Tulonge

Serikali yapiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko ya plastiki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira,Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake jijini dar es salaam leo kuhusu tamko la serikali la upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchi.(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)Na Ofisi ya Makamu wa RaisSerikali

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais (mazingira) Dk Terezya Huvisa amepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko ya plastiki nchini.


Dkt. Hufisa ameeleza kuwa Serikali imeamua kuchukua hatua hii ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa mazingira .


Alisisitiza kuwa, Zuio hili linahusu mifuko yote ya Plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni mia moja inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbali mbali kama vile vifaa vya mahospitalini.


“Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira.” Alisema.
Amesema jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa, na misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii ifanyike katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kufanikishwa katika vyombo vya sheria.

Madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama ,kutooza kiurahisi wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira.

Via: othmanmichuzi.blogspot.com

Views: 346

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by salum kitila on September 6, 2013 at 18:16

yap 

Comment by Mama Malaika on August 15, 2013 at 18:52
Safi sana..

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*