoni na Mchikichini Ilala kuwapa pole waathirika na kukabidhi misaada mbalimbali.

Majaliwa alisema vitendo vya baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa kujihusisha na uandikishaji waathirika hewa hauwezi kuvumilika na kuonya kuwa, watakaobainika watashughulikiwa kikamilifu.

"Serikali pia imepata taarifa za kuwepo kwa baadhi ya watu wanaojiita wahuni wanaojipenyeza katika makambi hayo kwa lengo la kupata misaada mbalimbali inayotolewa na serikali kwa kushirikiana na wahisani, tukibaini hilo pia tutaonyesha mfano," alisema.

Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, alisema serikali kamwe haiwezi kuvumilia kuona watu ambao sio waathirika wanaleta mzaha katika makambi yaliyotengwa akisema hatua hiyo ni sawa na kuwadhihaki walengwa.

"Ili kufanikisha hili, kwa kiasi kikubwa serikali inawategemea sana nyinyi waathirika mtuambie ni nani kati ya watu mlionao ambaye siyo mwenzenu. Hii ni kwa sababu kabla ya tukio hili mlikuwa mnaishi pamoja, tusaidieni kuwabaini wavamizi hao ili huduma zinaoelekezwa kwenu ziweze kukidhi mahitaji," alisema.

Akiwa kituo cha Hananasif, Majaliwa alishiriki tukio kubwa la taasisi ya Kiislam ya KSI Jamat kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali zikiwemo marobota ya nguo za mitumba, maziwa, chakula, maji, juisi na vyandarua.

Pale Mchikichini, Majaliwa alishuhudia taasisi hiyo ikigawa chakula cha jioni kwa wahanga zaidi ya 1,200 ambapo Rais wa KSI Jamat, Shiraz Walji alisema mbali na chakula, taasisi yake imeunda kikosi kazi maalum cha kujitolea kilichopiga kambi katika vituo hivyo kutoa kila aina ya msaada

Views: 320

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on December 28, 2011 at 21:04

Ha ha ha Boniely

Comment by Bonielly on December 28, 2011 at 15:43

Hilo hata ulaya lipo, watu wanazamia kwenye ndege sembuse hapo kwenye mafuriko,

Comment by Agnes Nyakunga on December 28, 2011 at 9:21

ni  lazima wazamiaji watakuwa wengi si unajua kwenye msafara wa kenge na vyura wamo pia!

Comment by Tulonge on December 27, 2011 at 16:00

Kufa kufaana mazee. Wabongo hatuna huruma

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*