Lile tukio la mtoto Guo Bin kung'olewa macho huko China tarehe 24 Agosti 2013 limeendelea kushika kasi baada ya Shangazi wa mtoto huyo Bi Zhang Huiying kushukiwa kuwa muhusika wa tukio hilo.Mtandao wa 'Xinhua' wa China uliripoti kuwa siku ya tukio mwanamke ambaye hakutambulika alimvamia mtoto huyo na kumng'oa macho. Baadae polisi walikuta macho ya mtoto huyo karibu na eneo la tukio yakiwa hayana mboni na hivyo kuashiria ulanguzi wa viungo vya kinadamu.
Siku sita baada ya tukio shangazi wa mtoto alijiua mwenyewe kwa kujitumbukiza kisimani.
Katika kuchunguza zaidi chanzo cha tukio hilo polisi walikuta nguo za shangazi wa mtoto zikiwa na damu, hivyo kuanza kuhisi anaweza akawa muhusika.
Hata hivyo wazazi wa Guo ambao ni wakulima walisema kuwa hawakua na ugomvi wowote kati yao na shangazi wa mtoto.
Mtaalam wa macho Hong Kong alijitolea kumtibu mtoto huyo bure, na kama itawezekana watamuwekea macho ya bandia (electronic eyes) ambayo yatamuwezesha kuona mwanga na maumbo ya vitu.
Kwa sasa Mtoto Guo anaendelea na matibabu hospitali. "Anaonekana mwenye furaha licha ya kukumbwa na mkasa huo, ni mvulana jasiri sana" alisema mmoja wa madaktari.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge