Tulonge

Serikali yatangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza mwakani kutokana na matokeo ya darasa la saba ambapo wanafunzi 427,60 kati ya 844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .

 

Jumla ya wanafunzi 844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.

 

Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.

 

Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.

 

Chanzo: ITV

Views: 1560

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*